“kanuni za kibiblia za usimamizi wa fedha zitakazo linda na kustawisha
uchumi wako”
UTANGULIZI:
Kuna mafundisho mengi kuhusu jinsi ya kufanya biashara,kufanya
ujasiriamali,kufanya miradi ,Kujiari n.k yote yaki lenga katika
kuzalisha na kupata fedha au kukuza uchumi.lakini kuna mafundisho kidogo
kuhusu upande wa pili ambao ni wa muhimu sana katika uchumi,jinsi ya
kusimamia fedha.matatizo makubwa ni namna ya kusimamia fedha kuliko
jinsi ya kuzalisha fedha.
wengi tuna pata fedha tatizo ni jinsi ya kuzisimamia,somo hili
litazungumzia eneo hili la pili la “ jinsi ya kutumia kanuni za kibiblia
za usimamizi wa fedha ili kuulinda na kustawisha uchumi wetu.”
KANUNI KUMI ZA KIBIBLIA USIMAMIZI MZURI WA FEDHA:
Biblia inatoa mwongozo mzuri wa usimamizi wa fedha ambao tukiufanyia
kazi tuta punguza kwa asilimia kubwa matatizo mengi ya kifedha tuliyo
nayo.Matatizo mengi ya kifedha tuliyo nayo yanachangiwa sana kwa namna
moja au nyingine na usimimamizi mbaya wa fedha zetu,wengi wetu tatizo
letu kubwa zaidi ni usimamizi wa fedha kuliko kuzalisha na kupata fedha.
usimamizi mzuri wa fedha utalinda uchumi wako na kuukuza uzalishaji
wako,kipato chako.Hata kama unazalisha sana fedha lakini kama una
usimamzi mbaya wa fedha uchumi wako utayumba tu.Matatizo mengi ya
kifedha tunakimbilia kuombewa na kukemea,lakini hayo yote bila
kujifunza usimamizi mzuri wa fedha utakuwa hujatatua tatizo katika
mzizi.hata ukiombewa kupata mpenyo wa kifedha matatizo ya kifedha
yatarudi baada ya muda mfupi kwa kushindwa kuzitendea kazi kanuni za
fedha.
1. MUNGU NDIYE MMILIKI WA FEDHA ZETU
Fedha ni Mali ya Bwana,sisi tu wasimamizi tu au mawakili,hivyo
tunawajibika na vile tunatumia kila fedha tuliyoaminiwa na Mungu.(
Mathayo 25:1-30 ; Zaburi 24:1,)
2. TAMBUA FEDHA NI SUALA LA KIROHO.
Kwa mtu wa Mungu fedha ni suala la kiroho,fedha ina athiri na inagusa
maisha yako ya kiroho pia.vile unavyo shughulika na fedha kuna sema
zaidi juu ya hali yako ya moyo kuliko ushuhuda wako.vile
unavyoshughulika na fedha zako ni kiashirio cha ukomavu wako kiriho.LUKA
16:10-11
Fedha inaweza kuwa mungu wako,fedha ina uwezo zaidi kutuvuta taratibu na
kwa ujanja kutoka kwa Mungu kuliko kitu kingine chochote.MATH 6:24,Ina
nguvu ya kuwa Bwana wetu.
Katika mifano 38 ya Yesu,16 inahusu fedha,katika agano jipya fedha
imezungumzwa zaidi kuliko habari za mbinguni na kuzimu vikiunganishwa
pamoja.mara tano zaidi imezungumzwa kuhusu fedha kuliko maombi,kuna
mistari zaidi ya 1500 inayohusu maombi na imani,wakati kuna zaidi ya
mistari 2000 inayohusu fedha na mali.Aslimia 15% ya Biblia ni kuhusu
fedha.
