SOMO: *HALI YA KIROHO YA ARDHI INAVYOHUSIKA NA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO*
ENEO: *DAR ES SALAAM*
SIKU: 2 March, 06 2017
MWL. C. MWAKASEGE
Leo tuangalie *NAMNA YA KUJIONDOA KWENYE MADHARA YA LANGO YA ARDHI YA NYUMBA UNAYOISHI INAPOMILIKIWA KIROHO YA NGUVU ZA SHETANI*
➡Ni
jambo pana na jipya kwa watu wengi neema ya MUNGU na iwe juu yako
kuweza kuona na kufahamu jambo hili maana kujua na kufunguliwa katika
jambo hili utafunguliwa katika mambo mengi sana
*Esta 8:1-2, 13-14*
*Mwz 22:17*
*Math 12:29*
*Kut 12:12-23*
*Tuangalie vipengele vichache vya jambo hili ili iwe rahisi kuelewa*
1⃣Ardhi na nyumba iliyojengwa juu yake vina uhusiano wa kiroho
➡Unasema unajuaje…..?
➡Kufuatana
na *Kumb 6:12* MUNGU amelinganisha nchi na nyumba kwa hiyo ardhi ile
ambayo ina mipaka halali inauhusiano wa kiroho na nyumba inayojengwa
2⃣Mlango wa nyumba una uhusiano na mlango wa ardhi
➡Kwanini? sababu kama ardhi ina uhusiano wa kiroho na nyumba basi na milango yao ina mahusiano
3⃣Ukigusa mlango wa ardhi kiroho unagusa pia mlango wa nyumba kiroho
*Matendo 16:26*
➡Tetemeko
lile halikuwa la kawaida lile la kuangusha nyumba bali lilikuwa lile la
kushughulika na ardhi ambayo juu yake gereza lilikuwa lipo
➡Sababu
walikuwa wapo gerezani kwa jinsi ya mwili isingekuwa rahisi wao kutoka
maana hawakufungwa kimwili bali kesi yao mpaka kufungwa kwao ilikuwa
kiroho
➡Ndiyo
maana MUNGU alileta tetemeko akatikisa misingi ya gereza na Biblia
inasema milango ya gereza ikafunguka haisemi ikavunjwa na vifungo
walivyokuwa wamefungwa vikaachia
➡Yule
askari alipoona milango iko wazi alitaka kujiua maana alijua wametoroka
lakini walimwambia asijiue akawakaribisha kwake akawanawisha miguu na
kuwatayarishia chakula na baada ya hapo walirudi gerezani
➡Kulipokucha asubuhi wale makadhi waliowafunga walitoa order ya wakina Paulo kuachiliwa.
➡Nini nataka uone hapa gereza halikuvunjwa wala kuwa na nyufa hata moja kutoka kwenye lile tetemeko
MUNGU hakuwa na shida na gereza la nje bali alikuwa na shida na gereza
la kiroho ambalo kwa jinsi ya nje watu wanaona kama vile kuta tu na
linaweza kuwa sehemu yoyote ile
➡MUNGU
alikuwa anashughulika na ardhi ili kushughulika na nyumba iliyo juu ya
ardhi akafungua milango ya ardhi ili kufungua milango ya gereza iliyoko
juu yake
➡Kama
nyumba yako ni ya utumwa imezungukwa na mazingira ya utumwa usihangaike
kuombea nyumba bila kuombea ardhi ya nyumba hiyo maana mlango wa ardhi
una uhusiano na mlango wa nyumba yako
➡Vita ya ardhi si vita ya kumshirikisha kila mtu maana ina mapamabano yake mabaya kama hujajipanga
➡Kama
huna NENO la kutosha ndani yako MUNGU akikusemesha huwezi kusikia maana
kusikia huja kwa *NENO la KRISTO* maana waweza kushughulika na ardhi
MUNGU akikwambia shughulikia mlango la ardhi
➡Wakina
paulo walienda kuhubiri wakatengeneza mahali pa kusali bila kucheck na
kushughulikia nani anamiliki lango la ardhi/nani ni mmiliki wa lile eneo
➡Waulize
watu wa nyumba ya Hamani maana kiroho nyumba yake ilikabidhiwa Esta na
Modekai sasa haijalishi kikao cha mirathi kimeamua nini maana wamiliki
ndio wanaoamua na kutoa ruhusa hali ya kiroho na hali ya maisha ya
nyumba hiyo inaendaje
➡Unaanzisha
kanisa/fellowship mahali badala ya kuangalia na kucheck nani
ameshikilia lango la roho nyingine inayopingana na kitu unachofanya na
ambaye ameshikilia lango la ardhi ambalo pia ndilo limeshikilia lango la
nyumba ya sehemu hiyo na msingi wa kiroho unayotumia kusali sasa kama
vifungo hivi vimefungwa kwenye ardhi na vikaja kuonenakana mpaka kwa nje
usipojua namna ya kuvifungua kwenye ardhi uwezi kufunguka
➡Angalia
habari ya kina Paulo kama waliendele na maombi kikundi cha cha ibada
kikavurugika wakafungwa jela hata baada ya kutolewa gerezani walifukuzwa
kutoka nje ya mji sababu walianzisha huduma mjini bila kusimamia
malango ya ardhi ya mji
*Matendo 16:39-40*
➡Walipotoka
gerezani walienda kwa Lidya na kukutana na ndugu/wapendwa tu na wale
wapendwa waliwafariji tu hawakuwa wa msaada nao wakaenda zao
➡Ndiyo
maana chunga sana watu wanaokushabikia huduma wakati hawajui vita
unayopitia, chunga sana watu wanakusumizia front line wakati hawajui
kupigana sababu ukifungwa gerezani watakufariji na kukupa pole na kusema
tunakuombea na wakati hawajui hata wanachoomba
➡Mji
ule ulikuwa na wapendwa lakini hawakuweza kuwasaidia kina Paulo sababu
inategemea ni nani aliyeshikilia lango la ardhi kiroho la mji ule.
