PONGEZI KWA MKUU WA WILAYA YA IRINGA MH.RICHARD KASESELA | Apostle Darmacy Blog MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 | Apostle Darmacy Blog

APOSTLE DAMAS

Breaking News

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Thursday, February 23, 2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 

 

Goo

 

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 
About Muses Radio Player...
Version 2.1 (html5)

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.
-->

Tangaza nasi

Breaking News
Loading...

Soma App

Soma App
DOWNLOAD Somaapp NOW!

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Sunday, June 26, 2016

PONGEZI KWA MKUU WA WILAYA YA IRINGA MH.RICHARD KASESELA

HONGERA  MH.RICHARD KASESELA KWA KUTEULIWA KUWA MKUU WA WILAYA YA IRINGA"Iringa DC ""

MKUU WA WILAYA YA IRINGA MH.RICHARD KASESESELA NA ANTHONY DAMAS BLOGER
http://apostledarmacy.blogspot.com/

NENO kutoka 

 Ezek. 22:30 “Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakaye tengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu.

Hitaji kubwa la nyakati zote tangu vizazi na vizazi, katika watu wa kada zote, jamaa, Taifa, Mataifa, Taasisi na Mashirika ya dini ni kupata viongozi wenye sifa na uwezo wa kuwaongoza wengine, pia wenye uwezo na hekima katika kuwaunganisha watu ili kuwafanya kuwa wamoja katika kutumia karama, vipawa, talanta, huduma na rasilimali walizonazo kwa manufaa ya maendeleo yao. Pia waweze kufikia na kukamilisha jambo/malengo na mipango yao waliyokusudia.
Viongozi wanajua wanalopaswa kulifanya na wana uwezo wa kuwachukua watu mbele zaidi ya pale walipo sasa.
 Uongozi ni kipawa (zawadi) ya Mungu kwa wanadamu ili wakae katika amani, utulivu na matumaini. Bila uongozi watu hukosa mwelekeo (dira) na amani, hivyo hufikia hatua ya kufarakana, kutawanyika, kukosa mwelekeo, kila mtu kwenda au kutenda lile analoona linamfaa yeye machoni pake. Rejea baada ya Yoshua kushindwa kuandaa kiongozi, pindi alipokufa wana wa Israel walipoteza mwelekeo kabisa, kila mwamuzi aliibuka na mfumo wake kwani hakuwepo kiongozi. Kwa sababu hiyo Mungu ameweka Uongozi ili watu wapate mwelekeo, amani na matumaini katika kuyatimiza mapenzi yake duniani. Tazama Amuzi. 21:25 watu walijiendea hovyo hovyo, Zek. 13:7 - Nitampiga Mchungaji. Hesabu. 27:15 - 23, Efeso. 4:11 - 13.

MAANA YA UONGOZI.
Uongozi ni hali/tendo la kuongoza.
Ni hali ya kutangulia mbele, kusimamia, kulinda na kuelekeza watu njia au mwelekeo wa kuuendea au kufikia malengo Fulani.
 

MAANA YA KIONGOZI: 

Mark.10:45, 1Tim.4;11 - 12, 1Petr.2:21.
Kiongozi ni mtu Yule ajuaye njia na yale apaswayo kupita nayo na kuzingatia katika njia hiyo.



Ni mtu Yule ajuaye mwelekeo wa jambo hilo au malengo hayo na anauwezo wa kuwatangulia na kuwavutia (shawishi) wengine wamfuate.




Ni mtu aliyepewa dhamana (aliyeaminiwa) na Mungu kuongoza watu wengine (kuwatumikia). Mfano: Yesu - Yoh.14:6; 10:2 - 4, Paulo - 1Kor.11:1; 4:16.

Ni mtumishi (mtumwa) wa wale anaowaongoza.

Mfano: Musa - Kut.10:25 - 26; 13:21 - 22, Yuda - Mw.46:28


Kumbuka:
Kiongozi wa Kiroho siyo mtawala (boss) bali ni mtumishi (mtumwa).
Kiongozi ni kielelezo (mfano) wa kupigiwa, kufuatwa na kuigwa na wengine - Unaosimama mbele yao kuwaongoza


Hivyo maisha ya kiongozi lazima yawe kielelezo katika maeneo matano (5) yafuatayo:- 


Katika Usemi: Chunga (angalia) sana matumizi ya ulimi (yale uyasemayo).
Yakobo 3:1 - 12.
Katika Mwenendo: (Tabia) - Maisha yako ya kila siku machoni pa watu.
Math.5:16, 1Petr.2:11 - 12, Fil.2:14- 16.
Katika Upendo: Kujitoa, kujali, kuhudumia na kuhurumia. Yoh.3:16,
Math.9:35 - 38.
Katika Imani: Maisha ya kumtegemea Mungu. Ebr.10:38; 11:1,6,
Hesabu.14:11, Yer.17:5 - 8, Rumi.1:17, Gal3:11.
Katika Usafi: Maisha Matakatifu - yenye ushuhuda mzuri mbele za watu.
Zb.16:3, Kumb.23:14, 1Kor.3:16 - 17, 1Petr.1:16.
 

