KIWANGO CHA MUNGU.
Na Apostle Darmacy.
Somo hili la kiwango cha Mungu ni mfululizo wa masomo mengine mengi
yanayofanana na kurandana nalo. Na katika utangulizi au mwanzo wa somo hili
tutaangalia juu.
SEHEMU 1
KUTUNZA KIWANGO CHA MUNGU KATIKA MAISHA YETU
Tuanze kujifunza somo hili kwa kuangalia
Malaki 3:6 katika mistari
hii ya malaki tunaona kuwa Mungu habadiliki ni yeye yule jana leo na hata
milele. Hivyo bali kiwango chake lazima kiwe kile kile jana leo na hata milele.
Kiwango tunaweza kukilinganisha na bendera kuwa bendera inaweza kuwa
inatangaza jambo Fulani linaloeleweka kadhalika na kiwango. Hivyo katika masha
yetu ili kutunza kiwango cha Mungu hatuna budi kuishi maisha ya haki.
SEHEMU 2
KUTUNZA KIWANGO CHA MUNGU KATIKA UTAWALA NA SIASA
Tuendelee kuangalia somo hili la kiwango cha Mungu hata ndani ya utawala na
siasa. Na kwa kuanza basi tuangalie mistari ifuatayo:
2Nyakati 26: 1-5,
16-19
Katika mistari hiyo hapo juu tunasoma juu ya mfalme uzia, aliyefanywa mfalme
akiwa na umri mdogo sana baada ya kifo babaye. Mfalme huyu alimtafuta Bwana
sana na kutaka kujua mapenzi ya Mungu kwa kufanya hivyo Mungu alimfanikisha sana.
Hali hiyo ilimfanya mfalme huyu kuwa na kiburi machoni pa Bwana na hata kufanya
kazi asizotakiwa kufanya kama kufukiza uvumba.
Mfalme huyu alikataa hata kuwatii makuhani ambao ndio waliwekwa wakfu kwa
ajili ya kufukiza uvumba. Adhabu yake ilikuwa ni kupigwa ukoma tena mbele ya
wale makuhani. Mfalme huyu ni mfano wa wafalme au waliopewa madaraka kisiasa
wakaonywa na kuadhibiwa kwa kutotunza kiwango cha Mungu katika utawala wao na
kisiasa.
Sasa tuangalie tena katika
Mithali 8:15 Katika mistari hii ya mithali
tunaona kuwa msaaada wa wafalme upo kwa Bwana. Pia na wahukumu kwa msaada wake
wanahukumu kwa haki. Hili ndilo suala la kuwanusuru viongozi na watawala. Mungu
anaendelea kututahadhalisha juu ya kutotii na kutokutunza kiwango chake katika
utawala na siasa.
Daniel 14 :32 Pia yeye ndiye muweza wa yote anayeweza hata
kuwaondoa na kuwaweka viongozi.
Daniel 2 :21. Katika suala zima la kiutawala na kisiasa jambo
muhimu la kuangalia ni vipi unatembea na Mungu wako na kipimo cha kuangalia uko
vipi kiroho ni pale mambo yako ya kimwili yanapoanza kuenda kombo. Hapo ndipo
utakapotakiwa kujipeleleza zaidi kiroho. Na utakapo-gundua kosa mara moja
ukatengeneza ndipo hata utawala wako utakapokwenda sawasawa.
2Wafalme 21
:1-6,16. Hivyo masuala ya siasa na ya kiroho ni pande mbili za shilingi.
SEHEMU YA 3
KIWANGO CHA MUNGU CHA KINABII KATIKA MAISHA YETU
Sasa hebu tuangalie kiwango cha Mungu cha kinabii katika maisha yetu
Luka
13 :31-35 Katika mistari hii hapo juu tunaona juu ya Yerusalemu awauwaye
manabii.
UNABII Ni ujumbe unaotumwa na Mungu kwa kusudi
maalumu kati ya watu wake. Unabii unapotoka unalenga kurekebisha kuonya,
kukosoa na kukemea.
Sasa tuangalie tunaitikia vipi :
CHANGAMOTO YA KINABII
Katika somo hili tunakusudia kuangalia kitu cha kufanya unapoletewa unabii
au neno la Bwana. Katika jamii ya kinabii ni lazima pawepo na watu wanaopenda
kutunza kiwango cha Mungu na wanaopenda kweli na kuishi katika hiyo.
MATATIZO KATIKA KUPOKEA NENO LA KINABII.
