Swali: "Ninawezaje kushinda dhambi katika maisha yangu ya kikristo?"
Jibu:
Biblia inazungumzia juu ya vitu hivi tulivyonavyo ili tushinde maisha yetu ya dhambi:
(1) Roho Mtakatifu – kipawa kimojachapo ambacho Mungu ametupa (kanisa
lake) kwa ajili ya kuwa na ushindi katika maisha ya kikristo ndani ya
Roho Mtakatifu. Mungu anatofautisha mtendo ya mwili na matunda ya Roho
Mtakatifu katika wagalatia 5:16-25. katika andiko hilo tunashauriwa
kutembea katika uwepo wa Roho Mtakatifu. “waumini wote tayari wamejazwa
na Roho Mtakatifu”,lakini hapa tunasisitizwa kupatia nafasi Roho
Mtakatifu atutawale na kutuongoza. Hii ina maana ya kuwa tusikilize
sauti yake tusije tukatenda mapenzi yetu wenyewe.
Tofauti ambayo Roho Mtakatifu anaweza kuifanya maishani mwa mtu ni kama
ile ya Petro, kabla hajajazwa Roho Mtakatifu alimkana Yesu mara tatu, na
alikuwa mbeleni ameahidi kumfuata Yesu mpaka kwenye hatari ya kifo
angekufa naye. Baada ya kujazwa na Roho alizungumza waziwazi na kwa
ujasiri mbele ya wayahudi juu ya mwokozi katika siku ya pentekote.
Unatembea ndani ya Roho ukiwa humzuii anapotaka kujidhihirisha (“kumzima
Roho” wathesalonike wa kwanza 5:19) na una kiu ya kujazwa naye kila
wakati (Waefeso 5:18-21). Je mtu hujazwaje na Roho Mtakatifu? Kwanza ni
kwa mapenzi ya Mungu kama vile ilivyo katika agano la kale. Alikuwa
akichagua watu Fulani, kuwajaza kwa ajili ya kutekeleza kazi ama wadhifa
Fulani (Mwanzo 41: 38; Kutoka 31:3; Hesabu 24:2; Samueli wa kwanza
10:10; na kadhalika.) Ninaamini kuwa kuna ushahidi katika Waefeso
5:18-21 na Wakolosai 3:16 yakuwa Mungu huchagua kujaza wale wanaojijaza
Neno la Mungu kwa kuwa kote kote ni kujazwa uwezo wa Mungu.
(2) Neno la Mungu, Biblia – Timotheo wa pili 3:16-17 inasema ya kwamba
Mungu ametupa neno lake ili lituandae katika kufanya kazi njema.
Linatufundisha jinsi ya kuishi na cha kuamini, linatufunulia kama
tumetenda makosa na kuturudisha katika njia ya sawa. Kama waebrania 4:12
inavyosema Neno la Mungu liko hai na lina nguvu ya kupenya ndani ya
nafsi zetu kung’oa lile tatizo ambalo mwanadamu hangeweza kulitatua.
Mwandishi wa zaburi azungumzia uwezo wa Neno la Mungu juu ya kubadilisha
maisha ya watu katika zaburi 119:9,11,105 na aya nyengine. Joshua
aliambiwa siri ya kushinda adui zake (inayoashiria pia vita vyetu vya
kiroho) ni kwamba asilisahau Neno la Mungu bali alitafakari usiku na
mchana ili akalitimize. Haya aliyatenda, ijapokuwa maagizo yenyewe
hayakuwa na uhusiano na mambo ya kivita lakini yakampa ushindi katika
vita vya kuimiliki nchi ya ahadi.
Hii ni sehemu ambayo mara nyingi tunaipuuza. Tunapenda kubeba biblia
tukienda kanisani ama kusoma aya za kukariri lakini hatuyatilii maanani
yale tuyasomayo. Hatuyatafutii nafasi maishani mwetu kiasi cha kutubu
dhambi zetu na kumtukuza Mungu kwa kipawa hiki. Tunasoma tu kiasi cha
kupata mtazamo Fulani juu ya wokovu lakini hatuongezi juhudi zozote
katika kutafakari kwetu mara kwa mara kiasi cha kutufanya tuwe na afya
nzuri kiroho.
Ni muhimu sana kwako ufanye tabia ya kusoma neno la Mungu. Kama bado
hujazoea basi Roho anakusisitiza uwe na tabia ya kulisoma Neno la Mungu.
