Vijana 50
wamepata semina ya mwongozo wa kuwa mabalozi wa malengo ya Maendeleo endelevu (SDGs) (Global
Goals Champions).
By Zainul Mzige
UMOJA
wa Ulaya (EU) na Umoja wa Mataifa (UN) wameweka nguvu ya pamoja
kuendesha kampeni ya uelewa wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)
nchini Tanzania.
Wakiwa Mkoani Iringa wamepata nafasi ya
kuzungumza na wanachuo 1,000 kutoka vyuo vikuu vya Iringa na Ruaha
kwenye semina iliyoelezea malengo ya dunia ambayo ni sehemu ya ajenda
2030 ya maendeleo endelevu duniani ambapo kati ya hao,
Kampeni hiyo imelenga kuwafanya vijana
waelewe malengo 17 ya dunia ambayo kwa sasa yana mwaka mmoja tangu
yapitishwe na kuwatanabaisha wajibu wao katika kufanikisha utekelezaji
wake ndani ya mazingira ya Tanzania.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi
Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya mpango wa misaada ya maendeleo UNDAP II
2016-2021 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) Iringa, Dr. Cephas Mgimwa
alipomtembelea ofisini kwake mjini Iringa.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akifafanua
jambo juu ya ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Mpango wa misaada ya
Maendeleo 2016-2021 (UNDAP II) kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU)
Iringa, Dr. Cephas Mgimwa alipomtembelea ofisini kwake mjini Iringa.
Mwanasheria
wa Chuo Kikuu cha Ruaha Iringa, Martin Noel akiwa ameongozana Mtaalam
wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu kuelekea kwenye
ukumbi wa mikutano chuoni hapo sambamba Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja
wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja
wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendesha
semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana 50 kutoka Chuo
Kikuu cha Iringa na Ruaha ambao watakuwa ni mabalozi wa malengo hayo ya
dunia huku lengo la UN ni kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo
mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia.
Mwakilishi
wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro
akielezea fursa za ufadhili wa masomo nje ya nchi katika tovuti ya Umoja wa Ulaya Tanzania wakati
wa semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana 50 kutoka
Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha ambao watakuwa ni mabalozi wa malengo
hayo ya dunia (Global Goals Champions) huku lengo la UN ni kuwaelimisha
vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia
iliyofadhiliwa na EU.
Mkufunzi wa
Malengo ya Dunia ambaye pia ni Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa
Mataifa nchini, Hoyce Temu akiwapiga msasa vijana 50 kutoka Chuo Kikuu
cha Iringa na Ruaha ambao watakuwa ni mabalozi wa malengo hayo ya dunia
(Global Goals Champions) huku lengo la UN ni kuwaelimisha vijana zaidi
ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia kwenye semina
hiyo iliyofadhiliwa na EU.
Mwakilishi
wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro
akiwa amejumuika na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha wakati
wa semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana 50 ambao
watakuwa ni mabalozi wa malengo hayo ya dunia (Global Goals Champions)
huku lengo la UN ni kuwaelimisha vijana zaidi ya 30,000 ifikapo mwaka
ujao kuhusu malengo hayo ya dunia ambapo semina hiyo imefadhiliwa na
Umoja wa Ulaya (EU) nchini.
Pichani juu
na chini ni vijana 50 kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha
walioshiriki semina maalum ya kuwa mabalozi wa malengo ya dunia (Global
Goals Champions) iliyoandaliwa na UN na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya
(EU) mjini Iringa.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia)
akimkabidhi cheti Rais wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) Iringa Athman
Waziri aliyehitimu kuwa balozi wa Malengo ya Dunia (Global Goals
Champion).
Picha juu
na chini Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro
Rodriguez akiendelea na zoezi la kutunuku vyeti kwa mabalozi wa malengo
ya dunia kutoka Chuo Kikuu cha Iringa na Ruaha.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha
ya pamoja na Mabalozi wa Malengo ya Dunia (Global Goals Champions) baada
ya kuhitimisha semina maalum iliyoshirikisha vijana 50 kutoka Chuo
Kikuu cha Iringa na Ruaha.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha
ya pamoja na Mwanasheria wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) Iringa, Martin
Noel baada ya kuhitimisha semina ya malengo ya dunia mjini Iringa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na Afisa Habari wa Chuo
Kikuu cha Ruaha (RUCU), Muazarau Matola.
Baadhi ya
Global Goals Champions katika picha ya kumbukumbu na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mtaalam wa
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu.
|
Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akiwa na Damas Anthony Global Goals Champions pamoja na Mwanasheria wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) Iringa, Martin
Noel baada ya kuhitimisha semina ya malengo ya dunia mjini Iringa. |
Mkufunzi wa
Malengo ya Dunia ambaye pia ni Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa
Mataifa nchini, Hoyce Temu akibadilishana mawazo na wahitimu wa semina
malengo ya dunia (Global Goals Champions) mara baada ya kuhitimisha
semina hiyo iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Ruaha mjini Iringa ambapo
imefadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
|
Zainul Mzige Operations Manager @ Mo Blog na Damas Athony baada ya kuhitimisha semina ya malengo ya dunia mjini Iringa.
|
credit to
Zainul Mzige
Operations Manager @ Mo Blog