SIKU 3. HALI YA KIROHO YA ARDHI INAVYOHUSIKA NA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO-MWL. C. MWAKASEGE | Apostle Darmacy Blog MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 | Apostle Darmacy Blog

APOSTLE DAMAS

Breaking News

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Thursday, February 23, 2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 

 

Goo

 

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 
About Muses Radio Player...
Version 2.1 (html5)

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.
-->

Tangaza nasi

Breaking News
Loading...

Soma App

Soma App
DOWNLOAD Somaapp NOW!

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Wednesday, March 8, 2017

SIKU 3. HALI YA KIROHO YA ARDHI INAVYOHUSIKA NA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO-MWL. C. MWAKASEGE


SOMO: *HALI YA KIROHO YA ARDHI INAVYOHUSIKA NA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO*
ENEO: *DAR ES SALAAM*
SIKU: 3 March, 7 2017
MWL. C. MWAKASEGE

*LENGO YA SOMO:*
Kuhakikisha ya kwamba Mafanikio yako yaliofungwa kwenye hali ya kiroho ya ardhi yanafunguliwa

*Kumb 6:12, 2Nyk 7:14*

*SUMMARY YA SIKU 2*

Pitia somo la siku ya kwanza na siku ya pili ili kujua tulipotoka maana kuna yale *mambo ya msingi 5 juu ya kufungua mafanikio yako yaliyofungwa na hali ya kiroho ya ardhi inayofanya mahali unapoishi pawe nyumba ya utumwa* siku ya kwanza na *vipengele 6 vya namna ya kujiondoa kwenye madhara ya lango ya ardhi ya nyumba unayoishi inapomilikiwa kiroho ya nguvu za shetani* kwa siku ya pili

Somo hili halifundishwi kama ile kawaida ila kila siku MUNGU anampa kitu kipya ili yule atakayesikiliza kwa siku hiyo atapata jibu lake

Si watu wengi pia wanalipokea kwa haraka sana mioyoni mwao somo hili na kwa sababu hiyo ROHO MTAKATIFU anarirudia na kurirudia ili lizidi kujengeka ndani yetu

Leo tuangalie *KUFUNGULIWA TOKA KWENYE KIAPO KILICHOIFUNGA NAFSI YAKO NA HALI YA KIROHO YA ARDHI*

Na katika kulitazama jambo tuangalie mambo kadhaa ambayo MUNGU ameachilia ndani ya kichwa cha Mtumishi ili yamkini yatufikishe mahali pa kuweza kuingia kwenye maombi na wale ambao kuna viapo vimewafunga wapate kufunguliwa

1⃣Njia mojawapo inayounganisha mafanikio yako kimaisha na hali ya kiroho ya ardhi ni maagano

*Mwz 9:13*
*2Nyk 7:14*

Anazungumzia juu ya kuiponya nchi yao na kumbuka nchi ni ardhi yenye umiliki halali na ina mipaka kabisa. Biblia ya kingereza imewaka wazi kabisa inazungumzia juu ya ardhi (land)

Sasa tazama kitu ambacho MUNGU alifanya wakati Nuhu ametoka kwenye safina wako watu wachache waliojulikana kama wapo na wanyama na ndege, ukisoma ile sura ya 8 na 9 na alipozungumza nao kwa habari za agano

..Anasema ni ishara ya agano kati yangu na nchi na hasemi ni ishara ya agano kati yangu na wewe bali ni ishara ya agano kati yangu na ardhi

2⃣Ishara ya agano hilo juu ya ardhi husika kazi yake ni hizi zifuatazo:

*MOJA* (i)
Kazi kubwa mojawapo ni kukumbusha kuwepo kwa agano

*Mwz 9:13-16*

*Tazama maneno haya*….nami nitalikumbuka agano langu lililoko kati yangu na ninyi…..

