MAOMBI YALIYOAMBATANA NA SHUKRANI | Apostle Darmacy Blog MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 | Apostle Darmacy Blog

APOSTLE DAMAS

Breaking News

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Thursday, February 23, 2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 

 

Goo

 

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 
About Muses Radio Player...
Version 2.1 (html5)

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.
-->

Tangaza nasi

Breaking News
Loading...

Soma App

Soma App
DOWNLOAD Somaapp NOW!

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Thursday, July 7, 2016

MAOMBI YALIYOAMBATANA NA SHUKRANI


Muombapo aminini yamekuwa nayo yatatendeka. Tunapopeleka maombi yetu (haja zetu) mbele za Bwana Biblia inasema tuamini kuwa tayari maombi hayo tuliyoomba yameshajibiwa nayo yatakuwa hivyo. Baada ya hapo ni shukrani mbele za Mungu. Kumshukuru Mungu kwa maombi tuliyopeleka mbele zake ni jambo la msingi kwani linafanya hata yale ambayo hatukumwomba Baba kwa kinywa chetu yafunguliwe. Si vyema kila wakati kuomba maombi ya kupeleka haja zetu kwa Mungu. Tunatakiwa wakati mwingine tuingie kwenye maombi ya kusifu na kushukuru tu kwani yana nguvu kweli kweli mpendwa ukijua siri yake. Tukitangaza matendo makuu ya bwana na jinsi alivyo mwema na jinsi alivyomwaminifu, alivyo mkuu na ya kwamba hakuna Mungu mwingine ila yeye peke yake. Ingia kwenye maombi haya mpendwa bila kupeleka haja zako kwake nawe uone jinsi anavyoweza kukutendea mambo makubwa ambayo hata hukudhania.

Katika injili ya mathayo tunasoma habari za wenye ukoma kumi ambao Yesu aliwaambia wakajionyeshe kwa makuhani na walipokuwa wakiendelea huko wakapokea uponyaji. Tunasoma kuwa kati yao wote kuni waliopona ni mmoja tu aliyerudi kwa Yesu kushukuru kwa uponyaji walioupokea. Watu wengi tumekuwa wepesi kwenda mbele za Mungu na kumweleza mahitaji yetu kwa unyenyekevu na machozi lakini pale tunapopokea majibu ya maombi yetu husahau kurudi kumshukuru. Hatuna budi kujifunza kuonyesha shukrani kwa Mungu kwa yote anayoyatenda katika maisha yetu.

1. Jenga tabia ya kuonyesha shukurani hata kama hujisikii kufanya hivyo

Shukrani huusisha moyo pamoja na kinywa. Mara nyingine moyo unakuwa mgumu hivyo huna budi kutamka maneno ya shukrani hata kama moyo hautaki na kwa kufana hivi utakuwa uhaihuisha moyo tena. Vyovyote vile unavyojisikia, una wajibu wa kumshukuru Mungu kwa mengi anayokutendea .

Efeso 5:20 na kumshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo.

Kolosai 3:17 Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.

2. Shukuru kwa mambo madogo ya kawaida

Mazoea huleta kujisahau hasa baraka ndogo ndogo za kila siku. Tunapaswa kumshukuru Mungu kwa mambo yote anayotutendea kila siku, kwa ajili ya familia zetu, kwa ajili ya kanisa, marafiki n.k.

3. Mshukuru Mungu katikati ya magumu

Mungu hatuambii tushukuru kwa sababu ya matatizo tuliyonayo bali tumshukuru katikati ya matatizo kwa kutambua kuwa wema wake bado upo nasi na ataonekana kututetea na kutuvusha.

4. Usiangalie matatizo uliyonayo b ali mpango wa Mungu katika maisha yako

Ili tuweze kuyaona yale ambayo Mungu anatenda katika maisha yetu na kuweza kumshukuru ni lazima tuone mbali, kule ambapo Mungu anatupeleka na yale ambayo ameahidi kuyafanya na sio kuangalia hali uliyonayo sasa. Ukilitambua hili kila wakati utakuwa mtu wa shukrani maana unajua nini Mungu anafanya katika maisha yako.

5. Waangalie wale ambao kwao utaona umuhimu wa baraka zako

Wakati mwingine tunashindwa kuonyesha shukrani kwa yale tuliyonayo kwa sababu hatuoni ukubwa au umuhimu wa baraka tulizonazo. Kama unalalamika kwasababu ya bosi wako ambaye anakusumbua  angalia jinsi watu wasio na kazi wanavyotaabika, unalalamika kwa sababu mtoto wako amechelewa kuongea, angalia wale wasio na watoto kabisa walivyojaa huzuni. Mshukuru Mungu kwa kile ulichonacho badala ya kulalamika na kulaumu kwa kile ulichokosa.

6. Uwe na muda wa kumshukuru Mungu kila siku

Wana wa israeli walikuwa na tabia ya kumshukuru Mungu kila siku. Nasi yatupasa kuwa na tabia hii katika maisha yetu.

1 Nyakati 23:30 nao wasimame kila asubuhi kumshukuru na kumsifu BWANA, na jioni vivyo hivyo;

7. Mshukuru Mungu mbele za watu

Tunapomshukuru Mungu mbele ya waamini wengine tunawatia moyo kuwa Mungu ni muweza na pia tunaliinua jina la BWANA kati ya mataifa.

Zaburi 35:18 Nitakushukuru katika kusanyiko kubwa; Nitakusifu kati ya watu wengi.

8. Zihesabu baraka zako

Andika yale yote Mungu anayokutendea na uwe unapitia mara kwa mara utaona jinsi ulivyo na mambo mengi ya kumshukuru Mungu. Prayer journal inafaa sana kwa hili  ukiwa nayo itakusaidia kuandika maombi yako na majibu yake.( ukiihitaji tuwasiliane).

9. Onyesha shukarani kwa watu wanaokuzunguka

Onyesha shukrani kwa familia yako na marafiki zako kwa kuwa nawe kwa nyakati zote na kwa yale wanayokutendea. Pia onyesha shukrani kwa watu wanaofanyika msaada katika maisha yako iwe ni kazini, sokoni, kanisani, barabarani n.k na kwa kufanya hivyo utajikuta unaonyesha shukrani zaidi kwa yule aliyewaweka ambaye ni Mungu.

10. Toa kwa wenye mahitaji

Unavyotoa kwa wenye uhitaji unaonyesha shukrani kwa Mungu aliyekupatia na pia unawawezesha na wengine kumshukuru Mungu kwa ajili yako.

2 Korintho 9: 11-12  mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote, umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu. Kwa maana utumishi wa hufuma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukuwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu.

Tukiyafanya haya tutaweza kuwa kama yule mwenye ukoma aliyerudi kuonyesha shukrani na kuepuka kuwa kama wale tisa ambao hawakuona umuhimu wa kumshukuru Mungu aliyewaponya.

 

MAOMBI YA SHUKRANI YANA NGUVU. Barikiwa.


Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.