Mhe Richard Kasesela mkuu wa Iringa mjini Leo alikuwa mgeni Rasmi katika changizo la kwaya kuu ya kanisa la Lutheran Kihesa Iringa.
Ambapo katika changizo hilo watu mbalimbali walishiriki baadhi yao ni pamoja na
Askofu Mkuu wa Wa Kanisa la Kilutheri Dayosisi ya Iringa Dr. O. Mdegela pamoja na Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Iringa Prf. Joshua Madumulla pamoja na wengine wengi wakiwemo Wachungaji, viongozi wa serikali pamoja na washirika.
Pia kuanza kutoa Huduma za jamii mfano kuona wangonjwa, kusaidia yatima pamoja na watu wenye mahitaji mbalimbali
Pia Mkuu wa Wilaya Mhe Richard Kasesela amesema amehaidi kutoa shilingi laki tano na kwa kwa ajuli ya changizo ilo. sambamba na hayo changizo hilo ilipatikana takribani Millioni nane laki Tisa na hamsini 8,950,000/=Tsh
Kumtolea
Mungu Fedha na Mali.
Eneo jingine lililo la muhimu sana katika
maisha ya mwamini ni eneo la utoaji wa fedha na mali kwa ajili ya Bwana. Eneo
hili ni muhimu sana kwa kuwa ni sababu kubwa sana ya Mungu kubariki watu wake
na kwa mtu ambaye amekosa uaminifu katika hili eneo ukaaa chini ya laana ila kwa
aliye mwaminifu uwa ndani ya Baraka.
Kuna aina mbali mbali za utoaji wa fedha
na mali, aina hizo ni kama:
A. Sadaka ya
kuwasaidia watu walio katika uhitaji.
Hii ni sadaka ya mtu kumsaidia mtu haswa
Yule ambaye hana matumaini na hana msaada kwa kutoa vile alivyonavyo na
kumpatia. Hii ni sadaka ya upendo kwa kuonyesha kumpenda Mungu na kumpenda Yule
unayemsaidia.
Hii ni sadaka ambayo mtu anaifanya mbele
za mtu kwa ajili ya Mungu, na ikifanyika kwa mtu kujitakia utukufu wake huwa
haina thawabu mbele za Mungu ila ikifanyika kwa moyo wa kupenda na kumtukuza
Mungu ni njema na ubeba thawabu kubwa mbele za Mungu.
Luka 6:38 “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa na
kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa kifuani mwenu. Kwa kuwa
kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakacho pimiwa.” Yesu anapotoa neno hili anazungumza na watu
walioamini kuwa imewapasa kutoa vitu vyao kwa watu(wenye uhitaji) ila kutoa
kwao si bure kwa kuwa ni lazima Mungu atawarudishia tena kupitia watu,
si kama walivyotoa bali ni zaidi kwa kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwa-sukwa hata
kumwagika.
Mfano wa sadaka hii katika biblia ni:
•
Sadaka ya Rahabu kujitoa na kujihatarisha ili
wapelelezi kutoka Israeli wapone.
Kitabu cha Yoshua 2:1-6
•
Sadaka ya BWANA Yesu kwetu wanadamu.
Kitabu cha Isaya 53
•
Sadaka ya mjane wa Sarepta kwa Eliya.
Kitabu cha 1 Wafalme 17:13-16 “
•
Sadaka ya Kornelio kwa watu wenye shida mbali.
Kornelio alikuwa mtoaji sana na aliwapa
watu sadaka nyingi sana, kama inenavyo katika Matendo ya mitume 10:2 “mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba
yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima.”
Sadaka ya mtu kujitoa na kutoa vitu vyake
vya thamani ni sadaka yenye thamani sana mbele za Mungu na ni ishara ya kuwa
mtu anampenda Mungu na yule anayemsaidia.
B. Sadaka
kwa ajili ya kuendeleza kazi ya Mungu.
Sadaka hii huitwa kwa majina mengi, na
wengine huiita sadaka ya lazima. Wengine matoleo, wengine upenda kuiita sadaka
ya ibada. Hii sadaka utolewa kila watu wa Mungu wakutanikapo pamoja kufanya
ibada, na mlengo mkuu wa sadaka hii ni kuiendeleza kazi ya injili ipate kusonga
mbele.
Ni sadaka ambayo utumika kuimalisha
miundombinu ya kanisa, na pia kuwa saidia watumishi wa Mungu, na shughuli
nyingine nyingi kama ilivyopangwa na kanisa husika la mahali pamoja. Hii ni
sadaka muhimu sana na ni ya lazima kwa kila muumini kuangalia kuitoa kila
anapokuwepo ibadani.
Hii ndiyo sadaka inenewayo kuwa usiingie
nyumbani kwa BWANA mikono mitupu.
C. Sadaka ya
malimbuko.
Hii ni sadaka ambayo ni ya mwanzo wa kila
pato ulipatalo katika yale uyafanyayo. Kama ni biashara basi yale mapato ya
kwanza ni malimbuko yako kwa BWANA, kama ni kazi huwa mshahara wa kwanza, kama
ni mazao uwa yale ya kwanza na vivyo hivyo kwa wanyama. Sadaka hii pia kwa
nyakati za leo uwasilishwa kanisani.
D. Sadaka ya
shukrani
Kitabu cha Zaburi 50:14
Hii ufanywa kwa lengo la kumshukuru Mungu
kwa lile lililotokea katika maisha liwe zuri au baya.
Mwalimu Mwakasege anaielezea kuwa ni
sadaka ya muhimu kuifanya kila wakati unapofanyiwa jambo au unapokumbwa na
jambo, na uelezea kuwa hii ni sadaka ya msingi sana kumshawishi Mungu azidishe
utendaji wake katika maisha ya mwamini.
E. Nadhiri.
Zaburi 50:5
Matendo ya Mitume 5:1-11
F. Fungu la
kumi.
Malaki 3:8-12
Hii ni sehemu ya kumi ya mapato yako yote uyapatayo, ni sadaka muhimu sana ambayo pia ipo kwa ajili
ya kuiendeleza kazi yake.
Halleluya Sifa na Utukufu nui Kwa Bwana Yesu!!!
TAZAMA BAADHI YA PICHA KATIKA CHANGIZO HILO