SEMINA YA NENO LA MUNGU DAR ES SALAAM TANGANYIKA PACKERS*
*HALI YA KIROHO YA ARDHI INAVYOHUSIKA NA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO*
*MWL MWAKASEGE*
*DAY 1: 5 MARCH 2017*
Semina hii italenga maeneo muhimu ya ardhi yanayohusika kufunga watu na
kujua namna ya kuwafunga kutoka katika maeneo waliyofungwa.
*LENGO: KUHAKIKISHA MAFANIKIO YAKO YALIYOFUNGWA KATIKA ARDHI YANAFUNGULIWA*.
*1* *KUFUNGUA MAFANIKIO YAKO YALIYOFUNGWA NA HALI YA KIROHO YA ARDHI
INAYOFANYA HALI YA MAHALI UNAPOSIHI PAWE NYUMBA YA UTUMWA*.
_Kumbukumbu la Torati 6 : 12 ndipo ujitunze, usije ukamsahau Bwana
aliyekutoa nchi ya Misri, nyumba ya utumwa._ Kufuatana na 2 Nyakati 7:14
ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na
kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia
toka mbinguni, *na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao*. Nchi
maana yake ni ardhi yenye mipaka halali ya kiumiliki
>>Hapa
anazungumzia nchi na sio taifa.. maana taifa linahusisha mkusanyiko wa
watu walio katika uongozi waliokubaliana.Taifa nalo lina mlololongo
wake. Katika biblia kuna taifa.. jamaa kabisa.. jamaa na lugha. Taifa
linaweza kuwepo lakini halipo katika nchi yake.. biblia inasema _Au
Mungu amekwenda wakati gani akajitwalia *taifa toka kati ya taifa
lingine*, kwa majaribu, na kwa ishara, na kwa maajabu, na kwa vita, na
kwa mkono hodari, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa maogofya makuu, kama
vile Bwana, Mungu wenu, alivyowatendea ninyi katika Misri, mbele ya
macho yenu? Kumbu 4:34_ . Israel walikuwa taifa lakini walikuwa katika
nchi ya Misri.
Wakati unasoma jua namna ya kutofautisha kati ya
nchi na taifa, na nilipoanza kulitazama hili suala la ardhi lilinipa
kujua mambo mengi sana. Nilipoanza kufundisha hali ya ardhi katika
mkoa mmoja.. watu walianza kuzunguka na kusema Mwakasege kapata wapi
hiki kitu.. watu wa kule waliniambia na niliwaambia muwe na amani..
maana hili neno ni la Mungu. Maana si wengi wanajua kuwa haya mambo
ninayoongea yapo kwenye biblia.
Huwa nafundisha waalimu kuwa
kabla ya kufundisha hilo neno liweke kwenye matendo kwanza wewe mwenyewe
maana yake fundisha kwa shuhuda na hapa tutafanya maombi hapa ili mpate
kuona. Ukiona nakufundisha masomo haya ujue mimi mwenyewe nimeyaweka
kwenye matendo na ndio nimeona matokeo yake na ndipo nakuja kukufundisha
kitu halisi ninachokijua.
*2.UKILINGANISHA 2 NYAKATI 7:14 NA
KUMB 6.12 UTAONA YA KUWA HALI YA KIROHO YA ARDHI INAWEZA GEUZA ENEO
KUWA NYUMBA YA UTUMWA.*
Kumbukumbu la Torati 6 :12 ndipo ujitunze, usije ukamsahau Bwana aliyekutoa nchi ya Misri, *nyumba ya utumwa*
Nchi ni ardhi yenye mipaka halali na nchi hapa kwa mujibu wa kumbu
6:12.. *nchi ya misri nyumba ya utumwa* kwa hiyo ardhi ya Misri
imefanyika nyumba ya utumwa.Ardhi ina uwezo wa kufanya eneo kuwa nyumba
ya utumwa.. tunaenda sawa sawa?Ukitazama kiroho utaona kiupana ardhi
maana hamna nchi iliyojengwa kama nyumba lakini Mungu anaita nchi ya
Misri nyumba ya utumwa.
