MBINU ZA KUKUSAIDIA KUOMBA VIZURI
KWA MUDA MREFU
1.
CHAGUA MAHALI PAZURI PA UTULIVU. *Mk 1:35
ili uweze kuomba kwa utulivu na kwa
umakini, chagua au tafuta mahali pazuri
patakapokupa utulivu katika kuomba (concentration in
prayer). Ndio maana Mungu
alipenda kuongea na Musa juu ya mlima. (Kut 24:12-18). Hata
Yesu alizoea kwenda
kuombea mlimani, mahali palipo mbali na vurugu za watu,
alipenda kwenda mlimani.
(Math 14:22-23). Tafuta mahali patulivu; chumbani, kanisani,
mlimani (Math 6:5-6)
2.
CHAGUA MUDA MZURI. *Mhu 3:1,7
Ili
uweze kuomba kwa umakini mzuri, chagua muda mzuri ambao akili yako ma mwili
wako viko fresh. Usilazimishe kuomba hata kama akili yako au
mwili wako umechoka sana. Kila jambo lina wakati wake. Kama umechoka sana, huo
si muda wa kuomba, bali wa kupumzika. Usilazimishe ratiba. ni bora upumzike ili
baadaye uweze kuomba vizuri baadaye. Usije ukajikuta unamkemea Yesu badala
shetani. Penda kuomba wakati una nguvu ya akili na mwili, ili uwe makini
kuongea na Mungu kwa akili timamu. Ndio maana Yesu alipenda kuamka alfajiri
sana kwenda kuomba mlimani. (Mk 1:35, Luka 4:42)
3. OMBA KATIKA ROHO (NENA KWA LUGHA). *Efe 6:18, Rum
8:26-27
Mbinu nyingine nzuri ya kuomba kwa muda
mrefu na kwa ufanisi, ni kuomba kwa Roho; yaani kuomba kwa kunena kwa lugha.
Tunapoomba kwa akili za kibinadamu, Mungu anasikia pia, lakini maombi yako
yanakuwa na mipaka / limited kwasababu akili ya mtu haijui kila kitu. Bali Roho
wa Mungu anajua kila kitu. Naye hutupa kipawa cha kuomba kwa lugha ya mbinguni
iliyo bora zaidi. (Yuda
1:20, Mk 16:17, 1Kor 14:1-4, 15-16,7)
4.
OMBA KWA KUFUNGA WAKATI MWINGINE. *Math 6:16-18
Kufunga kula kunasaidia kudhoofisha mwili, ili roho iwe
makini zaidi kuongea na Mungu kwa kina zaidi. Mwili huu siku zote haupendi
kufanya mambo ya Mungu. Na mwili ukiwa umeshiba, unakuwa na uchovu na uzito wa
kufanya mambo ya kiroho. Mbinu mojawapo ya kuudhibiti, ni kuunyima/kuupunguzia
posho yake ya chakula. Mwili ukidhoofika kiasi, roho yako inapata nguvu na
upenyo mzuri zaidi (Zab 35:13). Mashujaa wote wa imani walifunga na kuomba.
Ndio maana Yesu anasema ‘mfungapo’ akimaanisha ratiba ya kufunga, ipo.
Inasaidia.
5.
OMBA NA RAFIKI (PRAYER PARTNER). *Mhu 4:9-10
Neno la Mungu linasema, ni heri wawili kuliko mmoja. Kuna
faida ya kuomba pamoja na rafiki yako. Kwanza, mnapokuwa wawili au watatu,
inaleta hamasa na ari ya kuomba zaidi. Si rahisi kujisikia mvivu unapokuwa na
waombaji wenzako. Pili; nguvu ya kiroho inaongezeka. Neno linasema, mwombaji
mmoja anafukuza adui elfu moja, bali wakiwa wawili, wanafukuza (sio elfu mbili)
bali elfu kumi! Shangaa! (Kumb 32:20) Hiyo ni kanuni ya mbinguni/kanuni ya
Ki-Mungu. Kadri mnavyoongezeka, nguvu ya Mungu huongezeka.
