SULUHISHO LA FORENI DAR | Apostle Darmacy Blog MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 | Apostle Darmacy Blog

APOSTLE DAMAS

Breaking News

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Thursday, February 23, 2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 

 

Goo

 

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 
About Muses Radio Player...
Version 2.1 (html5)

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.
-->

Tangaza nasi

Breaking News
Loading...

Soma App

Soma App
DOWNLOAD Somaapp NOW!

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Friday, February 21, 2014

SULUHISHO LA FORENI DAR

Mojawapo ya mabasi yanayotembea nchi kavu na majini.

  • Kwa Afrika, Tanzania itakuwa nchi ya kwanza kuwa na aina hii ya mradi wa mabasi ya majini.
  • Mabasi hayo yana uwezo wa kutembea nchi kavu na majini, hii ina maana kuwa yatasaidia kwa mfano kusafiri kutoka Posta kwenda maeneo mengine yoyote ya jiji ambayo yanafikiwa na bahari.
  • Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) inasema mradi huo unaweza kusaidia kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya usafirishaji nchini. Share

Serikali, mashirika binafsi na wadau wa usafiri ndani na nje ya nchi wamekuwa wakifanya jitihada mbalimbali kukabiliana na msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam.

Msongamano huo ambao unachangiwa kwa kiasi kikubwa na uduni wa miundombinu ikiwemo barabara, umekuwa ni kero kwa wananchi na Serikali kwa jumla.

Serikali imewekeza katika Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi (BRT) na usafiri wa treni ndani ya Jiji la Dar es Salaam kama njia mojawapo ya kumaliza tatizo la msongamano wa magari na foleni.

Msingi wa tatizo

Chanzo kikubwa cha foleni jijini Dar es Salaam si wingi wa abiria bali ni wingi wa magari binafsi na njia finyu zisizokidhi mahitaji ya watu walioko katika jiji hilo.

Njia muhimu ya kupunguza foleni na msongamano wa magari ni kupunguza wingi wa magari barabarani na kuweza kuzipanua barabara ili kuwe na uwezekano wa kupita kwa urahisi.


Kutokana na foleni na uduni wa huduma za usafiri wa umma watu wa kundi la kati, wamekuwa wakikimbilia kununua magari binafsi kwa ajili ya kwenda nayo kwenye shughuli zao kwa urahisi.

Aidha, katika kuendeleza harakati za kupambana na tatizo la usafiri, Kampuni ya Transevents Marketing ya Tanzania kwa kushirikana na Kampuni ya Dutch Amphibious Transport Vehicles (DATV) ya Uholanzi inaendelea na mchakato wa kuleta usafiri wa mabasi ya abiria yenye uwezo wa kusafiri nchi kavu na majini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Transevents, Peter Nzunda anasema teknolojia hiyo ya mabasi ya nchi kavu na majini (amphibious) ina lengo la kupunguza tatizo la foleni kwenye barabara za Dar es Salaam hususan katikati ya jiji kwa kuwa mabasi hayo huweza kupita nchi kavu na majini.


Hii ina maana kuwa hata katika maeneo yenye barabara zisizo nzuri au zenye tope, magari hayo huweza kupita hivyo kutosababisha foleni kama ambavyo hutokea sasa katika baadhi ya maeneo hasa mvua zinaponyesha na kuharibu barabara.

Anasema mbali na lengo hilo, mabasi hayo yatatumika kama vivutio vya utalii kwa kufanya utalii wa baharini ambao kwa Tanzania haujashika kasi, licha ya sehemu kubwa ya nchi kuzungukwa na maji.

“Mpango huo wa mabasi ya nchi kavu na majini unalenga kutoa ushawishi kwa watu wa kundi la kati ambao wanatumia magari binafsi waegeshe magari yao na kutumia usafiri huu ambao utakuwa wa hadhi yao na unaokidhi haja kwa ubora wake,” anasema Nzunda
“Lengo ni kujenga maegesho ya magari maeneo mbalimbali kandokando ya bahari, watu wataegesha magari yao na kupanda mabasi yatakayopita majini kwenda Posta na baadaye kurejea kwa utaratibu huohuo na kuyachukua magari yao tena kwenye maegesho walipoacha magari yao”.

ANGALIA PICHA YA ITAKAVYOKUWA MARA BAADA YA KUKAMILIKA KWA MRADI WA MABASI YAENDAYO KASI

“Tunataka pia watu wanaokwenda kwenye fukwe wasiishie kulala na kucheza mchangani, bali wawe wanapanda mabasi haya na kutembelea sehemu  mbalimbali zenye vivutio baharini; hiyo itakuwa ni fursa ya watu kuzunguka baharini wakiwa ndani ya mabasi hayo yatakayokuwa katika miundo tofauti.

Mabasi hayo yatatumika kwa shughuli za harusi hasa kwa wanandoa ambao watapenda kufunga ndoa ndani ya maji.Pia yatatumika kwa safari za kitalii za wafanyakazi wa kampuni mbalimbali, wanafunzi, wanakwaya, wanavikundi na klabu za mipira.
Usafiri huu utakuwa ni wa bei ya kati ambayo itaendana na huduma bora na utalenga kuziba changamoto zote ambazo zinapatikana sasa kwenye usafiri mwingine wa umma,

“Kuna watu wanapanda magari kwa kulipia Sh1,000 badala ya Sh400 kutoka Posta kwenda Mwenge ili kukwepa adha ya kubanana kwenye daladala zinazokaa muda mrefu kwenye foleni, kwahiyo unaweza kuona ni kwa namna gani watu wanahitaji huduma bora za usafiri wa umma.”

Katika mazingira ya kawaida familia nyingi jijini Dar es Salaam zinatumia magari matatu kwa wakati mmoja yaani baba, mama na mtoto, jambo linaloongeza masongamano barabarani.

Pia usafiri huo utawafanya watu hao kuyaacha magari yao nyumbani au kwenye maegesho ya magari yatakayojengwa na hivyo kupunguza kabisa idadi ya magari barabarani.

Mabasi hayo pia yatapunguza gharama za maisha zinazotokana na matumizi ya mafuta kwani kama mtu anaweza kutumia lita 20- 50 kwa siku.

Serikali inasemaje

Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), David Mziray anasema teknolojia hiyo ya usafiri wa mabasi ya nchi kavu na majini imekuwa na msaada mkubwa kwa nchi nyingi Ulaya, kuja kwake Tanzania itakuwa ni habari njema hususan wakati huu ambapo jiji linakua kwa kasi.

 “Kazi yetu ni kupokea maombi na kuangalia kama yanakwenda sambamba na sheria na kanuni zetu na kama unavyojua hii ni aina mpya ya usafiri kwa hiyo lazima kutakuwa na mambo ya msingi ya kuyajadili na kuyapatia ufumbuzi kabla ya kuanza,” Anasema Mziray

Baadhi ya wananchi wanasema mradi huo unaweza kusaidia sana kuondoa kero ya usafiri Dar es Salaam

 

source

Blogger http://apostledarmacy.blogspot.com

Anthony DarmasyAnthony DarmasyAnthony Darmasy

 

 

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.