Uchumba | Apostle Darmacy Blog MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 | Apostle Darmacy Blog

APOSTLE DAMAS

Breaking News

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Thursday, February 23, 2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 

 

Goo

 

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 
About Muses Radio Player...
Version 2.1 (html5)

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.
-->

Tangaza nasi

Breaking News
Loading...

Soma App

Soma App
DOWNLOAD Somaapp NOW!

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Friday, January 17, 2014

Uchumba

Mambo ya kuzingatia katika kipindi cha Uchumba. 

Na Apostle Darmacy

Baada ya kuwa tumepata maombi ya vijana wengi kutaka kujifunza habari za Uchumba, nimeona ni vema nikaandaa somo hili ambalo tunaamini litafanyika msaada kwa vijana wengi ambao wapo kwenye uchumba au wanajiaandaa kuingia katika eneo hili. Hata hivyo somo hili ni pana sana, kwa sasa nimeandika vitu vichache vya msingi, 

Katika kitabu cha Muhubiri 3:1 Biblia inasema “Kwa kila jambo kuna majira yake, na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu”. Hivyo mwanadamu katika maisha yake hapa chini ya jua  kuna vipindi mbalimbali anavyovipitia hii ni pamoja na kipindi cha uchumba kwa sehemu kubwa ya watu.  

Katika kipindi hiki yapo mambo mengi ambayo wachumba hufanya, mengine ni mazuri na mengine hayafai kabisa. Na hii yote inatokana hasa na mitazamo au tafsiri ya uchumba kwa watu husika. Fahamu kwamba tafsiri unayokuwa nayo juu ya mchumba wako ndiyo inayokuongoza kujenga mahusiano ya aina fulani pamoja naye.

Lengo la somo hili ni;

Kuongeza ufahamu wa wachumba kuhusu kipindi hiki na Kuwapa vijana maarifa ya kuwasaidia kuishi kwa nidhamu ya Ki-Mungu katika uchumba wao. Pia ni kuwafikirisha vijana wanaotarajia kupita katika kipindi hiki mambo ya kuzingatia. Si wachumba wengi wanajua, Mungu anawataka wafanye nini katika uchumba wao au kwa lugha nyingine si wachumba wote wanaojua kwa nini kipindi cha uchumba kipo. Naam katika somo hili nimeandika mambo hayo kinaga ubaga.

Kwa kuwa suala la uchumba ni pana na lina mitazamo mingi, yafuatayo ni mambo tuliyozingatia katika uandishi wa somo hili;

  • Kuna makundi mbalimbali ambayo yana taratibu zao kuhusu mchakato wa mtu kumpata mke au mume kikiwepo kipindi cha uchumba. Makundi hayo ni pamoja na makanisa, makabila, familia nk.

  • Wachumba wanaweza kutofautiana kwa kiwango cha elimu, uchumi, ufahamu juu ya mambo mbalimbali, kikabila, umri na hata kwa rangi pia.

  • Kuna baadhi ya wachumba hadi kufikia muda wanakubaliana kwamba watakuja kuishi pamoja walishafahamiana tangu zamani na wengine hawakufahamiana.

  • Wachumba wanaweza wakatoka katika madhehebu/makanisa tofauti na hili ni kwa kuzingatia madhehebu/makanisa mengi yaliyopo.

     Lengo letu ni kuandika juu ya mwongozo wa Neno la Mungu katika kipindi cha uchumba. kwa lugha nyingine, je Mungu anataka wachumba wafanye nini katika kipindi chao cha uchumba?. Kumbuka uchumba ni kipindi/wakati. Basi kama ni wakati jua kabisa kuna baadhi ya mambo ambayo ni lazima yafanyike, kwani Biblia inasema katika Mhubiri 8:5b “ Na moyo wa mwenye hekima hujua wakati na hukumu”, neno hukumu linamaanisha maamuzi, mambo ya kufanya.   

    Yafuatayo ni mambo ya msingi kufanya katika kipindi cha uchumba;

    Jambo la kwanza –  Mruhusu Roho Mtakatifu afanyike Bwana wa uchumba wenu

    2Wakorinto 3:17 ‘Basi Bwana’ ndiye Roho; na alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru’. 

    Kumbuka Roho Mtakatifu ni msaidizi. Hivyo basi ni vema kumtumia vema hasa katika nyanja hii ya mahusiano katika kipindi hiki cha uchumba. Ni Roho Mtakatifu pekee mwenye uwezo wa kukujulisha mambo na siri nyingi kuhusu mchumba wako hata kama yeye hataki kukueleza. Ukimruhusu Roho Mtakatifu afanyike Bwana, yeye atakuongoza katIka kufanya maombi yanayolenga maeneo ya msingi juu ya huyo mwenzako. Kila mtu ameumbwa pamoja na mapungufu fulani au kwa lugha nyingine mapungufu/ udhaifu (weakness) ni sehemu ya maisha ya mwanadamu. Roho Mtakatifu anapokuwa Bwana wa mahusiano yako yeye atakusaidia kuona madhaifu au mapungufu ya mwenzako kama kitu cha wewe kujivunia(Strength) kwa maana ya kuona udhaifu wa mwenzako kama kitu chema na si kibaya.

    Kumbuka Paulo katika 2Wakorinto 12:9-10. —‘Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ….kwa hiyo napendezwa na udhaifu——- maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu. Hivyo Roho Mtakatifu atabadilisha tafsiri ndani yako za vyote unavyoona kwa mwenzako huenda juu ya umbile lake, umri wake, macho yake, kabila lake viwe vitu vya wewe kujivunia. Zaidi Roho Mtakatifu pia atakuongoza katika maombi yatakayosidia kuuondoa ule udhaifu ambao umekuja si katika mapenzi ya Mungu, yaani wa kishetani.

    Jambo la pilini wakati wa kuweka msingi imara wa uchumba wenu na kufahamiana zaidi.

    Hili jambo ni la muhimu  kuzingatia. Ni vema wachumba wakatafsiri na kuelewa vizuri maana ya uchumba. Wachumba wanapaswa kuwa na mipaka fulani katika uchumba wao na  kuwa makini kwa kujilinda na mazingira ya kila namna ambayo yanaweza yakapelekea wao kuanguka dhambini. Ni vema mkajua kwamba ninyi ni wachumba na si wanandoa. Na kama ni wachumba basi uchumba una mipaka yake na hamruhusiwi kufanya mambo ya wanandoa. Mipaka hii iwe kwa habari ya kutembeleana,kupeana zawadi, mawasiliano (ingawa mnapaswa kuwa makini na lugha mnazotumia pia) nk.  Lengo la kutafsiri misingi ya mahusiano yenu ni kujiwekea mipaka na mazingira yatakayowasaidia kuishi maisha ya nidhamu, ushuhuda na kumletea Mungu utukufu.

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.