MAMBO MACHACHE YANAYOWEZA KUONGEZA THAMANI KWENYE MAAMUZI YAKO YA KILA SIKU MAISHA YAKO BINAFSI
1. Punguza Muda wa Kuhudhuria Matukio Mbalimbali
Kizazi chetu ni Event Oriented yaani usipokuwa mwana matukio unaonekana
wa namna yako.Hakikisha unajenga tabia ya kupunguza Muda wa kuhudhuria
matukio mbali mbali si lazima kila tukio uhudhurie.Hakikisha unakuwa
personal reflection time kuhusu mambo yanayokuzunguka maishani mwako.Je
utahudhuria matukio mangapi,Matukio pia hayaishi uliyakuta na utayacha
lakini maisha yetu yana ukomo na yamejengwa katika vipindi maalumu.Ni
muhimu kujenga utaratibu wa kureflect mambo yako Binafsi.Haimaanishi uwe
mchoyo bali tumia ufahamu na uelewe wa namna ya kuchagua uhudhuriaji wa
matukio. Je kila tukio unalohudhuria lina faida kwako?Je kila tukio
lina value gani kwenye maisha yako binafsi? Unaweza ukawa na idadi kubwa
ya matukio kila siku lakini yasiwe yanaongeza thamani ya maisha yako
wewe binafsi. Tambua ulikuja pekee yako na utaondoka pekee yako hakuna
atakayebeba mzigo wako.
2. Punguza Lundo la Marafiki/Makundi
Huwezi kuwa na urafiki ya kila mtu na huwezi kuwa na ukaribu na kila
mtu.Unaweza ukaongea na kila mtu na kuishi na kila mtu lakini
haikujengei mtu huyo kuwa rafiki yako.URAFIKI ni Zaidi ya Salamu na
Kujua umeamkaje na kulalaje. Iwapo mtu hana Personal Intimacy
Relationship huyo sio rafiki ni mtu kama watu wengine tu. Tofauti huyu
unaongea naye na hao wengine haujapata fursa ya kuongea nao. Chagua watu
wachache wanaokufahamu vizuri Huku ukianza na watu wa familia yako then
wengine wafwate ndio uwashirikishe maisha yako na maamuzi yako.
Usipende kila mtu ajue jinsi ulivyo kila wakati.
3. Tafuta Muda wa Kuongea na Watu Waliokuzidi Umri
Jaribu kutafuta watu ambao wamekuzidi umri karibia mara mbili yako kwa Maana Nyingine Inaweza kuwa
Babu/Bibi yako au mtu mwingine mwenye Busara.
Muulize hadithi za maisha haswa aliposhinda na aliposhindwa na kwanini?
Nyakati.zinaweza badilika na teknolojia inakua lakini Kanuni za Msingi
za maisha huwa hazibadiki. BUSARA NA HEKIMA HUDUMU KWA MUDA MREFU LAKINI
FEDHA NA MALI HUJA NA KUONDOKA.Usitumie Muda mwingi kufikiria pesa
while kuna Zana nyingine muhimu kwenye maisha ambazo zinaweza kukuvusha.
Unaweza ukawa umesoma sana na unajua mengi lakini tambua life will
handing us over the same fate.Epuka ujuaji mwingi,hekima husikiliza na
elimu hupiga makelele.
4. Jenga Tabia ya Kupenda, Kusamehe na Kuwaamini Wengine
Tunaweza tusiwe tunaongea lugha moja wala kufanya kitu aina moja kwa
wakati mmoja lakini Upendo ndio kitu kinachuunganisha kwa Pamoja.Unaweza
ukakataa kumsaidia mtu leo lakini kesho ukamhitajia unaweza ukamuona
mtu hana thamani kwako leo lakini kunawakati kile alichonacho kinaweza
kukusaidia
Hakikisha unajenga tabia ya kusamehe na kuwaamini wengine.Epuka kujenga
hoja kwenye matukio ya kusikika.Unaposikia jambo mtatufe muhusika halisi
msikilize kile atakachokwambia kiamini haijalishi mazingira yanaruhusu
au la .Iwapo.si ukweli kwa wakati wake utagundua usilazimishe kusikia
kile unachokipenda wewe. Hii itakujengea kupunguza chuki kwa wengine na
kuwasikiza bila jeuri wala kiburi.
5.
Dhibiti Mihemko na Hisia Zako Kadri Siku Zinavyoongezeka
Ili uwe mtendaji mzuri na mwenye maamuzi bora imekupasa kujifunza
kuzibiti mihemko. Njia nzuri ya kudhibiti mihemko kama mkristo ni maombi
na mifungo ya muda mrefu iliyojengwa kwenye msingi wa neno la Mungu.
Hii itakupa muda mzuri wa kumsikiliza Roho Mtakatifu nini anakuelekeza
cha kufanya na sababu utakuwa tayari na uwezo wa kudhibiti mihemko na
maamuzi ya hisia utatekeleza kile anachokwambia na kitakuwa na faida
kwako.
6. Punguza Shughuli (Activities) na Ubusy
Mara nyingi tumekuwa na shughuli nyingi ingawa si vibaya ambazo huenda
nyingine hazina ulazima. Mara nyingi watu ambao hawana muda binafsi wa
utulivu huwaga wana hasira za hapa na pale lakini wanakuwa na Maamuzi ya
Muda ambayo huwa hayatatui tatizo la kudumu.Ondoa shighuli ambazo
hazina ulazima na ikiwezekana nyingine zikatae,wewe ni mtu mmoja huwezi
kufanya kila kitu waachie wengine.Iwapo unaona una vyeo vyingi punguza
wachie wengine maana mwisho wa siku unaweza kuwa kituko achia wengine
wafanye kwa ufanisi zaidi ili uweze kujenga muda binafsi wa kuwa na
reflection ya maisha yako.
7.
Epuka Kufanya Maamuzi Yatokanayo na Mitandao ya Kijamii (Facebook,
Twitter, Google, Whatsapp etc) Pamoja na Social Media (T.V, Radio etc)
Kizazi chetu tumekuwa na tunashindwa kufanya maamuzi mengi yalio mazuri
sababu hatuna Muda binafsi wa utulivu sababu utakuta muda mwingi
tunaiamini mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kuliko
tunavyojiamini wenyewe bila kujua Vyombo vya Habari na Mitandao hio iko
kimaslahi zaidi iwe moja kwa moja au isiwe ..Hata iwapo wewe binafsi
utaharibikiwa au kufanikiwa wao haiwahusu sana so ni muda muafaka wa
kuhakikisha unakuwa na muda wa kuchuja na kuangalia yale yaliopo kwako
binafsi bila kuangalia ushawishi kutoka kwenye Mitandao ya Kijamii au
Vyombo vya habari ingawa ni muhimu kusikiliza lakini visiwe ndio muamuzi
wako wa mwisho.Pia Epuka kupelekea matatizo yako mengi na changamoto
zako kwenye Social Media na social Networks ili kupata public sympathy
na suluhisho la kile unachopitia.Hii itakusaidia kuepuka pressure kwenye
maamuzi yako mengi.
Credit to
Faraja Naftal Mndeme
Toa Maoni Hapa Chini