GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.
RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.
MUSIC EQUIPMENTS,CLEANNELESS AND MAINTAINACE BY NYAKALO
Kongamano Kubwa La Vijana na Watoto Mega fest 2016
Damas Anthony Afisa Maendeleo ya jamii
"Ni muhimu sana kwa vijana kuelewa Malengo ya Dunia. Huu ni wakati wao. Kwa kuyaelewa malengo haya inarahisisha utekelezaji wake. Nimefurahi kuona muamko wa vijana waliojitekeza hapa na natumaini watawafikishia wengine ujumbe huu.”
MUSIC EQUIPMENTS,CLEANNELESS AND MAINTAINACE BY NYAKALO
Kongamano Kubwa La Vijana na Watoto Mega fest 2016
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
Peniel Medical Missions
We envision seeing a world in which people living in remote and underprivileged communities have access to quality health care so as to trim down health inequalities in the society
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.
-
Chama cha Kuogelea nchini Tanzania (TSA) kimeteua wachezaji wawili
watakaoshiriki mashindano ya vijana ya Jumuiya ya Madola yaliyopangwa
kufanyika mjini Na...
RSA NI IBADA Mhe. Perreira Silima (NW-MN) 2015
-
*Mhe. Perreira Silima - Naibu Waziri Mambo ya Ndani na Mwenyekiti wa Baraza
la Taifa la Usalama Barabarani**Mhe. Perreira Silima - Naibu Waziri Mambo
ya N...
Ambassadors Mega Festival - MEGAFEST
-
*Conference kuubwaa ya vijana *
*(Ambassadors Mega Festival) *
Hii ni zaidi ya kambi zaidi ya mkutano zaidi ya Fiesta na zaidi ya sherehe
Hizi shamrasham...
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!
ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.
RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.
Samwel John Sitta alizaliwa Desemba 18, 1942 huko wilayani
Urambo Mkoa wa Tabora. Sitta alisoma Shule ya Msingi Urambo kati ya
mwaka 1950 – 1953, kisha alikwenda Wilaya ya Sikonge mwaka 1954 - 1957
na kuendelea na masomo ya “Middle School” katika shule ya “Sikonge
Middle School”. Baadaye mwaka 1958 – 1963 alianza masomo ya sekondari
Shule ya Wavulana Tabora yaani “Tabora Boys” kidato cha I – IV na cha V –
VI.
Mara tu baada ya kuhitimu masomo ya sekondari, Sitta alijiunga Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kusomea Shahada ya Sheria (L LB) mwaka
1964 na kuhitimu mwaka 1971.
Sitta amesoma shahada yake kwa miaka 7 kwa sababu mwaka 1966, wakati
yuko mwaka wa pili na akiwa kiongozi wa wanafunzi UDSM, wanafunzi
waligoma na kuandamana kupinga kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
na kukatwa mishahara yao baada ya JKT. Hoja ya wanafunzi ilikuwa na
mantiki kubwa, kwamba mbona vigogo wa serikali na wanasiasa wanalipwa
mishahara minono na marupurupu makubwa?
Baada ya shinikizo hilo la wanafunzi Mwalimu Julius Nyerere alikubali
kupunguza mshahara wake wa Sh4,000 bila kodi akaagiza pia mishahara ya
mawaziri ipunguzwe kwa asilimia mbili. Miezi miwili baadaye akatangaza
Azimio la Arusha (Februari 5, 1967) kuyapa uzito malalamiko ya wanafunzi
hao.
Watukutu wawili – Sitta na Wilfred Mwabulambo (Wote sasa marehemu) na
wengine kadhaa – waliojitia wazimu na kutetea kile walichokiita haki
zao, (haki za wakulima na wafanyakazi), walimshutumu Mwalimu Nyerere kwa
maneno makali wakidai “…ni heri wakati wa ukoloni kuliko utawala wa
Mwalimu”.
Mwalimu Nyerere alikasirika na kuwafukuza chuo wanafunzi wote 400 kwa
kile alichokiita “kwenda kufunzwa adabu majumbani mwao”. Miezi kumi
baadaye, baada ya Nyerere kushawishiwa na hasira kutulia akaamua
kuwarudisha chuoni wanafunzi 392. Viongozi wa mgomo; Sitta na wenzake 7
walitiliwa ngumu, hawakurejeshwa chuoni.
Busara za viongozi wa chuo zilifanya Mwalimu aliliwe zaidi na kuandikiwa
barua mbili maalumu na chuo zenye Kumb. Na. C3/Sa.13 ya 2/3/1967 na
C3/Ss.13 ya 9/07/1967. Mwalimu alikubali kilio hicho na kuwaruhusu
vijana hao wanane warudi kwa sharti kwamba wale watukutu wawili (Sitta
na Mwabulambo) watandikwe viboko na “Mwalimu Nyerere” mwenyewe. Hii
ndiyo ilikuwa pona ya Sitta ambaye alirejea UDSM na kuendelea na masomo
kwa miaka kadhaa hadi alipohitimu mwaka 1971.
Wakati Sitta anarudi chuoni tayari alikuwa mwajiriwa wa Kampuni ya
Mafuta ya “CALTEX OIL” kama Meneja wa Tawi (1967 – 1969) na mwaka 1969 –
1975 aliajiriwa na Shirika la Maendeleo la Taifa kama Katibu na
Mkurugenzi wa Utawala.
Baadaye mwaka 1976 Sitta aliamua kujiendeleza kielimu katika masuala ya
Usimamizi nchini Uswisi kwenye Chuo Kikuu cha IMEDE ambako alihitimu
Stashahada ya Juu ya Usimamizi mwaka huohuo 1976.
