Thursday, February 23, 2017
MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017
- Next You are viewing Most Recent Post
- Previous Denice Simeo Youth Development Expert atoa ushauri kwa vijana wa chuo
google+
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.
3⃣ *SEMINA YA NENO LA MUNGU UWANJA WA OTTU-MBEYA*
*NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO*
*NA MWL MWAKASEGE*
*SIKU YA TATU* 3️⃣
*TAR 12-OCTOBER -2016*
*LENGO LA SOMO* *NI KUIMARISHA UHUSIANO WAKO NA MUNGU KATIKA KRISTO YESU*
🏃🏻🏃🏻SUMMARY
*1. Usidharau wala kupuuzia ndoto uliyoota maana ni lango mojawapo la Kiroho*
*2. Vijue vyanzo vya ndoto na jua kuombea ipasavyo , Kabl sijasema jambo la tatu nataka nikuambie jambo moja kwanza kwa kitu kilichoko mbele.*
Ukisoma habari za Rahabu utashangaa maana huwanajiuliza Maswali mengi sana kwanini Mungu alikubali kuingia gharama zoote hizo za kuibomoa Yeriko lakini Yeye alikuwa anamhitaji mtu mmoja tu *Rahabu* na Ukisoma Kitabu cha Waebrania unaona kinasema Rahabu Yule kahaba. Sasa kwanini kisingekaa kimya maana baada ya kuchukuliwa na wana wa Israel hakuwa kahaba tena. Lakini lengo lake kuu kutuonesha kuwa *haijalishi shetani amekufanya kitu gani au kakuchafua kiasi gani thamani yako ni damu ya Yesu msalabani. Haijalishi ni ukuta gani uko katika maisha yako , Yupo Mungu anaeweza kubomoa ukuta na kukuweka huru atika maisha yako. Maana thamani yako ni damu ya Yesu kumwagika. Mungu atatumia kila mtu kuhakikisha kuwa anakuokoa, na Mungu atabomoa kila ukuta kwakoni ukuta wa umasikini au wa kujikatia tamaa, au wa umasikini ataubomoa kabisa, atakuweka huru.
Kwa sababu ya Rahabu, ndugu zake wote walipona, Mungu alichagua kahaba kwa ajili ya kuwachapa injili ili wapate kujua kuwa liko Tumaini kwa Mungu. Na ukisoma biblia utoana *(Yoshua 6:23)* ikisema Rahabu baada ya kuokolewa alikaa nje ya matuo ya Israel lakini Joshua alipokuja alimuweka katikati ya Israel mpaka leo. *(Yoshua 6:25)* na ukisoma Mathayo 1:5 utaona Rahabu akiingia katika ukoo wa Yesu.
Fahamu hili *Kama mbele yako ni kuzuri sana kunakuwa na vita yako kubwa sana*
Ukisoma habari za Paulo kabla ya kuitwa Paulo alikuwa anaitwa Sauli, Baadae alikuja kuwa mhubiri mkubwa sana wa injili. Na mara ya kwanza alitumia Torati kupinga injili lakini baada ya kuokoka alitumia Torati ile ile kuhubiri injili. Fahamu hili yuko Mungu anayeweza kugeuza mambo yote usijidharau jipe tumaini kwa Bwana.
Tuendelee na somo
*3. Ngo’a kilichopandikizwa na shetani ndani yako kwa njia ya ndoto na upate kuondoa na madhara yake*
_Ayubu 4:12-16 ‘’ Basi, nililetewa neno kwa siri, Sikio langu likasikia manong'ono yake. Katika mawazo yaliyotoka katika maono ya usiku, Hapo usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu. Hofu iliniangukia na kutetema, Iliyoitetemesha mifupa yangu yote. Ndipo pepo ilipita mbele ya uso wangu; Na nywele za mwili wangu zilisimama. Hiyo pepo ilisimama kimya, nisiweze kutambua sura zake, Mfano ulikuwa mbele ya macho yangu; Kulikuwa kimya, nami nilisikia sauti, ikinena_
_Ayubu 33:14-15 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;¬_
_Daniel 7:1 Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danieli aliona ndoto, na maono ya kichwa chake, kitandani mwake; basi akaiandika ndoto, akatoa habari ya jumla ya mambo hayo_
>>Katika Ayubu anazungumzia juu ya ndoto na maono ya usiku. Mahali pengine kwenye biblia wametumia maono, lakini ni ndoto. Na aliposema katika *usingizi kitandani* maana yake ni ndoto
>>Kwa kusoma mistari hii mistari unaona vitu kama vine hivi.
*1 Alipata neno katika mawazo yake* ‘’ Basi, nililetewa *neno kwa siri*, Sikio langu likasikia manong'ono yake’’ Ayubu 4:12
*2 Iligusa na kusikia kwake* Kama umekuwa msomaji wa habari za ndoto, na utajua kuwa lango la ndoto lipo kwenye nafsi. Na Biblia inazungumzia sikio la ndani.