Kuna baadhi ya matatizo yanayofanya neno la kinabii kupokelewa tofauti na
lengo au kusudi lake. Baadhi ya matatizo hayo ni kama
I) Kukubaliana na kila kinacholetwa mbele zetu kama neno toka kwa Bwana na
hivyo kuangukia katika mikono ya manabii wa uongo.
II) Kuishi na hofu ya kudanganywa na manabii wa uongo na hivyo kukataa hata
neno ambalo lingeweza kutusaidia. (yaani neno halisi la kinabii).
III) Kushindwa kulipima neno la Bwana na hivyo kuchanganyikiwa na kuitikia
vibaya ujumbe wa kinabii. Hivyo ili kukabiliana na shida namba (I) na II hatuna
budi kujua jinsi ya kupima unabii au ujumbe wa neno la Mungu ili tufahamu ikiwa
ni wa kwake au la.
SULUHISHO.
Kabla ya kuchukua hatua yoyote unapoletewa neno la kinabii au ujumbe wa neno
la Mungu ni kulipima neno hilo.
1Yohana 4 :1 Wapenzi msiiamini kila roho bali zijaribuni hizo roho
kwamba zimetokana na Mungu kwa sababu manabii wengi wa uongo wengi wametoka
duniani na tena, ujaribuni mambo yote, lishikeni lililo jema.
1Thesalonike 5 : 21 Hivyo tusipolipima neno hilo tunafanya dhambi,
maana dhambi ni uasi na uasi ni kutotii au kukiuka maelekezo
JINSI YA KUPIMA NENO/ UNABII
Ili tupime neno tunahitaji kipimo na kipimo kinategemea kiwango cha kibiblia
maana unabii hautaletwa popote na kwa mapenzi ya mwanadamu bali wanadamu
walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na roho wa Bwana
2Petro 1.21.
Mtume Paulo akisisitiza kwa watu wa korintho kupima kwanza neno la kinabii
na sasa tuangalie vipimo vya kipimia neno linalotoka kwa Bwana.
Je unabii unapatana na maandiko au neno la biblia ?
Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya wanadamu bali wanadamu
walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na roho mtakatifu. 2Petro 1 :21
Neno linalotujia lipatane na yale yaliyokwisha kuandikwa katika Biblia.
Mfano kuna watu walipata unabii kwa tarehe fulani wapande mlima na kukutana na
Bwana Yesu na kuwa ndio siku ya unyakuo. Lakini tayari Biblia inaeleza wazi
kuwa
Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye hata malaika
walio mbinguni wala mwana, ila Baba peke yake Mathayo 24 :36
Je unabii unaimarisha agano lake na Mungu. Au watupeleka mbali na Mungu ?
Kukizuka katikati yako unabii akikutolea ishara au ajabu ikatukia
akisema tuitumikie hiyo wewe usiyasikilize maneno ya nabii yule na yule nabii
au yule mwotaji wa ndoto na wewe... Kum. 13 :1-5
Sisi tuna agano la kumwishia Bwana na kutembea pamoja naye. Hivyo hakuna
ujumbe toka kwa Bwana. Unaweza kutuhimiza au kusababisha tuvunje agano naye na
kuiandama dunia. Hivyo hakuna Mungu wa kuongea jambo kisha akajikanusha.
Je lile neno au unabii linatupa hiari ya kuamua au linatulazimisha kwa vitisho
?
Basi Bwana ndiye roho walakini alipo roho wa Bwana ndipo penye uhuru
2Korintho 3 :17.
Je lile neno au unabii linatupa hiari ya kuamua au linatulazimisha kwa
vitisho ?
Basi Bwana ndiye roho walakini alipo roho wa Bwana ndipo penye uhuru
2Korintho 3 :17. Pamoja na faida kubwa iliyopo ndani ya wokovu bado Mungu
amewaacha wanadamu kuamua au kumpokea Bwana Yesu awaokoe au kumkataa, wakaenda
motoni. Hata katika mambo mengine Mungu anayoyafanya na sisi anatuacha tuchague
kumtii yeye anachosema au la, hatulazimishi. Mungu anachofanya katika maisha
yetu hukiweka katika mioyo yetu ili tukifanye kwa hiari yetu tukihimizwa tokea
ndani.
Kwa maana Mungu ndiye atendaye kazi ndani yenu ili kutaka kwenu na
kutenda kwenu na kulitimiza kusudi lake jema Wafilipi 2 :13
Ukiona mtu analeta neno na anakulazimisha kutii weka alama ya kuuliza. Au
ukiona mtu analeta ujumbe katika hali ya utisho na kudhoofisha nafsi yako ya
kuamua kutii au la basi jua hapo kuna tatizo.
Je neno lililosemwa linatimia ?
