Wakati
wanachuo wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha mjini Mbeya
wakiahidi kupeleka vijijini kampeni ya malengo ya maendeleo endelevu
(SDGs) Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez amesema
kwamba utekelezaji wa malengo hayo uko mikononi mwa vijana zaidi.
By Zainul Mzige
Operations Manager @ Mo Blog
Alisema nchini Tanzania zaidi ya nusu
ya watu wake ni vijana hivyo wakielewa malengo hayo itakuwa rahisi
kushawishi wengine kuhuisha maendeleo hayo na shughuli zao za kila siku
huku wakitunza mazingira.
Alisema shauri kwanini malengo yamekuwa
mengi wakati yale ya Milenia yalikuwa nane tu, Mratibu huyo alisema
kwamba suala si uwingi wa malengo bali maana yake na haja ya
utekelezaji.
Mkuu wa
Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya, Dr. Daniel
Mosses akimkaribisha na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
aliyemtembelea ofisini kwake mjini Mbeya.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Alisema MDGs (Malengo ya Millennia)
iliacha masuala kadhaa bila uelekeo ikiwamo suala la mazingira na
mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kuwapo kwake kunahakikisha uwapo wa
maendeleo endelevu kwa kuwa kila kitu kinategemea sana mabadiliko ya
tabia nchi kwa sasa.
Alisema ni matumaini yake kwamba kuzinduka kwa jamii ya vijana itasaidia kukabiliana na changamoto hizo za sasa za dunia.
Kauli ya mratibu huyo iliungwa mkono na
wanachuo hao ambao walisema kwamba wanaona uhalisia wa mahitajhi ya
sasa na kwamba watawasilisha kampeni hiyo maeneo wanayotoka ili kuwapo
na mabadiliko.
Mkuu wa
Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya, Dr. Daniel
Mosses akiwa kwenye mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro
Rodriguez aliyeambatana na Mtaalam wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa
Mataifa nchini, Hoyce Temu.
Kwa kuwa wengi ni vijana na kwa kuwa
asilimia 75 ya vijana wanaishi vijijini, itakuwa heri kama
walivyofundishwa na Umoja wa Mataifa kupeleka salamu vijijini ili
kukabiliana na tatizo la mazingira na mabadiliko ya tabia nchi ambayo
yanafumua misimu ya kilimo na upatikanaji wa mvua.
Kushirikisha vijana ni suala la msingi
sana, hasa ikizingatiwa kwamba sehemu kubwa ya vijana wanatoka vijijini
ambako malengo ya maendeleo endelevu yana maana zaidi kwa umma, alisema
Kidai Kabula Shaban, Mwanafunzi anayesomea Shahada ya Sanaa, Sosholojia
na Kazi za Jamii.
Mkuu wa
Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya, Dr. Daniel
Mosses akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez kuendesha semina ya malengo ya dunia
(Global Goals) kwa wanafunzi wa chuo hicho iliyofadhiliwa na Umoja wa
Ulaya (EU).
Amesema amefurahishwa mno na mpango huo
wa kuelimisha vijana hasa utunzaji wa mazingira ili kukabiliana na
tabia nchi. Alisema yeye alivyoelimishwa basi atahakikisha anawaelimisha
wengine kuwa watekelezaji wa maendeleo hayo. Akirejea mazungumzo ya
mwanafunzi huyo kwa niaba ya wenzake.
Alvaro alisema amefurahishwa na mwamko
wa vijana wa kutaka kujua malengo hayo na ni imani yake kwamba kwa
kuwakujua wao basi jamii itaerevuka mapema zaidi.