3. TUNZA KUMBUKUMBU ZOTE ZA FEDHA
Kutunza kumbukumbu ni hatua ya kwanza kukusaidia katika kuandaa bajeti
yako ambayo utaishi nayo.tafuta daftari ndogo na anza kuweka kumbukumbu
za wapi fedha zako zinakwenda,ni kazi ngumu lakini itakusaidi kwa
mipango ya muda mrefu ya kifedha.kiasi gani unatumia kwa mwezi kwa
usafiri?simu?chakula?matibabu?
chakula n.k ni lazima ujue wapi fedha yako
inatoka na wapi fedha yako ina kwenda. Nini nina mililki,nini nina
dai,nini nina daiwa,natuamiaje(MITHALI 27:23-24, 23:23,)
4. FANYA TATHIMINI YA MARA KWA MARA YA FEDHA ZAKO:
ni muhimu kufanya tathimini kwa uaminifu kuhusu uchumi wako,mapato
yako,madeni,vitega uchumi vyako n.k. hii itakusadia kufanya marekebisho
unayoyahitaji na kukusaidia kuishi kwa mpango,kama huwezi kutathimini
hutaweza kupanga,ukishindwa kupanga,tayari umeshindwa kusimamia fedha
yako.(MITHALI 21:5 LUKA 14:28)
5. JIWEKEE MFUMO WA KUPANGA BAJETI NA KUUFUATA:
Bajeti kirahisi nikuandika katika karatasi nini unategemea kupata kama
mapato na njisi gani unategemea kutumia.panga matumizi yako.Ni mpango wa
jinsi gani utatumia rasilimali fedha ambazo unatarajia kupata ,bajeti
inapaswa ijumuishi vyanzo vya mapato pia mpango wa matumizi wa mapato
mf.mpango wa chakula,kodi,zaka,utoaji,akiba n.k(Mithali 21:5, Mithali
21:20)
6. JIWEKEE UTARATIBU WA KUWEKA AKIBA
Weka Akiba, kwaajili ya dharura,akiba kwaajili malengo maalumu, (Mithali
21:20a ;13:11)
Mithali 6. Tenga kiasi cha kuweka akiba anza na kiasi kidogo kwanza.
7. JIFUNZE KUTOA KWA UKARIMU-
(Mithali 11:24-25).kanuni ya uchumi wa Kimungu ni tofauti,kadiri
unavyotoa na sivyo unavyo jilimbikizia ndiyo uchumi wako
unastawi.Kumtolea Mungu,kutoa kwaajili ya kuwabariki wengine,kutoa
kwaajili ya wahitaji(Mithali 28:27 Mithali 11:25.Mithali 19:17,Mithali
3:9-10),Kutoa kunafungua Baraka za Mungu katika Maisha yako.
8. TUMIA FEDHA YAKO KWA HEKIMA NA RIDHIKA NA ULICHO NACHO:
Zingatia vipaumbele na umuhimu,Epuka matumizi ya anasa,manunuzi ya bila
mpangilio,manunuzi ya papo kwa papo,usifanye matumizi yaliyo
nje,yanayozidi kipato chako au uwezo wako wa kifedha.Jifunze kuridhika
na kuuepuka tamaa.usifuje fedha kwa matumizi ya ovyo.jifunze
kuridhika(Mithali 21:20 ;Waebrania 13:5,Mhubiri 6:9)
9. TUNZA VITU NA MALI AMBAVYO UMEVIGHARIMIA FEDHA.
Vitu,mali ni fedha,usipovitunza utatoa fedha tena kununua. Tunza
visiharibike ovyo,vitumike kwa uangalifu ili kuokoa gharama ya
matengenezo au kununua upya.
10. EPUKA MADENI.
biblia haijakataza moja kwa moja kuhusu kukopa,ila kwa uwiano wa
maandiko Haiti moyo madeni,bali inakatisha tamaa kukopa.inazungumza
zaidi madhara ya kukopa.Unapokuwa katika deni unakuwa katika
kifungo,Madeni yana haribu uhusiano.usitumie fedha zaidi ya ile
unayozalisha utaishia kwenye madeni.weka akiba kidogo kidogo badala ya
kukopa.
MITHALI 22:26-27,ZABURI 37:21,MITHALI 22:7
HITIMISHO:
Pengine umekuwa unapitia katika kipindi kigumu cha kifedha,uchumi wako
umeyumba,kabla ya kuhitaji fedha zaidi unahitaji kuzifanyia kazi kanuni
hizi za usimamizi wa fedha.Mungu anakusubiri ujifunze na kuzingita
kanuni hizi za fedha ili akufungulie mlango mkubwa zaidi wa kifedha,ni
jukumu lako kutii kanuni hizi na hali yako ibadilike au ubaki katika
hali uliyo nayo.Mungu akubaliki unapochukua uamuzi wa kusimamia fedha
zako kama wakili mwaminifu.