Kukumbusha kwa watu wote waliohusika na maagano, kiswahili kinakosa lugha iliyo nyepesi sana juu ya neno agano maana tukisema ni mapatano halitoshi au mapatano ya kimkataba linasogea kidogo maana agano ni pana kidogo

Jambo ambalo watu wengi hawafahamu Agano haliwezi kuwa Agano isipokuwa kuna kitu cha kiroho kati yake, kunaweza kuwa na mapatano lakini hakuna kitu cha kiroho kati yake

*MBILI* (ii)
Kukumbusha kuwepo kwa kiapo kwa sababu ishara ni alama ya uaminifu kwenye kiapo husika

*Yosh 2:11-13-19*

Rahabu alipokuwa amegundua ukombozi wake umekaribia, kivipi ni kwa imani kama Waebrania isemavyo, kwa hiyo hakuangamia pamoja na waovu wengine sababu aliwakaribisha wale wa pelelezi kwa furaha, kwa shukrani na kwa imani

Swali la msingi kwanini MUNGU asiwapitishe pembeni ya mji wa Yeriko kwa safari yao ya kwenda Kaanani? Maana mji ule uliangamizwa wote na watu wakao humo isipokuwa Rahabu na familia yake na hata wakati wanaondoka Joshua aliachilia laana ili asiwepo mtu wa kujenga hapo

Fahamu ili kilichomfanya MUNGU aende Yeriko ni Rahabu peke yake hakuna kitu kingine chochote kilimpeleka kule maana Rahabu alikuwa na destiny, alikuwa na kitu katika maisha yake na shetani alifikiri akiachilia uasherati ndani yake na kumfunga katika ardhi ya mji wa yeriko hakuna atakaye mkumbuka. Ukitizama utaona tokea pale MUNGU alimwamisha na kumwingiza katika familia ya wayahudi yeye pamoja na familia yake na kumjengea maisha yake ya baadaye

Mji waYeriko ulifungwa wote kwa jinsi ya kiroho si ya mwili na ndiyo maana ilifunguliwa kwa jinsi ya kiroho. Gharama zote za kuuzunguka mji ule siku zote 7 kama angeulizwa angejibu ni Rahabu ndiyo maana walinyamazishwa

Kuna kitu MUNGU anaweka katika maisha yako na shetani anajaribu kukuzamisha kabisa, haijalishi mahali ulipo, haijalishi shetani amekufunguka kwa namna gani kama ni katika uasherati ama wizi au shida ili kusudi ile ndoto MUNGU aliyoweka ndani yako isije kuchipua *SIKIA NENO LA BWANA MUNGU ATAKUFUATILIA NDANI YA YERIKO NA ATAKUTOA NA SI TU KUKUTOA YERIKO NA ATAKUTOA KATIKA UASHERATI* atakuweka katikati ya watu ambo kila mtu atashangaa umetokea wapi na hawataacha kusema IMANI yake imemtoa pale na kumfikisha hapa na kusema yuko *MUNGU ambaye anaweza kushughulika na ukahaba*

Ilichukua jeshi lote la Israeli kumtoa mtu mmoja

*“Ndiyo maana saa nyingine ninaposimama kwenye madhabahu huwa sijaribiwi kufikiri na wingi wa watu nafikiria kuangalia mtu mmoja ambaye MUNGU amemkusudia”*

Rahabu aliwaapisha kwa kusema ninawaapisha kwa BWANA, maana yake ninawafunga kwa MUNGU wenu alafu akasema wampe alama ya uhaminifu, wakasema tusije tukaingia hatia ya kiapo ulichotuapisha…funga kamba hii, wale wapelelezi walikuwa wanatembea na kamba nyekundu ni kamba waliyokuwa wanatembea nayo ili ijulikane ni watu wa agano.

