Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa Pamoja na Chuo kikuu cha Iringa siku ya tarehe 25/06/2016 kutakuwa na uzinduzi wa Boma la Kihistoria

Kutakuwa na matukio mbalimbali yatakayoambatana na ufunguzi ikiwemo
maonesho ya kitamaduni na sherehe rasmi za ufunguzi. Tunawakaribisha
wakazi na watanzania wote kuja kusheherekea utamaduni na historia ya
nyanda za juu kusini.
Pamoja na maonesho mbalimbali ya kuvutia ikiwemo Historia
ya Iringa, Uganga na tiba asili, Hazina na asili ya Utamaduni wa Mkoa
wa Iringa, pia kuna jambo la ziada la kujifunza kwa kila mtu.
Tafadhali jiunge nasi na kuona matokeo ya miaka kadhaa ya kazi ya
kujitolea ya kulifufua Boma la iringa na kulifanya kuwa alama ya
kipekee kusini mwa Tanzania.
 |
Hili ndilo jengo la makumbusho ambalo linaziduliwa leo.
|
 |
| Mgeni Rasmi ni Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk Augustine Mahiga. |
MKUU wa Chuo Kikuu cha
Iringa (IUCo), Profesa Joshua Madumulla amesema Nyumba ya Makumbusho ya Mkoa wa
iringa itafanya kazi kubwa ya kukusanya na kutunza vitu mbalimbali vya kale.
 |
| MKUU wa Chuo Kikuu cha
Iringa (IUCo), Profesa Joshua Madumulla |
Vitu hivyo vya kisayansi, sanaa na historia vitatoa fursa kwa jamii ya ndani na
nje ya nchi kujionea hazina ya urithi uliopo mkoani Iringa. Lina vitu mbali mbali vya zamani vya kihistoria vikiwemo
Mifupa ya Binadamu wa zamani
Vyungu
Pasi ya chuma
Historia fupi ya mke wa Mkwawa
“Uwekezaji katika urithi wa utamaduni hauna budi kupokelewa kama sehemu muhimu
ya program itakayosaidia kukuza uchumi wa jamii husika na taifa kwa
ujumla,”alisema.
Ukarabati wa nyumba hiyo iliyojengwa takribani miaka 116 iliyopita na utawala
wa mjerumani aliyeitumia kama boma lake kuu, umefanywa kupitia mradi wa
Kuendeleza Utamaduni Nyanda za Juu Kusini (Fahari Yetu) unaofadhiliwa na umoja
wa nchi za Ulaya (EU) kwa zaidi ya Sh Milioni 230.
“Fursa ya kulibadili jengo hilo la boma la kihistoria kuwa jumba la makumbusho
ni msingi imara wa kukataa hatari ya kuyumbishwa na mabadiliko yasiyoleta tija
katika kukuza na kuendeleza tamaduni zetu na utalii wa kiutamaduni nchini,”
alisema.
Meneja msaidizi wa mradi huo unaokishirikisha chuo hicho kikuu, Jimson Sanga
alisema uzinduzi wa nyumba hiyo utafanywa na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk Augustine Mahiga.
 |
| Meneja msaidizi wa mradi huo unaokishirikisha chuo hicho kikuu, Jimson Sanga
|
Sanga alisema katika hafla hiyo itakayowashirikisha mawaziri wengine na
viongozi mbalimbali wa serikali, siasa, mila, utamaduni na taasisi mbalimbali
za ndani na nje ya nchi, utakwenda sambamba na maonesho ya rasilimali za
utamaduni na historia ya mkoa wa Iringa.
Wizara ya Maliasili na Utalii imetoa kibali kwa Chuo Kikuu cha Iringa
kulikarabati na kulihuisha jengo lililojengwa na wakoloni wa kijerumani
miaka 114 iliyopita maarufu kama Iringa Boma na kuwa jumba la
makumbusho.
Jengo hilo ambalo litafanyiwa ukarabati na mradi wa kuendeleza na
kukuza utamaduni wa asili kanda ya Nyanda za Juu Kusini unaoitwa Fahari
yetu unaotekelezwa na Chuo Kikuu cha Iringa kwa ufadhili wa Jumuiya ya
nchi za Ulaya kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita limekuwa likitumika kwa
shughuli mbalimbali za Serikali ikiwemo ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya
Iringa.
Jengo hilo lililojengwa kwa usanifu wa hali juu kwa kutumia mawe,
tofali zilizochomwa na tope au udongo na wakoloni wa kijerumani yapata
miaka 114 iliyopita limekuwa Makao Makuu ya ofisi ya Mkuu wa wilaya ya
Iringa kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita.
Kutokana na kuwa na historia ya kuvutia, Serikali kupitia idara ya
mambo kale imekuwa na mchakato wa kuligeuza kuwa jumba la makumbusho
ambapo baada ya ofisi mpya ya Mkuu wa wilaya ya Iringa iliyogharimu
zaidi ya shilingi bilioni 1.8 kukamilika.
Kwa mujibu wa Naibu Mkuu Chuo Kikuu cha Iringa Utawala Dokta Hosea
Mpogole, chuo kikuu hicho kupitia mradi wake wa Fahari Yetu wamepata
kibali cha kukarabati jengo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa
Wamoja Ayubu amesema lengo ni kulibadili jengo hilo na kulifanya kuwa
jumba la makumbusho kwa kukusanya na kuweka ama kutunza kumbukumbu,
kufanya maonesho mbalimbali ya urithi wa utamaduni wa Mkoa huo kwa ajili
ya kukuza utalii na kuleta maendeleo endelevu
Jumuiya ya Nchi za Ulaya wametoa zaidi ya shilingi Bilioni 3.2
kuendesha mradi huo wa Fahari Yetu ambao utadumu kwa miaka mitatu.
KWA HISANI YA DAMAS ANTHONY BLOGER
TAZAMA BAADHI YA PICHA ZA TUKIO ZIMA LA UZINDUZI HUO.