*3.UTUMWA WA WANA WA ISREAEL ULIKUWA WA KIROHO LAKINI ULIJITOKEZA KATIKA MAISHA YAO YA KILA SIKU*
Hapa kuna sababu 3
*I) Shida haikuwa kazi.. bali mazingira ya kiroho ya kazi waliyokuwa wanafanya hiyo kazi*
_Kutoka 1 :11-14 Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo
yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi.
12 Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi
kuenea. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa Israeli. 13 Wamisri
wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali; 14 wakafanya maisha yao kuwa
uchungu kwa kazi ngumu; kazi ya chokaa na ya matofali, na kila namna ya
kazi ya mashamba; kwa kazi zao zote walizowatumikisha kwa ukali._
Tuangalie kazi walizokuwa wanafanya maana kazi zile walizofanya wakiwa
Misri ndizo hata Kanani walifanya maana walikuwa wanajenga miji ya
akiba na majumba. Biblia inasema wakifanya kazi ngumu, sasa hapa nataka
uelewe si kila kazi ngumu ni utumwa. Maana maeneo yote kama ni
kushughulika na chokaa na ujenzi kote walifanya (Kanani na Misri) sasa
tatizo lilikuwa ni mazingira ya kiroho.
Hata walipomlilia Mungu
kwa sababu ya Utumwa. _Kutoka 2 :23 Hata baada ya siku zile nyingi
mfalme wa Misri akafa; wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule
utumwa, wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule
utumwa._
Utumwa si kazi bali ni mazingira ya kiroho
yanayotengeneza hali ya kimaisha, na yanabana fikra na kuweka mipaka
namna Ya kufanya kazi. Na si wengi wanajua hili. Utasema kwanini kwa
sababu
*2. WALISHINDWA KUJITOA*.
Maana ingekuwa ni kazi
wangeacha.. ni sawa na mtu analalamika kuwa kazi ngumu na bado yuko
kazini analalamika weeee lakini kazi haachi .. sasa si utoke utafute
nyepesi, kuna maana gani kulalamika na kuendelea kubaki mazingira yale
yale.
Unaweza ukawa mtumwa katika mazingira ya nyumbani na ni
tofauti na mazingira ya gereza maana mazingira ya nyumbani yanadanganya
lakini bado utumwa ni utumwa haijalishi uko gerezani au nyumbani.
Wana Israel Katika mazingira ya kawaida hawakujua kama wako utumwani..
kama Mungu asingewatangazia kuwa watumwa wasingejua. Maana walipoanza
kulia Mungu aliwaondolea utumwa na hakushughulika na uchungu bali
alishughulika na utumwa..Mzee Yakobo alikufa walimzika Kanani na hamna
mtu alibaki kule waliacha kaburi tu. Na wote walirudi Misri, hawakujua
kwanini wanarudi Misri, sababu ilikuwa ni ya kiroho zaidi.
*3.ILIBIDI MUNGU AWATOE KWA NGUVU*
Kumbukumbu la Torati 7 :8 bali kwa sababu Bwana anawapenda, na kwa
sababu alitaka kuutimiza kiapo chake alichowaapia baba zenu, ndiyo
sababu Bwana akawatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya
utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri. Sio swala la kazi bali
yalikuwa ni mazingira ya kiroho. Na ilikuwa kazi ya kulima, au
kutengeneza matofali lakini ilikuwa ni kazi ya utumwa..
Japo
walikuwa wanalima lakini walikuwa wanaona uchungu.. na hawakujua nini
kimewabana.. maana kama kazi ingekuwa utumwa basi kila mtu asingetafuta
kazi. Maana kuna baadhi ya wapendwa hawataki kufanya kazi na wanaaza
kuhalalisha kwa kutumia mistari ya biblia na kusema kuwa utaishi kwa
imani lakini Biblia inasema asitaka kufanya kazi na asile
*4. WAISHIO NDANI YA NYUMBA WANATAMBULIWA KIROHO KWA KUANGALIA JINA LA MMILIKI WA NYUMBA HIYO.*
_Esta 8 :1-2 1 Siku ile mfalme Ahasuero alimpa malkia Esta nyumba yake
Hamani, yule adui ya Wayahudi. Mordekai naye akahudhuria mbele ya
mfalme; kwa maana Esta alikuwa amedhihirisha alivyomhusu. 2 Basi mfalme
akaivua pete yake, aliyompokonya Hamani, akampa Mordekai. Naye Esta
akamweka Mordekai kuwa juu ya mlango wake Hamani._
>>Ukisoma ile sura _Esta 7 :10 Basi wakamtundika Hamani juu ya mti
aliomwekea tayari Mordekai. Ghadhabu ya mfalme ikatulia._
Sasa unganisha na Esta 8:1.. Ester alipewa nyumba ya hamani.. Nyumba katika ngazi ya kiroho inatazamwa tofauti sana.