Ikiwa Bwana amesema jambo atalitimiza yeye hawezi kusema uongo. Ikiwa neno
lile lina masharti basi masharti yake yakitimizwa litatendeka kama Bwana
alivyosema.
Nawe ukisema moyoni mwako tutajuaje neno alilolisema Bwana ? atakaponena
nabii kwa jina la Bwana lisifuate jambo like wala kutimia hilo ndilo neno
alilolinena Bwana .... Kumb. 18 :20-21
Ukiona mtu aliyeleta neno wakati fulani anakupa maelezo ya kutetea kwanini
jambo alilisema na lile neno halikutimia jua halikutoka kwa Bwana. Maana Bwana
hahitaji kutetewa na mtu.
Je neno au unabii unapeleka utukufu wapi ?
Ikiwa linakujia neno ambalo utukufu na heshima haiendi kwa Yesu bali inaenda
kwa mtu kikundi au dhehebu uwe mwangalifu na neno hilo. Ukiona unapata neno la
kuinua mtakatifu hakuhusika katika shughuli hiyo. Yesu alipoeleza wanafunzi juu
ya ujio wa roho katika
Yohana 16 :14 Anasema yeye atanitukuza mimi, kwa
kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari kwa hiyo nawaarifu ya
kwamba hakuna mtu aliye katika roho wa Mungu kusema Yesu amelaaniwa wala hawezi
mtu kusema Yesu ni Bwana isipokuwa katika roho mtakatifu
1Wakorintho 12.3 Ukiona mtu anakuletea neno huku akitaka umaarufu
na ubora alio nao jua mtu huyo anajitafutia utukufu. Wengi wa hao hupenda
kutumia unabii kuwafanya watu wamwandame na kumsikiliza. Watu wa jinsi hii ni
hatari katika mwili wa kristo.
Je maisha ya mtu yana matunda ya tabia njema ya kikristo ?
Bwana yesu akitaadharisha juu ya manabii wa uongo alisema mtawatambua kwa
matunda yao.
Mathayo 7 :15-16. ikiwa mtu anayeleta neno la Mungu kwake
anaishi katika dhambi na hafanyi jitihada yoyote kuishinda na kuitubu
usikubaliane na neno lake. Maana kama kweli anasikia toka kwa Mungu angesikia
neno la Mungu kwa ajili ya maisha yake na hitaji lake la kutubu.
Ushuhuda wako wa ndani unasemaje ?
Roho mwenyewe ushuhudia pamoja na roho zetu Warumi 8 :16 na tena ;
Na
amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu ndiyo mliyoitiwa.... Wakolosai 3 :15
Pamoja na mambo mengine yote jua kuwa Roho mtakatifu anawasiliana nawe
kupitia katika roho yako ikiwa umezaliwa mara ya pili. Neno la Mungu
hutufundisha kuwa roho ya mwanadamu ni taa ya Mungu na pia kwa vile tumezaliwa
upya katika roho zetu inakuwa rahisi Roho mtakatifu kuleta ujumbe katika roho
zetu kama kuna amani moyoni na ujumbe basi usiutelekeze na kama huna amani nao
chukua muda uombe ili kujua kwa nini huna amani nao.
Haya ni kati ya mambo ya kukusaidia kupima. Kuna mengine zaidi ambayo
tutayaangalia katika masomo yanayofuata lakini haya tu ukiyatumia tayari
yatakunusuru na ajali nyingi za kiroho.
JE UNAIPONYA NAFSI YAKO AU UNAIANGAMIZA ?
LUKA 9 :23-25 "Akawaambia wote, mtu yeyote akitaka kunifuata na
ajikane mwenyewe ajitwike msalaba wake kila siku anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye
kuiponya nafsi yake ataiangamiza na mtu atakaeiangamiza nafsi yake kuwa ajili
yangu ndiye atakayeisalimisha. Kwa kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote
kama akijiangamiza au kujipoteza mwenyewe?"
Maneno haya aliyasema Yesu mwenyewe na kufaa kama njia kwa mtu yeyote aliye
tayari kumfuata ajitwike msalaba wake kila siku na amfuate. Haya ni masharti ya
Yesu kabla ya kuondoka. Inaweza kukufikirisha kuwa unaiponya nafsi yako kumbe
unaiangamiza.
Bwana Yesu anasema kuwa anayetaka kumfuata ajikane. Hapa kunaweza kuwa
kumkana mwenyewe maana ile ya kwanza inaweza kufanana kabisa na ile ya Yuda
Iskariote ya kumkana Bwana Yesu. Yuda alijikana mwenyewe kumjua Bwana Yesu.