KWA HISANI YA DAMAS ANTHONY TAZAMA
BAADHI YA PICHA MKUU WA WILAYA WA IRINGA KATIKA UTENDAJI KAZI WAKE

 Mkuu wa wilaya ya Iringa Pamoja na balozi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk Augustine Mahiga. tarehe 25/06/2016 katika  uzinduzi wa Boma la Kihistoria.http://apostledarmacy.blogspot.com/2016/06/uzinduzi-wa-boma-iringa.html





Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akikimbiza Mwenge na wakimbiza Mwenge kitaifa tarehe 21/06/2016
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela na Mkuu wa wilaya ya Musoma Mh Humphrey Polepole walishiriki katika hafla ya ya kuwaaga wanachama wa shirikisho la vyuo vikuu CCM ambao wamemaliza muda wao. 
14/06/16 Mkuu wa wilaya ya Iringa alitembelea kiwanda cha Mandela Furniture kiwanda kinachoendeshwa na Mke wa Marehemu Felix Mandela. Baada ya kufariki Mumewe 2012 watu wengi walitegemea kiwanda hiki kitakufa kwani mama alikuwa hajawahi kufanya shughuli hizi za kutengeneza samani kiwanda kimeendelea kuwa imara na sasa kinatengeneza madawati 150 kwa wiki pia kinatengeneza samani kwa ajili ya vyuo vikuu na mofisini na majumbani.
14/06/2016 Mkuu wa Mkoa wa Iringa akiongozana na Mkuu wa wilaya walitembela VETA kukagua utengenezaji wa madawati kukamilisha zoezi la madawati. Mpaka sasa VETA wanaendelea kukamilisha order ya madawati 5147. Wamewarejesha wanafunzi wote walio soma VETA. Baada ya zoezi hilo wanafunzi hao watapata bahati ya kujiunga na JKT.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa DC Mhe Richard Kasesela
  alikuwa mgeni Rasmi katika mahafari  ya EASTAFRICA COMMUNITY EAC katika chuo kikuu RUCU
Ambapo ametoa  ushauri kwa wanafunzi kwa habari ya uwekezaji kipindi wakiwa shule mfano kwa Iringa kuna fursa ya upandaji Miti. 
22/05/2016 MKUU WA WILAYA ya Iringa Mh Richard Kasesela aliongoza kikosi cha wana nchi na maafisa wa wanyama pori kumsaka Kiboko aliyevamia mazao ya wananchi na kutishia maisha ya wananchi katika kijiji cha Magunga tarafa ya Kiponzelo. Kiboko huyo alijificha kwenye eneo oevu amabapo wananchi wa kijiji hicho waliogopa kutembea kufanya shughuli za kilimo. mnamo saa 10 na nusu jioni kiboko huyo alipataikana na kuuawa na baadae wananchi kugawiwa nyama yake. Ilikuwa kazi ngumu kumtoa kwenye dimbwi alilo angukia baada ya kuuawa kwa risasi.
20/05/16 Mkuu wa wilaya ya Iringa aliendesha kikao cha wadau wa mazingira katika wilaya ya Iringa. Kikao hicho kiliudhuriwa na wafanya biashara na wakulima wakubwa, wakulima wa kati, Taasisi zisizo za kiserikali, Magereza, wataalamu wa misitu na mazingira. Pia kulikuwepo na watendaji wa halmashauri. Katika maazimio ya kikao waliazimia kuanza zoezi la kulinda vyanzo maji, na kila mmoja ahakikishe anapanda miti

 
8/5/16 katika  uzinduzi wa album ya kwaya ya FAITH ya chuo kikuu Iringa ikiitwa "Temebea na Yesu"
kwenye changisho la madawati Dar es Salaam  na pesa ya kutengeneza madawati 511 ilipatikana.CHANGIA MADAWATI OKOA IRINGA NA KIZAZI CHA BADAE

http://apostledarmacy.blogspot.com/2016/05/madawati.html
 

Mkuu wa wilaya ya Iringa aliposhiriki zoezi la kuokoa wahanga wa mafuriko Pawaga

 

PICHA YA JUU KATIKA MAFURIKO YA PAWAGA

Pawaga kwenye maafa ya mafuriko 


Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.