Naanza kueleza Kumb 6:12 ndipo ujitunze, usije ukamsahau Bwana
aliyekutoa nchi ya Misri, *nyumba ya utumwa* Ondoa misri weka utumwa..
hajailishi uko wapi kama wewe ni Mmsiri watakujua kuwa wewe ni mtumwa
hata kama uko USA au China .
Na walipokuwa wanabishana juu ya
kuteuliwa kwa Haruni kuwa Kuhani wa Mungu, Mungu alisema walete
fimbo kwa ajili ya nyumba moja moja.. maana kila familia wana ID
(Utambulisho) . Haruni hakuhitaji kuleta fimbo ya watoto wake, maana
fimbo moja tu ilitosha kutambulisha familia yake.
Nyumba ya
Yakobo wana kitambulisho kinacho fanana. Kwa hiyo ukisema nyumba ya
Yakobo haijalishi wako wapi ila wanatambulika kama ni watoto wa Yakobo.
HAMANI alipokufa alikuwa na alama na alipokufa Hamani Ester ndiye
alipewa mamlaka (yaani adui ndio alipewa madaraka) .. haijalishi watoto
wake Hamani wanajipanga kiasi gani kurithi mali za baba yao lakini
Ester ndiye msimamizi mkuu wa nyumba yao yaani ndiye mwenye sauti. .
Ile Pete ya Hamani alipewa modekai na alipewa na mamlaka kwenye
lango.. na nyumba ile ya Hamani waliobaki wote waliuwa. Haijalishi
hawako nyumbani lakini wako marked kiroho kuwa ni wa nyumba ya Hamani
.. haijalishi wayahudi wako wapi.. walikuwa marked..
Nyumba ya baba yako kama wamepewa adui zako utapa shida sana.. maana biblia inasema uzao wako utamiliki malango ya adui
_Mathayo 12 :29 Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye
nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu?
Ndipo atakapoiteka nyumba yake._
Maana yake nani anayemiliki
nyumba na uzao wako.. huwezi wafungua waliofungwa kama hauna nguvu ya
kumshika yule aliyewashika wafungwa wako.
*5.MUNGU ALIWATOA WANA WA ISRAEL KUTOKA KATIKA NYUMBA YA UTUMWA KWA KUPITIA KWENYE MALANGO YA NYUMBA YA UTUMWA*
_Mathayo 12 :29 Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye
nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu?
Ndipo atakapoiteka nyumba yake._
Alitumia damu ya agano na nchi
ya misri kipindi kile ilikuwa ina mazingira ya kitumwa na Mungu
alifuata uzao wa Ibarahim na alienda kuwatoa kwa sababu ya agano..
walikuwa na alama za kiagano, japo walikaa maiaka 400 na utumwani na
walikuwa hawasogei kimaisha lakini Mungu aliwatoa.
Je Mafanikio yako hayasogei kwa kuwa uko nyumba ya Misri ya utumwa nayo imekufunga?
Hata kama ni kwenu ardhi yenu imekuwa nyumba ya utumwa utapata shida
sana. Ndio maana utaona Kijana ana akili lakini yuko nyumbani, muda
wote anazubaa tu nyumbani, na hatafuti hata kazi yupo yupo tu , na
unashangaa watoto wa jirani wanasogea ila wako wamekwama kabisa..