Lakini maana ya pili ni ile ya kukataa mambo unayoyapenda wewe mwenyewe
kuyakataa kwa ajili ya Bwana yaani kuacha vyote. Unasikiliza Bwana wako anasemaje
hata kwa vitu vyako mwenyewe. Kwa mfano una gari lako lakini hulitumii
upendavyo bali Bwana apendavyo. Bado unaweza kuwa na pesa ni zako mwenyewe.
Tunaweza kupata mfano mzuri kutoka kwa mtumwa na Bwana wake. Mtumwa sharti
asikilize Bwana wake anasemaje, akiona kama muda huu autumie kulala Bwana wake
anasema kachote maji na anakubali kwa kuwa ni Bwana wake amesema.
Yesu mwenyewe ni kielelezo cha haya yote hata yale aliyoyataka kuyafanya au
jinsi alivyopenda mwenyewe hakufanya ila alimwacha Bwana yaani Baba yake na
mara zote alikiri kuwa mapenzi yako yatimizwe.
Wafilipi 2 :5-8 Katika mistari hii tunaona kuwa Yesu mwenyewe
alijifanya si kitu akanyenyekea hata mauti ya msalaba. Ndio maana anasema kuwa
yeye anayetaka kumfuata na ajitwike msalaba wake kila siku amfuate. Msalaba
hauna maana ya ugonjwa wa muda mrefu kama wengi walivyozoea kusema.
Msalaba una maana kuomba ni ishara ya maumivu.
Kati ya watu tunaowaona kuwa ndio kielelezo cha kubeba msalaba katika Biblia
ni Yusuph, Daniel, mwanamke mjane wa serepta, watu hawa walijikana walijitwika
msalaba wao wenyewe.
Mungu anasema kuwa kuna faida gani mtu kuupata ulimwengu na kupoteza nafsi
yake mwenyewe. Hakika hakuna faida yoyote.
JE UNAIPONYA NAFSI YAKO AU UNAIANGAMIZA
Luka 9 :23-25 Yesu alisema maneno hayo alipokuwa anakaribia kuja
msalabani. Alisema kama mtu anataka kumfuata yako masharti ni lazima aikane
nafsi yake na ajitwike msalaba wake kila siku amfuate
Masharti ya ufuasi ni : Masharti ya ufuasi ni :
-Kukana ni kukataa hadharani
- Kukana ni kuukataa ubinafsi
- Kukana ni kutoa maisha yako na kumpa Yesu ili ayatawale.
- Kukana ni ile hali ya kushinda mapenzi yako ya binafsi na kumwachia Mungu
aweze kutawala.
- Kukana ni kukubali kabisa kutawaliwa na mapenzi ya Bwana.
- Kukana ni kukubali kuachilia ndoto zako mipango na hali yako na kumwachia
Bwana atawale.
Yesu kristo ndiye kielelezo cha kujikana
Filipi 2 :5-8
2. Lazima kujitwika msalaba kila siku na kumfuata yesu
msalaba ni alama ya mateso, aibu kukataliwa na hata kudharauliwa.
Yeye aliyetutangulia ni kama alionyesha ni njia ipi tutakayopitia yaani njia
ya mateso.
Luka 9 :23.
Watu walio tayari kumfuata Yesu kubeba msalaba kitu chochote hakiwatengi na
Bwana na wako tayari kufanya chochote kile Bwana anachowaagiza kufanya.
Watu wanaoziangamiza nafsi zao kwa ajili ya Bwana hao ndio Bwana anaowataka.
Kama hujamwachia Yesu maisha yako ili ayatawale unakuwa unaamua kama
unavyotaka mwenyewe.
Kanuni ya Yesu ni kama unataka kumfuata ni lazima ujikane mwenyewe ujue kuwa
wewe ni mali ya Bwana.
Lazima tujue kuwa Mungu anatufahamu kabisa na anatukumbuka.
Hebu tujikane wenyewe, tukatae njia zetu na tukubali Bwana atuendeshe
mwenyewe.
Tunatakiwa kumtii Bwana na kufuata vile anavyotaka.
Luka 17 : 32-33 Mke wa Lutu alipoamua kujiponya alijiangamiza.
Galatia 6 :12-14 Mtume Paulo alisema haoni fahari kuwa kitu kingine
chochote bali anaona fahari juu ya Bwana.
Angalizo: Hebu tuangalie maisha yetu wenyewe je tunajenga wapi ?
Anayefikiri anaiponya nafsi yake anaiangamiza lakini anayeipoteza kwa ajili
ya Bwana anaiponya.
Toa Maoni Hapa Chini