*TATU* (iii)
Kukumbusha masharti yaliyoambatanishwa na kiapo

Hakuna kiapo kisichokuwa na masharti ili kuonyesha hakuna agano lisilokuwa na masharti na ni masharti ya kisheria na kihalali ile roho iliyowaunganisha kwenye agano kazi yake ni kufuatilia masharti

Ndiyo maana alipowaapisha kwa BWANA walimpa masharti:
Huruhusiwi kusema
Hakikisha ndugu zako unaowataka waje aje
Hawaruhusiwi kutoka nje

3⃣Kiapo cha agano kinabeba wahusika wakufuatiliwa

*Yosh 2:12-13*

Rahabu wakati anazungumza na wale wapelezi hata kuingia kwenye kiapo ndugu zake hawakuwepo lakini aliingiza jina la baba, mama yake na ndugu zake na listi ya vitu walivyokuwa navyo kwa hiyo kila kilichotajwa hakikurusiwa kuwa nje ya nyumba

Kuna watu ndani yamioyo yao MUNGU amewabebesha familia, wengine kampuni, wengine kanisa unamwona yuko peke yale lakini hayuko peke yake ndani yake amebeba majina ya watu na vitu vyao na kila mahali anawakumbuka kwamba anao.

Kumbuka habari ya yule tajiri aliwabeba ndugu zake aliokuwa anawabeba kwenye pesa na alijua watapita na kuja njia hii hii wale ndugu watano akataka wapelekewe taarifa mapema

Joshua alipewa watu wa kusafiri nao na watu wote wale urithi wao ulikuwa kwa Joshua

Watu wa namna hiyo katika ulimwengu wa roho wana alama zao ambazo zinafuatailiwa kila wakati na unapoingizwa kwenye kiapo haijalishi kwamba umekubali ama hujakubali swala ni kwamba aliyekuingiza kwenye kiapo ana sauti gani juu yako..kupitia kwenye kizazi, uhalali wa kukaa mahali pamoja

Kama mwenye nyumba ameapa kwa mungu wake juu ya ardhi ya hapo kwake ambayo na wewe unakaa maana yake amekuingiza kwenye kiapo

Ndiyo maana viapo vya maagano vinasumbua sana maana vinafunga watu hata kama hawajui kama wamefungwa

4⃣Kiapo kinafungamanisha nafsi ya mtu na alichojiapiza

*Hes 30:2* (Mahusiano ya kiroho kati ya baba na binti yake)-Daka hiyo ilikuwa aja ya Mtumishi akafundishwa na MUNGU

Kwa hiyo kiapo ni kifungo na kiapo kinafunga nafsi na kitu ambacho mtu ajiapiza nacho

Rahabu alipowaambia niapie kwa BWANA alikuwa anafunga nafsi za wale wapelelezi kwa kitu watakacho kisema, walijua kabisa huyu anazungumza kitu cha kiagano

*Math 5:33-36*

YESU alizuia viapo mahali ambapo havitakiwi kuwepo, kuna vitu alivitaja kwa maksudi kabisa:-
Usiape kwa kichwa chako
Usiape kwa mji wa Yerusalem
Usiape kwa mbingu na
Usiape kwa mji
Usiape kwa ardhi

YESU kwa lugha nyingine alikuwa anatufundisha kuwa waangalifu katika kuapa maana kuapa ni kuifunga nafsi yako na ardhi na roho iliyoko mahali pale inabana hayo maneno uliyotamka mahali hapo

5⃣Ishara ya agano inafanya wahusika wafuatiliwe katika ulimwengu wa roho kujua ikiwa masharti ya kiapo yanazingatiwa

Ukisoma habari za MUNGU na agano lake la Ibrahim , Isaka na Yakobo utakuta anasema …kile kiapo nilichowaapia baba zako…MUNGU anamwambia Musa sijakufuata kwa ajili yako ila jina lako kwenye kiapo, nifuatilie toka ukiwa tumboni, nicheck utavyoishi na kula saa ikifika nijifunue kwako, nataka kucheck kama unafuata masharti

Wewe unaweza kusahau juu ya masharti ya kiapo lakini MUNGU hawezi kusahau

Miungu inaingia mikataba katika ardhi kwamba ikufanikishe ama isikufanikishe katika ardhi kwa nini sababu kwenye ardhi ndiko kulikowekwa siri ya mafanikio ya hapa duniani.