*3 Hapa utaona mstari wa 14 Hofu ilimuangukia na Roho ya hofu ilimuingia ndani yake*. Kwa hiyo ndoto ndiyo iliyoingiza wazo ambalo hakuwa nalo katika maisha yake yaani wazo la hofu. Ndoto iligusa mifupa yake na mifupa yake na akaanza kupata matatizo. Na kama ni wewe umepewa jukumu la kumbadilisha mtu huyu inatakiwa ushughulike na vitu vyote vinne.
*Ngoja nikuletee shuhuda chache*
Nilikuwa Dar es Salaam mwaka Fulani. Na nilikuwa karibu na hospitali moja ivi na nilishuka kwenye gari, huwa si mara nyingi nashuka kwenye gari nikiwa maeneo ninayofahamika. Kwa sababu siku moja kule Arusha nilikwenda dukani na lilikuwa ni duka Kubwa, lakini Mke wangu akaniambia utaweza nikamwambia ndiyo, nikaenda hapo dukani nikawa na Sukuma Toroli na nahitaji kununua vitu, ghafla watu wakaniona na wakaanza kunifuata, sasa hamna kitu kigumu kama unataka kununua vitu na kuna watu wanakusimamia kwa nyuma. Basi kila mtu hapo anahitaji maombi. Na siku moja nimeenda benki ghafla Wafanyakazi wa pale wote wakaweka *Temporary closed* kwa sababu nao wanahitaji maombi. Si maisha mepesi sana kuishi kama hivyo maana utatamini uishi kama wengine ila ukionekana tu kila mtu anahitaji maombi.
Sasa nilipokuwa nje ya gari langu nilimouna mama mmoja na binti yake na binti yake alikuwa anachechemea mguu. Na walikuwa wameniona niliposimama basi wakaja, Yule mama alisema tumekuona na tulitaka tuje kukusalimia. Nikamuuliza wana shida gani pale hospitali, Binti akaniambia kuwa ameumia kwenye ndoto. Kwa sababu aliota ndoto usiku kuwa analikuwa anapiga mpira na akaumia na alipoamka akaona kweli mguu wake umeumia. Basi nikafanya nao maombi pale na baada ya Maombi alikuwa mzima kabisa kama hajawahi kuumwa kabisa. Na maombi niliyoyafanya ni ya kung’oa madhara yaliyoletwa na ndoto. Na tusingefanya yale maombi hakika ile hali ingemsumbua kwa muda mrefu sana.
>>Pia kuna mwingine aliniandika kuwa huwa anaota ndoto kuwa anaangukia kwenye shimo moja lina maji lingine halina maji na kuna mguu mmoja tu ambao ndio unatangulia yaani kuteleza kuingia kwenye shimo na baada ya muda kidogo ule mguu wake ulileta kidonda.
>>Mwingine kaniandika hapa, kasema hivi niko kanisani naombewa na Mume wangu akaja kuniparua macho, na baada ya hapo macho yangu yalianza kuniuma sana kama yanataka kung’oka na baada ya muda tena mume wangu alinifukuza na hataki hata uniona.
_Isaya 29:8 Tena itakuwa kama mtu mwenye njaa aotapo, kumbe, anakula; lakini aamkapo, nafsi yake haina kitu; na kama mtu mwenye kiu aotapo, kumbe, anakunywa; lakini aamkapo, kumbe, anazimia, na nafsi yake inatamani; hivyo ndivyo utakavyokuwa huo wingi wa mataifa waletao vita juu ya mlima Sayuni_
¬_Waebrania 12:22-24 Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi, mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika, na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili¬_
Katika Ebrania ndiyo tunasoma maana kamili ya mlima Sayuni, kwa sbabu mlima Sayuni ni mdogo sana kuliko hata mlima Rungwe lakini mlima Sayani unaongelewa hapa ni *na majeshi ya malaika elfu nyingi, mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika, na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili¬*_na sasa ukiona katika Isaya unaona kuwa mtu huyu alikuwa ameota ndoto kama anakula, lakini alipoamka alikuwa kama hana kitu. Kwa hiyo ndoto ya mtu huyu pia iligusa viungo vyake na nafsi.Hivi ndivyo alivyoshetani akitaka kuanzisha vita huwa anapita kwenye ndoto na baada ya hapo unakuta mtu anaanza kuwa na hasira na neno la Mungu bila sababu.
Na watu hawa ambao shetani kawabana, inakuwa shida sana kwao kulisikia neno la Bwana. Na kama si Mungu kulilinda kanisa lake huyu mtu aliyeingiliwa na shetani kupitia ndoto na akapandikiza vitu vibaya sana na hasira kali sana, na asipoombewa vizuri anaweza fanya kitu kibaya sana.
Msichana mmoja alinitafuta sana baada ya kuoka akawa anasema baba naomba unisamehe, nikamuuliza kwanini, akasema niliingia mkataba na shetani ili nikuue. Akasema siku moja niliingia hotelini ulipkuwepo na Wafanyakazi wa hoteli hawakunigundua nilikuwekea sumu kwenye chakula ambayo ingekuua kwa dakika tano tu. Na baada ya kula tuliona hata hamjafa na tulikimbia. Na hatukuishia hapo siku moja tulijua gari uanendesha wewe mwenyewe na tukaenda katika kizuizi kimoja cha barabara ambacho askari wapo ili watuombee lifti na baada ya hapo tuweze kulipindua gari. Basi tulipofika mahali pale askari wakatusimamisha wakawa wanawaombea lifti hao wadada lakini askari alisema mzee kwa kuwa mmejaa basi endeleeni. Ukweli ni kuwa tulikuwa wawili tu, lakini Mungu alituongezea malaika na tulionekana kamatumejaa.
