Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa
Umma imetangaza nafasi za kazi 1,134 katika sekta mbalimbali za ofisi za
umma.
Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa
Umma, Xavier Daudi nafasi hizo za kazi ambazo zinapatikana katika
tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ya www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya
waajiri mbalimbali wa ofisi za umma.
Katibu alifafanua kuwa nafasi 949 ni kwa ajili ya
waajiri walioainishwa katika ofisi za wizara, halmashauri na nyingine
185 ni za taasisi na wakala mbalimbali za Serikali.
Aidha, amewataka waombaji wote wa fursa za ajira
kufungua matangazo yote mawili ya kazi na kuzingatia masharti ya
Matangazo yote kama yalivyo katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili
kabla ya kutuma maombi yao Aprili 9, 2013.
Daudi alifafanua kuwa waajiri ambao watatoa ajira
hizo ni makatibu wakuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Fedha, Wizara ya
Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Wizara ya Maendeleo Jinsia na Watoto, Wizara ya Kazi na
Ajira na Ofisa Mtendaji Mkuu Wakala wa
Wengine ni Makatibu wakuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi,
Wizara ya
Kilimo Chakula na Ushirika,
Wizara ya Viwanda na Biashara,
Wizara ya
Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Nishati na Madini,
Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi,
Wizara ya Maji na
Katibu Ofisi ya Rais Maadili.
Wengine ni Makatibu Tawala wa Mikoa ya
Kagera,
Iringa, Ruvuma, Mbeya, Mwanza, Shinyanga,
Manyara, Dar es Salaam,
Morogoro, Geita, Pwani,
Mara, Kilimanjaro, Lindi, Singida, Tabora,
Tanga,
Katavi na Arusha; pamoja na wakurugenzi wa halmashauri za majiji
na manispaa Mwanza,
Iringa, Songea, Shinyanga, Morogoro,
Singida,
Kigoma/ Ujiji na Temeke.
Nafasi nyingine ni kwa ajili ya wakurugenzi wa Halmashauri za
Wilaya
Mufindi,
Kyela, Rungwe, Mbeya, Chunya,
Biharamulo, Bukoba,
Muleba, Namtumbo,
Songea, Morogoro, Makete, Mkuranga,
Mbinga, Tunduru,
Ukerewe, Sengerema,
Ilemela, Busega, Maswa na Meatu.
Nyingine ni Wilaya za Shinyanga, Kishapu, Kilosa,
Msalala, Rufiji, Rorya, Ruangwa, Lushoto, Mkinga, Mpanda, Monduli,
Ngorongoro, Kigoma, Nachingwea, Rombo, Same, Singida, Urambo, Tabora,
Babati, Mbulu, Simanjiro na Kiteto.
Pia zimo Wilaya za Handeni, Pangani, Kibondo,
Chamwino Mtwara, Nanyumbu, Mpwapwa, Kongwa na Tandahimba pamoja na
halmashauri za miji ya Njombe na Kibaha. Nafasi nyingine ni za Baraza la
Kiswahili la Taifa (Bakita) na Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa).
Nafasi hizo zilizotangazwa zimegawanyika katika
kada zifuatazo; Mchambuzi Mifumo ya Kompyuta daraja la II – (nafasi 10),
Ofisa Vipimo II – nafasi 6,
Mpima Ardhi, daraja la II (nafasi 26),
Mhandisi daraja la II – Ufundi Umeme – Nafasi 9,
Ofisa Mipango Miji
daraja la II– nafasi 13 na
Mhandisi daraja la II - Ujenzi (Nafasi 16).
 |
CLIK LINK HAPO CHINI |
http://www.ajira.go.tz/
Blogger http://apostledarmacy.blogspot.com


CREDIT http://www.ajira.go.tz
Toa Maoni Hapa Chini