HUYU NDIYE MWIGIZAJI WA FILAMU YA YESU AMBAYE BAADHI YA WATU HUDHANI KWAMBA NI YESU.
Historia ya mtu ambaye ameigiza filamu ya Yesu inayofahamika kwa jina la
''JESUS'' ambayo iliigizwa mnamo mwaka 1979 huko nchini Israel, http://apostledarmacy.blogspot.com
imeamua kufanya hivi baada ya kuona ni kwa jinsi gani filamu hiyo
imekuwa ikigusa maisha ya watu wengi kiasi kwamba baadhi ya watu
wanasahau kwamba mtu aliyemo kwenye filamu hiyo ni mwigizaji tu na siyo
Yesu.hata yeye amekiri kwamba wakati wa uigizaji alikuwa akisuluhisha
mambo yaliyokuwa yakijitokeza yeye na waigizaji wenzake baada ya wao
kusahau kwamba yeye si Yesu bali anaigiza tu. KARIBU.
 |
Brian Deacon ndani ya filamu ya ''JESUS'' |
Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni
mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini
Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao baba yake akiwa
fundi makenika na mama yake akiwa ni nesi ndoa yake ya kwanza na Rula
Lenska ilivunjika ambapo alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara
Deacon,ndoa yake ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo mwaka
1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.
Aliigiza filamu ya Yesu ambayo pia ilimfanya aokoke mara baada ya
kuitazama akiwa na miaka 30,baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa
waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260
wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba wanafaa akiwa ni
mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo
akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya
sanaa za majukwaani na uigizaji.
 |
Brian Deacon miaka iliyofuatia baada ya kuigiza kama Yesu. |
Amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa
wakala wake aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama yeye(Brian)atafaa
kwenye kumwigiza Yesu,lakini anasema alifanikiwa,baada ya hapo akawa na
wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu
kumweleza jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo mengine,ingawa
yeye alisema nitatumia sauti yangu na maelezo kutoka kwa
muongozaji.Amesema wiki tatu kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo
alisoma kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo
imenukuliwa kutoka kitabu hicho ambapo Brian amesema kusoma kwake
kulimpa nguvu sana na moyo wa kuigiza filamu hiyo na kuweza kumfahamu
vyema Yesu kuwa ni mtu wa aina gani.
 |
watu wakiangalia filamu ya Yesu ambayo bwana Brian Deacon ni mwigizaji mkuu. |
Katika miezi saba waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian
amesema,walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri
mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake
kwamba wamsaidie kwani amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa
siku hiyo lakini anasema alikuwa anashangazwa na nguvu za ajabu
alizokuwa akizipata na kuendelea kuigiza ingawa wakati huo nasema
alikuwa mkristo jina wa kanisa katoliki,alikuwa anauwalakini kuhusu
mafundisho na huduma ya Yesu kwa ujumla,siku moja wakati anaigiza
alikuwa anawaombea watu mara mwanamke mmoja alishika mkono wake kumbe
alikuwa na mapepo alimuombea na mapepo yalimtoka mwanamama huyo.

Siku nyingine waliokuwa wakiigiza kama wanafunzi wa Yesu wapatao 12
wakiwa ndani ya basi walikuwa wamepanga kugoma kutokana na malipo
waliyokuwa wakipata cha ajabu Brian anasema director alikuja kumuomba
yeye(Brian)azungumze nao warejee kazini akashangaa akamwambia mimi sio
Yesu ni Brian Deacon,akaamua kuzungumza nao,baada ya masaa 36 walikubali
kurudi kuendelea na kazi
Amesema mtihani mwingine ni siku alipokuwa hotelini Tel Aviv ghorofa ya
18 usiku mara kukawa na moto hotelini hapo baada ya mwingereza mmoja
aliyekuwa akivuta sigara kusahau kuizima hivyo kusababisha moto,lakini
anasema bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa ila walifanya kazi siku
inayofuatia muda mrefu bila muongozaji kujali kwamba hawakulala vyema
usiku.
 |
watumishi wa Mungu wakiwa njiani kwenda kuonyesha filamu ya Yesu katika uinjilisti huko Kongo. |
Amesema
siku hiyo mmoja wa waigizaji anayeitwa Tom Panella alianzisha mada kwa
kusema moto uliokuwa umetokea ni hila za shetani,na kusababisha mjadala
wa muda mrefu ni vipi shetani anahusishwa kwenye swala hilo lakini jibu
likawa,shetani hataki filamu hiyo irekodiwe ndio maana analeta hila
zake.haikuwa kazi rahisi kurekodi filamu hiyo na pia si ujuzi wa
kufurahia,baada ya kumaliza kurekodi kwa takribani miezi 18 ilianza
kuonyeshwa kwa baadhi ya watu na ndipo hata yeye kwa mara ya kwanza
akaona ni kwa jinsi filamu hiyo ilivyonanguvu,ukweli na kugusa mioyo ya
watu.
Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza majukwaani na kwenye
runinga, ambapo kwa miaka zaidi ya 30 sasa tangu kutoka filamu ya Yesu
tayari imetazamwa na watu zaidi ya bilioni tatu katika nchi 233(kwa
takwimu za mwaka 2001),zaidi ya watu milioni 117 waliamua kubadilisha
maisha yao na kumpokea Yesu,filamu hiyo ambayo ilitengenezwa chini ya
Campus Crusade for crusade ambao kwasasa wanaitwa Life Ministry pia
nchini Tanzania wapo chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage.ambapo tayari
imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200 zikiwa
njiani kutafsiriwa.
Brian anawaambia watu kwamba yeye ni mwigizaji tu na sio Yesu kama watu
wengine na kuwataka watu hao kujua hivyo ambapo anasema ameendelea
kupata barua mbalimbali za kumpongeza na kumshukuru kwa kazi nzuri
aliyofanya kwenye filamu hiyo,ambapo kwa upande wake anasema anayo
nakala ya filamu hiyo kwenye maktaba yake nyumbani kwao Uingereza,ambapo
kwa takribani miaka 20 filamu hiyo imekuwa ikitazamwa duniani kote na
kubadilisha maisha ya watu.
kati ya filamu alizowahi kushiriki ni pamoja na A zed & Two Noughts
ya mwaka 1985,The Feathered Serpent ya mwaka 1976-1978 na Tamthilia ya
iitwayo Lillie iliyoigizwa mwaka 1978 akitumia jina la Frank Miles.
Huyo ndiye Brian Deacon mwigizaji mkuu wa filamu ya ''JESUS''iliyoigizwa mwaka 1979 huko nchini Israel.
habari kwa msaada wa mtandao.
Toa Maoni Hapa Chini