~~Kama si Mungu kutulinda wangekuwa wanatufanya mambo mabaya sana. Siku moja nilikuwa kwenye mkutano (semina) sehemu nyingine na nilipokuwa nataka kuachilia Baraka Roho mtakatifu akasema ngoja kwanza waite hao watu au waombee rehema maana baraka hizi zitageuka laana kwao. Kwa sababu walikuwa wanatamka maneno magumu kwa ajili yangu na mke wangu.
~~Pia siku nyingine kwenye semina niliona malaika kaja na upanga, na watu walikuwa na hasira na mimi na Malaika akasema nimekuja ili niwamalize au uwombee rehema, basi nikawaita mbele. Wakaanza kujitokeza mmoja mmoja na niliona malaika ananiambia bado wawili nao nikaita tena wakaja kwa nao na ndipo malaika akatoweka.
~~Hivi vitu ni halisi kabisa. Sasa nataka tuangalie vitu vichache ili tuweze kuomba hapa.
*1 Lazima uombe toba kwa kusababisha lango la ndoto kufunguka na shetani kupita hapo kwenye ndoto.
Kutokujua sheria sio sababu ya wewe kuvunja sheria*.
>>Toba inafanya mambo mawili makubwa, 1. na inakupa uhalali kisheria 2. Inampa Mungu uhalali wa kukupigania. Ni sawa na ndege ya marekani ikienda kuokoa watu, na itaokoa watu wotewa marekani na nafsi ikibaki ndipo itaokoa na watu wengine.
Damu ya Yesu kupitia toba unayoifanya ndiyo inakupa uhalali wa wewe kusaidiwa na Mungu.
*2 Ng’oa Roho iliyoingia kwako*,
katika Isaya tumeona Roho ya Hasira, na katika Ayubu ni Roho ya hofu. Na nataka kutahadharisha watu hapa kuwa usipambane na watumishi wake kwenye nafasi walizonazo kwa Mungu, gharama yake ni kubwa sana.
*3 Omba uponyaji wa madahara yaliyotokea.*
Kama ni mifupa ombea mifupa, na Yule aliyeomba kuwa ombewe maana nyoka aliyemng’ata alikuwa kamuachia sumu. Na tulipoomba alitapika sumu (kitu cheupe)
*4 Kama hujaokoka okoka hii ni kwa usalama wako*
Wokovu unampa Mungu uhalali wa kuja kwako na ndio maana Yesu alikufa msalabani ili aweze kukukomboa na kukuokoa kwa hiyo ni muhimu sana kuokoka.
Tulipokuwa Kigoma siku ya kwanza nikawaambia kuwa Yesu sio wa wakristo na Biblia sio ya wakristo. Si unajua Kigoma watu wengi sio wakristo. Kwa hiyo nilipowaambia hivyo wakawawananishangaa, biblia inasemaje katika Yohana 3:16 ni kuwa Mungu aliupenda ulimwengu,ina maana Yesu ni watu wote na ukimuamini ndio unakuwa mkristo. Biblia nayo ni manual (Mwongozo) ambayo Mungu kama muumbaji katuwekea ili tujue namna ya kuishi hapa duniani kama Yeyeyanavyotaka.
Ukishaokoka unapata mahali pa kukulea kiroho na pia kusanyika na wenzio sio baada ya kuokoka unakuwa unakaa peke yako peke yako. . sasa utaelewa maana yake nini Nuhu alihubiri kwa miaka 120 na alipata watu nane tu. Na hatuoni biblia ikisema mkristo bali ni watu wliomuamini ndio waliokoka.
*5 Kama umeokoka basi Mungu akupe neno lake la kukusaidia kusafisha njiailiyochafuliwa na ndoto*
Neno la Mungu ni nuru, nit aa maisha mwetu, neno la Mungu ni pumzi yake kwa ajili ya kutuongoza maisha yetu. .
Baada ya hapo mwalimu alituombea sana hasa watu waliopata shida kupitia ndoto. Ili kuona live semina semina hizi tembelea
FACEBOOK
https://www.facebook.com/Christopher-Diana-MwakasegeMana-Ministry-132462780111984/
Youtube
https://www.youtube.com/channel/UC4p4lrpgpNd-9bHPgHJ4xWw
Ustream
http://www.ustream.tv/channel/mwakasegemanaministry
website
www.mwakasege.org na kama umeokoka kupitia mafundisho haya soma somo la Utangulizi katika link hii http://www.mwakasege.org/mafundisho/hongera/utangulizi.htm
Pia semina iko live
1. Redio Baraka ya Mbeya. 107.6
2 Redio Rungwe FM
3.Redio HHC ALIVE YA Mwanza
4.Redio sauti ya Injili
UBARIKIWE SANA
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.