Ulimwengu mwingine wowote hauna udongo kasoro ardhini na mbegu zote za kiroho ziliwekwa ardhini kwa sababu Sura ya kwanza inasema kila kilichoumbwa kilikuwa ni neno na neno ni mbegu na sura ya pili kila kilichochipuka kilichipuka kutoka kwenye udongo kwa hiyo lile neno lilikuwa mbegu lilivyotamkwa MUNGU akaliweka kwenye udongo kwa hiyo udongo una mbegu za kiroho

Siri ya mavuno yako iko kwenye ardhi, siri ya hali ya hewa iko kwenye ardhi na hii ni ishara ya agano MUNGU aliyoweka na Nuhu kwamba katika vitu alivyowekeana naye na ardhi ipo na kama ipo kuwa na uhakika na mbingu yake ipo maana hutegemea na kufanya kazi pamoja

6⃣Badala ya kukimbilia kuvunja agano badilisha na tangua kwanza kiapo ili kuliondoka jina lako na nafsi yako kwenye kifungo

*Hes 30:2,10-15*

Usipotangua kiapo yote yaliyosemwa kwenye kiapo yatatokea

Rahabu aliwaapisha kwa BWANA hakulijua agano likoje lakini alijiingiza kwa njia ya kiapo na kuvunja lile agano ilikuwa kutengua kile kiapo kwamba watu wale/ndugu zake wasikae ndani ya ile nyumba/ ndani ya lile agano.

Sasa kiapo kile hakitawafunga hata kama agano lipo

Shida watu wengi sana wanakimbilia kuvunja agano wasilolijua limefungwaje na limefungiwa wapi na vitu gani vimehusika kwenye agano.

Usijaribu kumkwamua mwingine wakati wewe umekwama toka wewe kwanza

Joshua aliwaambia watu chagueni hivi leo ila mimi na nyumba yangu tutamtumikia MUNGU wakasema nasi tutamtumia huyo MUNGU akawaambia kwanza ondoeni alama za miungu yenu kwanza

Ukifunga nafsi kwa kiapo usipotangua kila ulichokisema kitatokea na kinaweza kukusumbua miaka na miaka. Unatangua kwa kutumia *DAMU YA YESU* maana ni DAMU ya AGANO na ni *DAMU BORA* kuliko damu zozote zile

7⃣Miguu yako ni lango rahisi la kutumia kuifunga nafsi yako na ardhi katika kiapo cha kiroho

*Zab 56:6*
*Zab 57:6*

Shetani anatumia nyayo kushika nafsi yako kwa hiyo anaotea nyayo zako. Shetani amekuwekea nyavu kwenye miguu lakini usikii nyavu unasikia moyoni mwako kukata tama, kila ukikanyaga husogei mpaka umeacha kutembea

Sasa unaweza kujua kwanini Rahabu alipokuwa anataka kutolewa kule ilibidi wazunguke kwa miguu siku zote zile, sababu miguu ya watu wa MUNGU inaweza kuachilia nguvu za MUNGU inapokanyaga mahali

Walipokuwa wanazunguka walikuwa wanatafuta misingi ya ile kuta zile hazikuwa kuta zimejengwa kawaida bali zilikuwa kuta za kiroho, sababu ile ardhi ilikuwa na misingi ya kiroho 7 na ule wa 7 ulifungwa mara 7. Kile kitu na kila mahali kulianguka chini kasoro nyumba ya Rahabu misingi mingine yote ilibomoka

Kuokoka kwako na kupona kwako si sababu ya matendo yako bali *ALAMA YA DAMU YA YESU moyoni mwako*

 

*TANGAZO MUHIMU*
👌🏽Jumamosi asubuhi kama una huduma ya ualimu hata kama hujui njoo kuna mafundisho na shule ya ualimu kujua na kutambua

👌🏽Na tarehe 14 May Diamond Jubilee siku ya vijana

👌🏽Kila siku maombi yatakuwa yanafanyika mahali hapa kufuatata na somo la siku hiyo

*Video ya somo*: https://youtu.be/91O3UI_0E30

 

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.