Apostledarmacy.blogspot. wampongeza Godwin Msigwa kwa kutangaza Uchumba wake kwa Dr. Faraja
Hongera Sana Mtumishi wa Mungu Godwin Msigwa na Dr. Faraja Hosea Kwa kufika hatua ya Uchumba
|
Godwin D. Msigwa na mke wake mtarajiwa Dr. Faraja Hosea |
MUNGU WA MBINGUNI AWABARIKI!!!!!
Tarehe 3 Desemba 2016 Bwana Godwin D. Msigwa alitoa mahali na kumvisha pete ya
uchumba mke wake mtarajiwa Dr. Faraja Hosea Mpagike mkoani Njombe.
Tuzidi kuwaombea katika mwanzo huu wa kuelekea katika agano la
ndoa.
Swali: "Bibilia inasema nini kuhusu uchumba.
|
Mchugaji akitoa neno |
Jibu: Ingawa neno “uchumba” halipatikani katika Bibilia,
tumepewa kanuni kwamba Wakristo wanastahili kupitia kabla ya ndoa.
Kanuni ya kwanza ni kwamba ni lazima tutafautishe mtazamo wa dunia
kuhusu uchumba kwa sababu mtazamo wa Mungu wahitilafiana na ule wa dunia
(2 Petero 2:20).
Huku ikiwa mtazamo wa dunia juu ya uchumba huenda
usiwe na jinsi tunavyo taka, cha muhimu ni kutambua tabia ya mtu kabla
tufanye ahadi naye. Lazima tujue ikiwa huyu mtu ameokoka katika roho wa
kristo (Yohana 3:3-8) na kama huyo mtu wako ana nia ile kama ya kristo
(Wafilipi 2:5).
Lengo kuu la uchumba ni kumtafuta mpenzi wa maisha.
Bibilia inatuambia kwamba, kama Wakristo tusioe wasio Wakristo (2
Wakorintho 6:14-15) kwa sababu hii itafanya uhusiano wetu na Kristo na
tuaibishe tabia zetu na kanuni zetu ziwe hafifu.
Wakati mtu amejitoa kwa uhusiano, hata kama ni wa uchumba, ni muimu
kukumbuka kumpenda Mungu kuliko vitu vyote (Mathayo 10:37). Kusema au
kuamini kuwa mtu mwingine ni “vitu vyote” au kitu cha maana katika
maisha ni kuabudu sanamu, ambayo ni dhambi
(Wagalatia 5:20; Wakolosai
3:5).
Pia hatustahili kuichafua miili yetu kwa kufanya usherati (1
Wakorontho 6:9, 13; 2 Timotheo 2:22). Dhambi ya usherati sio dhambi kwa
mwili pekee bali ni kinyume na Mungu (1 Wakorintho 6:18). Ni muimu
kuwaeshimu na kuwachukulia kuwa watu wa heshima vile tunavyojipenda
wenyewe (Warumi 12:9-10).
Na hii ni kweli kwa uhusiano wa uchumba. Hata
kama mnachumbiana, kuifuata kanuni hii ndio njia nzuri kuwa na msingi
salama wa ndoa. Mojawapo ya maamuzi tutakayofanya, kwa sababu wakati
watu wawili wanaoana, hushikana na kuwa mwili mmoja kwa uhusiano ambao
Mungu anaunuia uwe wa kudumu na usiovunjika (Mwanzo 2:24; Mathayo 19:5).
Tazama Baadhi ya picha
|
Picha ya pamoja ya Godwin D. Msigwa na mke wake mtarajiwa Dr. Faraja Hosea pamoja na wazazi Bw/Bi Hosea Mpagike |
Toa Maoni Hapa Chini