Chini ya mfumo wa chama kimoja, Sitta alikuwa kiongozi wa juu wa CCM na
serikali akiwa mbunge, mkuu wa mkoa na Waziri katika nyakati tofauti na
ameendelea kuwa mbunge na waziri katika mfumo wa vyama vingi.
Sitta alimuoa Margareth Simwanza Sitta
Mbio za ubunge
Enzi za chama kimoja 1975 - 1995 Sitta alikuwa mbunge wa Jimbo la Urambo
(kabla halijagawanywa na kuwa Urambo Magharibi na Mashariki) na pia
alifanikiwa kuwa waziri kwa nyakati tofauti. Kwa mfano wakati wa kipindi
cha mwisho cha Mzee Mwinyi, Sitta alikuwa Waziri za Katiba na Sheria.
Mwaka 1995 Sitta aliingia kwenye mapambano mapya ya siasa za vyama vingi
na kwa bahati mbaya akawa mmoja wa vigogo walioangushwa na wabunge wa
NCCR. Mshindani wake mkuu alikuwa Msina Jacob Abraham. Msina alishinda
kwa kura 10,788 dhidi ya 9,497 za Sitta.
Sitta alirudi tena kwenye jukwaa la siasa mwaka 2005 kwenye uchaguzi
mkuu na aliwashinda wapinzani wake wakuu Lumatiliza Yotamu Lubungila wa
NCCR na Wilson George Ntakamulenga wa CUF. Sitta alipata kura 28,660
(72.3%) na kurejesha heshima yake jimboni Urambo Mashariki. Kurudi kwa
nguvu kulimpa nafasi ya kuwania na kuteuliwa na CCM kugombea uspika wa
Bunge la Tanzania na akaliongoza Bunge la Tisa aliloliita bunge la
Viwango Na Kasi "Speed and Standards" kwa mafanikio na changamoto
nyingi.
Mwaka 2010 Sitta alishiriki tena uchaguzi Urambo Mashariki akawashinda
wapinzani wake wakuu Msafiri Abdulrahmani Mtemelwa (CHADEMA) na Zombwe
Lotto Edward (CUF) kwa kupata kura 19,947 (70.47%). Baada ya ushindi
huo, Sitta alijaribu tena kuwania uspika bila mafanikio; utendaji wake
wa kuiuma serikali na wakati mwingine kuipuliza kwenye Bunge la Tisa
ulimfanya achukiwe na serikali.
Ilipoonekana ana nguvu akatengenezewa “chui wa karatasi” (mshindani),
Andrew Chenge. Chenge naye akachukua fomu ya uspika ghafla,
likatengenezwa ‘zengwe’ kuwa wagombea wote wana nguvu, hapo CCM ikapata
mwanya wa kutamka kuwa haiwataki wote ili kuondoa mvutano. Sitta
akapoteza ndoto za uspika na ukahamia kwa mwanamama Anne Makinda.
Rais Jakaya Kikwete alipotangaza Baraza la Mawaziri mwaka 2010 alimpa
Sitta Wizara ya Afrika Mashariki kama Waziri,vilevile alihamishiwa
Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi.
Mbio za urais
Samuel John Sitta alianza mbio za urais “kimyakimya” tangu alipokuwa
Spika wa Bunge la Tisa (2005 – 2010). Kuna nyakati alikuwa akitoa kauli
zinazoashiria kuwa nchi inayumba na haina uongozi thabiti huku
akionyesha kuwa nchi ina viongozi thabiti na hawajapewa uongozi mkuu wa
nchi, akiwemo yeye.
Hata alipoliongoza Bunge la Katiba mwaka 2014, mara nyingi Sitta
alionekana kama mtu mwenye shauku kubwa na urais na alipohojiwa, mara
kwa mara, juu ya urais alionyesha ana ndoto hizo. Mara kadhaa,
alilalamika kuwa wala rushwa wakubwa wanampiga vita kwa sababu ni msafi.
Katika Uchaguzi wa 2015, Sitta alitangaza nia ya kuwania Urais na
alichukua fomu ya kugombea urais kupita chama cha Mapinduzi ambapo baada
ya uchaguzi wa ndani chama, John Magufuli ndo jina lililofanikiwa
kupenya na kuteuliwa na chama kugombea Urais wa Tanzania.
Mungu Ailaze Roho Ya Marehemu Mahali Pema Peponi Amen.
"Ni muhimu sana kwa vijana kuelewa Malengo ya Dunia. Huu ni wakati wao. Kwa kuyaelewa malengo haya inarahisisha utekelezaji wake. Nimefurahi kuona muamko wa vijana waliojitekeza hapa na natumaini watawafikishia wengine ujumbe huu.”
MUSIC EQUIPMENTS,CLEANNELESS AND MAINTAINACE BY NYAKALO
Kongamano Kubwa La Vijana na Watoto Mega fest 2016
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
Peniel Medical Missions
We envision seeing a world in which people living in remote and underprivileged communities have access to quality health care so as to trim down health inequalities in the society
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.
SOMO: UMOJA WA BIBLIA NA DR.MWALUSAMBO - PART 1
-
UMOJA WA BIBLIA NA DR.MWALUSAMBO - PART 1
Biblia ni kitabu cha ajabu kuliko vitabu vyote duniani. Kwa nini? Ni kwa
sababu jina lenyewe lina maana ya vit...
WASIFU WA BALOZI ANTHONY DAMASSY 1992 - 2017
-
Antony Damassy alikuwa na dreams kubwa sana katika maisha yake. Kwanza
alipenda sana kujitoa kwa jamii bila gharama yoyote, aliwahurumia wanyonge,
na samb...
Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa aipongeza Tanzania
-
*Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine
Mahiga (Mb.) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Antonio
Gut...