UZINDUZI WA KITABU CHA MAISHA NA HUDUMA YA ASKOFU MOSES KULOLA.
 |
Muonekano wa kitabu cha MAISHA NA HUDUMA YA MOSES KULOLA. |
Jumapili ya jana kumekuwa na tukio kubwa
na muhimu limefanyika katika kanisa EAGT Temeke, karibu na hospital ya
Temeke ambapo kitabu cha MAISHA NA HUDUMA YA MOSES KULOLA. kimezinduliwa
rasmi na sasa kitauza nchi nzima. Kitabu hicho kimeandaliwa na kina
historia nzima ya marehemu Askofu mkuu Moses Kulola. jinsi alivyoanza
huduma na maisha ya huduma kwa ujumla. sio kitabu cha kukoka.
Katika uzinduzi huo licha ya waumini
wengi pamoja na watumishi wengi wa MUNGU kuhudhuria, walikuwepo pia
mjane wa marehemu Kulola, Mama Kulola pamoja na Mchungaji Daniel Kulola
ambaye ni mtoto wa askofu Kulola.
N i kitabu kinachogusa sana maana huduma
ya Askofu Kulola ilikuwa ni muhimu sana katika Kanisa la Tanzania na
kupitia huduma hiyo maaskofu na wachungaji wengi maarufu leo ni zao la
uinjilisti wa askofu Kulola. BWANA YESU alitenda kazi yake kupitia
mtumishi wake Askofu Kulola kwa kiwango cha hali ya juu, Askofu Kulola
alitembea Tanzania njia kuhubiri Injili na hadi mwisho wa kufanya kazi
ya MUNGU hapa duniani alikuwa anaongoza makanisa zaidi ya 4000.
Zifuatazo ni baadhi ya picha za uzinduzi wa kitabu hicho kama zilivyoandaliwa
 |
Maombi tayari kwa kitabu kuzinduliwa |
 |
uzinduzi |
 |
Mama Kulola |
 |
Mama Kulola |
Toa Maoni Hapa Chini