Picha ya pamoja
ASKARI wa vyombo vya Ulinzi na Usalama
nchini wametakiwa kutumia fursa ya maduka yenye bidhaa zenye gharama nafuu(Duty
Free shop)zilizofunguliwa katika Magereza mbali mbali ili kupata vifaa vya
ujenzi katika kujenga makazi yaliyobora nay a kudumu.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mambo ya Ndani, Mbarak Abdulwazkil, alipokuwa akizungumza katika hafla ya
uzinduzi wa duka la bidhaa zenye gharama nafuu (Magereza Duty Free Shop) katika
Gereza la Ruanda Mkoa wa Mbeya.
Amesema mpango wa kufungua na kuanzisha
maduka hayo ni azma ya serikali ya kuruhusu mpango huu kwa watumishi
wanaohudumia katika sekta ya ulinzi na usalama kuwasaidia kuepukana na kadhia
waliokuwa wakiipata awali.
Amesema maafisa na watumishi wakitumia
vizuri fursa ya maduka hayo katika bidhaa za vifaa vya ujenzi itasaidia kuepuka
aibu inayoweza kuwapata maaskari wengi baada ya kustaafu kazi kutokana na
kukosa nyumba bora ya kuishi.
Ameongeza kuwa Maafisa na Askari
wanaostahili kupata huduma katika maduka hayo wanatakiwa kuzingatia masharti,
kanuni na taratibu mbali mbali zilizopo na zitakazotolewa mara kwa mara
kuhusiana na utoaji wa huduma husika ili ziweze kuleta mabadiliko makubwa
sasa(Big Result Now) kutokana na kuwa na bei nafuu kuliko maduka mengine.
Kamishina wa Magereza Nchini, John
Minja, amesema Jeshi la magereza limejipanga kuhakikisha linasambaza maduka
kama hayo nchi nzima kwa ajili ya kutoa huduma kwa maafisa na Askari ambapo
hadi sasa Jeshi hilo limefikisha maduka Sita.
Ameyataja maduka hayo kuwa ni pamoja na
Gereza la Ruanda lililofunguliwa leo Mkoani Mbeya, Ukonga-Dar Es
Salaam,Isanga- Dodoma,Karanga- Kilimanjaro, Chuo KPF-Morogoro na Butimba-
Mwanza.
Minja amesema kwa mujibu wa sheria ya
uendeshaji wa maduka hayo, wanaostahili kupata huduma ni watumishi wa Jeshi la
magereza pamoja na familia zao ambapo utaratibu utakaotumika kupata huduma hizo
ni vitambulisho vyao vya kazi ili kuhakikisha kanuni na utaratibu wa uendeshaji
wa maduka unazingatiwa ipasavyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Transit Military
Shops(Mtoa huduma ya vyombo vya ulinzi kwa Majeshi ya Tanzania), Alfazar Meghji
ametoa shukrani kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na
Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kendelea kumpa mikataba ya kufanya kazi Tanzsania.
Amesema Military Transit Shop itaendelea
kushirikiana na uongozi wa Jeshi la Magereza katika kusambaza huduma ya Duty
Free Shop katika Magereza yote Tanzania bara ili kuhakikisha kuwa maafisa na
Askari wa Jeshi la Magereza wanaweza kupata manufaa mazuri na bora.
Hata hivyo akitoa shukrani kwa niaba ya
Wageni waalikwa katika Sherehe za uzinduzi wa duka hilo, Jaji Mfawidhi wa
Mahakama kuu kanda ya Mbeya, Jaji Samweli Chocha amepongeza jitihada za jeshi
hilo katika kuhakikisha watumishi wake wanakuwa na maisha mazuri.
Ameongeza kuwa pamoja na vigezo na
masharti yaliyowekwa katika upatikanaji wa Huduma ni vema Jeshi hilo
likaangalia upya umuhimu wa wakazi wanalizunguka eneo hilo namna ya kufaidika
na bidhaa zilizomo Dukani kutokana na kutamanishwa na ubora wake.
Habari hii ni kwa hisani Mbeya yetu na http://apostledarmacy.blogspot.com/
|