Wewe unafikiri ni sawasawa hapa kumbe katika ukoo mna alama ya kuwa ni
watumwa, yaani mmefungwa na ndio maana hamsogei na kama mna agano na
Mungu na shetani hata waaachia kirahisi rahisi
Maana unalima
kama watu wengine, lakini wako utumwani Wana wa Israel hawakujua na
ndio maana waliona uchungu wakati wanafanya kazi, kumbe sababu ya
mazingira ya kiroho..
Hata wale wasimamizi walikuwa wanasimamia
kwa sababu ya mazingira ya kiroho na waliwatesa sana wana wa Isarel,
ndio maana utaona Mtu anahama nyumba kutoka nyumba ya kupanga kwenda
kwenye nyumba yake unakuta hata kazi anachaaaza na anakuwa mvivu
Watu wengi hawajui kwanini Mungu aliwapitisha wana wa Israel langoni
katika nyumba na hawajui kwanini. Na alitumia malango na alitumia
damu ya Pasaka waliyopaka katika malango. Watu wako hapa wamefungwa
wasipate kazi.. na hata nyumbani kwao hawatoki na wamekwama hapo yaani
wamefungwa kabisa
Wengine wamefungwa kwa kitu cha imani na wapo
wapo na asilimia kubwa sana ni vijana wa kiume hawafanyi kazi na
wanafika muda wa kuoa lakini ukiwauliza kazi hawana majibu kisa wao ni
watumishi na wanasema katika mlima wa Bwana inapatikana, msichana
anakuuliza kuwa je ukinioa tutakula nini huna majibu na anajua kuwa
huyu kijana hajajipanga bado. Sasa ili kukuheshimu anatesema ngoja
nikaliombeee kumbe kakuheshimu tuu na hataki kukuabisha.
Kuna
kitu cha imani kimepita mahali na kina shida. Ukiwaukiza wako wapi
watakueleza jina la nyumba ya baba yao. Yesu anasema kanisa ni nyumba
alama ya kiroho kanisa inategemea jina la kanisa.. na wengine
ukiwauliza unasali wapi watakupa jina la Mtumishi na badala jina la
kanisa..
Na ina maana ni alama.. ukisema mimi ni mlutheri ina
maana una alama au mpetekoste inaonesha alama yao . Lakini akikuambia
jina la mtumishi ina maana alama aliyoweka mtumishi ni kubwa (sina shida
au ni vibaya ila nakufundisha tu namna ya kutafsiri haya mambo kiroho
kwanza). Pia mwingine ukimuuliza jina la mchungaji wako ni nani unakuta
hata hajui, ina maana kuna shida mahali mpaka umesahau jina la mchungaji
wako. Kwa sababu umeshindwa kukaa chini ya mchungaji na ndio maana
unasahau na jina lake .
Ardhi ni kama computer kubwa,
nikakanyaga hapa ardhi inajua huyu mtu ni nani.. Ardhi ya kule
nilikozaliwa inaleta ripoti na ile ya kule ninakoishi nayo inaleta
report kwa maana ardhi inatunza kumbukumbu na ndio maana Ukikataliwa
mjini utakataliwa na mashambani..
Yesu anapitisha kondoo
langoni.. na sio dirishani.. , na ndio maana na wewe ili utoke inabidi
upite mlangoni maana wanaopita dirishani ni wezi , sasa naenda kufanya
maombi hapa naunganisha ardhi ya hapa na ya huko kwako popote ulipo
unapotufuatilia. Weka mikono yako katika magoti yako .
Akani
alipokorofisha ardhi ilimeza wote wa nyumbani mwake, sasa chukulia
mmoja hayupo na kawaida ardhi inaambiana ina maana nae kule kule
alikokuwa nae alimezwa . ndio maana utakuta ardhi ya kwenu umewafunga na
wewe uko mbali na kwenu lakini utaona pale wenzio wanapochanua wewe
unachakaaa.
Baada ya hapo Mwalimu aliomba san asana.. pata
nafasi angalia somo hili Youtube na pia aliita watu kuokoka. Fuatisha
maandishi haya ili ufanye sala ya toba na baadae soma kitabu cha hongera
kwa kuokoka.
http://www.mwakasege.org/mafundisho/okoka.htm
http://www.mwakasege.org/mafundisho/hongera/utangulizi.htm
Toa Maoni Hapa Chini