➡Maana
walioshikilia kama hawaitaki huduma kuwa na uhakika itafungwa na watu
kuhamia kwenye huduma ama kanisa jingine hata kama wapendwa wapo na
usije fikiri watakusaidia watakufariji tu
➡Vikundi
vingi sana vya maombi watu hawajui ni kwanini ghafla vimechanua na
ghafla vimekufa sababu ni moja tu ulianzisha kikundi cha maombi bila
kushughulikia lango la ardhi ambalo Modekai ndiye aliyeshikilia lango
hilo na kama uko kinyume naye kuwa na uhakika kikundi hicho kitafungwa
kabisa
➡Ndiyo
maana unaweza kukuta makanisa mengine yanapata shida eneo hilo lakini
nyumba nyingine hazipati hiyo shida ama kanisa moja linapata shida na
jingine wala sasa ni mambo mawili au moja lina operate kwa viwango vya
juu sana au siyo tishio
➡Ndiyo maana watu wengi wanapata shida kwenye nyumba zao Biblia inaita nyumba za kitumwa na wako kwao.
➡Umewahi kufikiri kwa mfano hicho kiwanja ulichonunua ni nani anamiliki lango la hicho kiwanja katika ulimwengu wa roho?
➡Nani
amepewa kumiliki ardhi uliyojenga? Wengine alipewa marehemu sasa
ukichanganya jambo hili kiroho kuwa na uhakika kama usipojua namna ya
kutengeneza kisiwa cha ardhi ya kwako utapata shida sana kuvuka na vita
yake si nyepesi
4⃣Kama vile nyumba ilivyo na mlango zaidi ya mmoja vile vile na ardhi ina milango zaidi ya mmoja inayoweza kutumika kumfunga mtu
*Isay 26:1-2*
➡Nchi ili kurikaribisha taifa, taifa lazima lipite kwenye lango.
➡Anapozungumzia lango kwenye nchi anazungumzia lango la kwenye ardhi linaloruhusu watu kupitia, kuingia na kutoka
*Matendo 16:26-27, 24*
➡….milango… Biblia haituambii milango ilikuwa mingapi mlinzi alipoamka alikuta milango yote imefunguliwa na funguo anazo yeye.
5⃣Kila lango la kiroho katika ardhi au nyumba lina walinzi wa kiroho
*Matendo 12:6,10*
➡Kulikuwa na walinzi kwa ajili ya Petro na kulikuwa na walinzi kwa ajili ya mlango/nyumba
➡Kuna mapepo unapewa wewe ukitoka nyumbani unakuwa nayo na kuna yale yamepewa kulinda ardhi ya nyumba yako hayatoki.
➡Alipofika
kwa wapendwa waliokuwa wanaomba aligonga mlango (maana yake wakikupa
kibali na kukufungulia ingia) malaika halazimishi wapendwa kufungua,
wakati huku pengine malaika alimpitisha na milango kufunguka yenyewe.
Swala ni kwanini hawakumfungulia? maana yuke dada hakufungua mlango
baadaye walikuja wakamfungulia
➡Ardhi
ile ilikuwa na malango 4, walipita lindo la kwanza na la pili hata
mlango wa chuma na wa kuingilia mjini na mpaka kwa wale wapendwa
waliokuwa wanamwombea kuna watu ambao wamefunguliwa lakini wako
gerezani.
➡Fikiri
Petro kama malaika alipomtokea angemwambia avae nguo na viatu kisha
akapotea maana yake nini yuko huru keshavaa nguo na viatu lakini yuko
gerezani kafungwa hana uhuru tena
➡Ndiyo
maana tuna watu wengi sana tunawaombea na inapofika kwenye kufunguliwa
kwao tunafunga mlango tunatamani kuwaona kwenye chumba cha maombi lakini
kuwafungulia hatufanyi hivyo.
➡Wengi
tunawaombea halafu tukikutana nao tunakumbuka na kuona lile tatizo bado
kwako hata kama wamebadilika kwa hiyo tunajikuta bado hatujawafungulia
ghafla wanarudi gerezani
6⃣Omba kwa imani na kwa juhudi hadi aliyefungwa apite milango yote iliyomkwamisha
*Matendo 12:5*
*Waamuzi 5:8*
➡Kati ya eneo la uwanja la mapambano la MUNGU ni langoni
➡Petro
ililazimika avuke geti 4, mbili ndani ya gereza, moja ndani ya mji na
nyingine kwa waliokuwa wanamwombea hivyo MUNGU akikupa eneo la kuwavusha
watu na kukupa namna ya kuomba omba mpaka uwavushe geti zote
➡Wakati
mwingine unapohitaji msaada wa vita unahitaji watu ambao wanajua
kupigana uhitaji msaada wa pole hata kama ni pole bali hawata nyamaza
mpaka umetoka
➡MUNGU
atakupa mamlaka ya kukanyaga na kupita malangoni na kuachilia *DAMU YA
YESU* hapo maana hii ni ahadi ya MUNGU kwa Ibrahimu
*MAOMBI*
Angalia link hii kule mwishoni kushiriki maombi
https://youtu.be/ryFv_R47ScM
#MUNGU_akubariki_Mtumishi_wa_MUNGU_Mwl_C_Mwakasege
#Usiache_kumwombea_rafiki
#Usiache_kuombea_semina
#UFALME_KWANZA