Kwahiyo, wakati mwingine, omba na rafiki yako,
unayemwamini, unayeweza kumshirikisha mambo yako ya binafsi. Mashujaa wengi wa
imani, walikuwa na marafiki wa kiroho. (Prayer Partners). Kwa Mfano:- Math
17:1-9
Musa - alikuwa na Joshua, Haruni na Huri
Eliya - alikuwa na Elisha
Daniel - alikuwa na Shadrack, Meshack na Abednego.
Yesu - alikuwa na Petro, Yakobo na Yohana.
Paul - alikuwa na Barnaba, Timotheo na Tito.
Wewe Je? Uko na nani katika urafiki wa
kiroho?
Kama huna rafiki wa karibu wa kuomba naye, usikurupuke
kujichaglia. Tulia umwombe Mungu akupe mtu atakayekuwa wa msaada kwako. Mtu
mtakayefungamanishwa naye katika roho, hata kama mmetengana kijiografia, lakini
katika roho, mko na umoja mzuri wa imani. (Math 18:18-19)
6.
OMBA KATIKA MKAO UNAOKUPA UHURU NA NGUVU ZAIDI.
Katika kuomba kwa muda mrefu, mkao uliouzoea utakusaidia
kwenda mwendo mrefu. Yakupasa kujua nguvu yako na udhaifu wako (strong point
and weak point). Wakati wa kuomba, epuka mikao inayokuchosha haraka na tumia
mikao inayokua nguvu zaidi. Kwa Mfano:- Ukiwa umechoka, usipende kuomba kwa
kupiga magoti au kwa kuegemea kitandani. Ni bora uombe ukiwa umesimama au
unatembea tembea, ili kuepuka usingizi na uchovu. Waombaji hodari wanaujua
mikao inayowasaidia kuomba maombi marefu. Wengine hawana mikao maalum, bali
wakiwa katika maombi, huwa wanabadilisha-badilisha mikao ili wasichoke. Hiyo ni
mbinu nzuri pia.
Mifano
ya Mashujaa wa imani;
Ibrahim – aliomba kwa kusimama (Mwa 18:22)
Daniel - aliomba kwa kupiga magoti (Dan 6:10)
Paul - aliomba kwa kupiga magoti (Efe 3:14)
Yesu - aliomba kwa kulala chini (Math 26:38-39)
Eliya - aliomba kwa kukaa chini na
kuweka kichwa kati ya miguu (1Fal
18:42)
Mimi - huwa napenda kuomba kwa kutembea tembea
Naweza
kumaliza kilomita nyingi chumbani kwangu
Nikitembea
huku nikiomba.
Wewe Je? Unaujua mkao wa nguvu? Kama hujui, Tafuta kujua
OMBA NA MUZIKI LAINI
Muziki
wa kiroho, na wataratibu, unaweza kukutengenezea mazingira mazuri sana ya
kuomba kwa muda mrefu. Muziki wa kuabudu, unavuta uwepo wa Mungu kwa namna ya
pekee. Neno linasema, waimbaji na wanamuziki walipoimba na muziki ukapigwa, nao
wakawa kama mtu mmoja, utukufu wa Mungu ukashuka na kulijaza lile hekalu hata
makuhani hawakuweza tena kuhudumu (2Nyak 5:12-14). Kule mbinguni,
kila malaika wa sifa, ana kinubi (zeze/gitaa). Elisha hakutoa unabii, mpaka
mpiga kinubi alipopiga kwa ustadi, ndipo mkono wa Bwana (Roho wa Mungu)
alipokija juu yake, naye akatabiri.
Najaribu kukuonyesha, kuna
connection kati ya muziki wa kiroho na utukufu wa Mungu. Kwahiyo, ukiweza
kuomba huku umeweka kanda au CD ya nyimbo za kiroho za taratibu, utapata
(experience) hamasa ya kiroho (motivation) na utasikia una nguvu ya kuomba kwa
muda mrefu. Kama unaweza, tengeneza kanda au CD maalum yenye nyimbo nzuri
unazozipenda wewe, ili uwe unaipiga wakati wa maombi. Utajikuta unaweza kuomba
kwa muda mrefu na kwa bubujiko zuri zaidi
Toa Maoni Hapa Chini