Naye Mtaalamu wa masuala ya Mawasiliano
wa Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu amesema kwamba kampeni ya kuhamaisha
vijana kuyashika na kuyatekeleza malengo hayo yatafungwa Dar es salaam
Mkuu huyo wa Mawasiliano alisema kwamba
ziara ya UN katika mkoa wa Iringa na Mbeya ni sehemu ya uendelezaji wa
kampeni iliyoanza miezi siota iliyopita baada ya kupitishwa kwa malengo
hayo na mkutano wa viongozi wa dunia na Tanzania kuridhia.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendesha semina kuhusu malengo
ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo
Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
Alisema lengo la kufuata vijana ni kwa kuwa wao ndio wenye maisha ya baadaye hasa kwa sasa wakiwa asilimia 67.
Alisema wanazunguka nchi nzima kutafuta makundi ya vijana kwa kuamini kwamba wakijua na kuyashika basi mafanikio yatakuywepo.
Umoja wa Mataifa umeshatembelea mikoa
10 ikiwamo ya Dodoma, Mbeya, iringa wakitegfemea kupata mabalozi 600
ambao wanatarajia kuwafikia watu milioni 1 ifikapo mwakani.
Aidha wanatarajia kufika Julai 2017
watu milioni 15 watakuwa wanaelewa kwa ufasaha zaidi maendeleo endelevu
kwa kutumia vyombo mbalimbali ikiwamo vyombo vya habari , mikutano ya
kampeni nakadhalika
Mtaalam wa
Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akiwapiga
msasa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji jijini Mbeya wakati wa
semina kuhusu malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyofadhiliwa na
Umoja wa Ulaya (EU).
Mtaalam wa
Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akifafanua
jambo wakati wa semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa
Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji jijini Mbeya iliyofadhiliwa na Umoja wa
Ulaya (EU).
Mwalimu wa
Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji cha jijini Mbeya, Furaha Komoro akiuliza
swali kuhusu juhudi za Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha usawa wa
kijinsia unakuwa na uwiano sawa pande zote.
Mwanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji akishiriki kutoa maoni kwenye semina
ya malengo ya dunia iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa na kufadhiliwa na
Umoja wa Ulaya (EU).
Mwanafunzi
anayesomea Shahada ya Sanaa, Sosholojia na Kazi za Jamii chuoni
hapo, Kidai Kabula Shaban akiuliza swali kwa mkufunzi (hayupo pichani)
wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
Pichani juu
na chini ni sehemu ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji
jijini Mbeya walioshiriki semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)
iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
Mmoja wa
washiriki akipitia kijarida cha malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)
katika semina iliyofanyika Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji jijini Mbeya.
Picha juu
na chini ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha
ya pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji cha jijini
Mbeya waliohudhuria semina ya malengo ya dunia (Global Goals)
iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
Pichani juu
na chini ni semina maalum ya mabalozi wa malengo ya maendeleo endelevu
(SDGs Champions/Global Goals Champions) wakipigwa msasa wa SDGs na
Mtaalam wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu
(hayupo pichani).
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akikabidhi cheti kwa Balozi wa
Malengo ya Maendeleo Endelevu (Global Goals Champion) Mwanafunzi wa Chuo
Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) ambaye pia ni mrembo wa taji la Miss
Mbeya 2016, Eunice Robert.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akikabidhi cheti kwa Balozi wa
Malengo ya Maendeleo Endelevu (Global Goals Champion) Rais wa serikali
ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya,
Mahona Byura.
Picha juu
na chini ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akikabidhi
cheti kwa baadhi ya Mabalozi kati ya 50 wa Malengo ya Maendeleo Endelevu
(Global Goals Champion) katika Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji cha
jijini Mbeya.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na mabalozi
wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) Global Goals Champions wakiwa
wameshikilia vyeti vyao mara baada ya kuhitimisha semina maalum kwa
mabalozi hao.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na mabalozi
wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) Global Goals Champions wa Chuo
Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha jijini Mbeya wakiwa wameshikilia
baadhi ya SDGs.
kuhitimisha semina ya malengo ya dunia mjini Iringa. |
credit to
Zainul Mzige
Operations Manager @ Mo Blog