Nina kushauri uwe na kumbukumbu ya yale uliyoyasoma kwa kuyanakili
kwenye daftari lako au kwenye kompyuta. Biblia ndicho kifaa Roho hutumia
katika maisha yetu na maisha yaw engine (Waefeso 6:17), ikiwa ni sehemu
kubwa ya silaha mojawapo ambayo Mungu hutupa ili tupigane vita vya
kiroho (Waefeso 6:12-18)!
(3) Maombi – Hii pia ni njia nyengine ambayo Mungu ametupatia. Njia hii
wakristo wengi huitaja tu kwa maneno lakini hawaitumii. Tuna ibada za
maombi na nyakati za maombi na kadhalika lakini hatuoni manufaa ya jambo
hilo sawa na kanisa la kwanza (Matendo 3:1; 4:31; 6:4; 13:1-3, na
kadhalika). Paulo mara kwa mara arudia kueleza vile alikuwa akiwaombea
wale aliokuwa akiwahudumia. Lakini tunapokuwa peke yetu hatuitumii njiaa
hii. Mungu ametuahidi mambo mazuri ya ajabu kuhusiana na maombi
(Mathayo 7:7-11; Luka 18:1-8; Yohana 6:23-27; Yohana wa kwanza 5:14-15,
na kadhalika.) Paulo analiongezea mkazo tena katika mafundisho yake juu
ya kujiandaa kwa ajili ya vita vya kiroho (Waefeso 6:18)!
Je, ni muhimu kiasi gani njia hii? Tunapomtazama tena Petro, tunaona
maneno ya kristo aliyomwambia kabla hajamkana kule Gethsemane. Yesu
alipokuwa akiomba Petro alilala. Yesu akamwambia, “Kesheni mkiomba ili
msiingie majaribuni: Roho inataka lakini mwili ni dhaifu” (Mathayo
26:41). Wewe pia kama Petro unataka kufanya mema lakini huna nguvu
yakutosha kufanyia hayo. Lazima tufuate mausia ya Mungu, tuendelee
kumtafuta, tukibisha na kumuuliza… na atatupatia nguvu ile tuitafutayo
(Mathayo 7:7 na kuendelea). Lakini lazima tuitilie mkazo njia hii
maishani mwetu ndiyo tufaulu. Sisemi ya kwamba maombi ndiyo njia maalum
zaidi. La sivyo. Mungu ni wakutisha. Maombi ni kukubali hali zetu za
udhaifu, ukuu wa Mungu mwenye nguvu na asiyeshindwa ili tupate uwezo huo
huo tuweze kuyafanya yaliyo mapenzi yake (wala si yetu) (Yohana wa
kwanza 5:14-15).
(4) Kanisa – Hii ni mojawapo ya njia tunazozifumbia jicho. Yesu
alipowatuma wanafunzi wake aliwatuma wawili wawili (Mathayo 10:1).
Tunaposoma juu ya habari za safari za wale wamishenari katika kitabu cha
matendo ya mitume, hawakuenda mmoja mmoja bali katika makundi, wawili
wawili au zaidi.Yesu alisema mahali wawili au watatu wamekusanyika kwa
ajili ya jina langu, nami nitakuwa katikati yao (Mathayo 18:20).
Anatuamuru tusiache kukusanyana pamoja kama kawaida za watu wengine
zilivyo bali tuutumie wakati wa kuwa pamoja kwetu kwa kutiana moyo
katika upendo na matendo mema (Waebrania 110:24-25). Anatuagiza kutubu
dhambi zetu mmoja kwa mwingine (Yakobo 5:16). Katika habari za hekima
katika agano la kale tunaambiwa ya kwamba chuma hunoa chuma mwenziwe,
vivyo hivyo mtu huchangamsha sura ya rafiki yake (Methali 27:17) “kamba
ya nyuzi tatu haikatiki rahisi.” “kuna nguvu katika umoja wa wengi
(Mhubiri 4:11-12).
Baadhi ya watu ninaowafahamu wamepata kaka na dada katika kristo
wanaotangamana pamoja au kwa simu na wanaelezana vile wanaendelea na
maisha ndani ya kristo na wanawajibika katika kuombeana huku wakiishi
maisha sawa na Neno la Mungu. Mabadiliko mara nyingine huja haraka na
wakati mwengine polepole. Lakini Mungu ametuahidi ya kwamba kadri
tunavyoendelea kutumia njia hizi alizotuwekea, ndivyo atatuletea
mabadiliko maishani mwetu. Vumilia ukijua ya kuwa ni mwaminifu katika
ahadi zake.