SIKU 4. *HALI YA KIROHO YA ARDHI INAVYOHUSIKA NA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO* *MWL MWAKASEGE* | Apostle Darmacy Blog MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 | Apostle Darmacy Blog

APOSTLE DAMAS

Breaking News

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Thursday, February 23, 2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 

 

Goo

 

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 
About Muses Radio Player...
Version 2.1 (html5)

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.
-->

Tangaza nasi

Breaking News
Loading...

Soma App

Soma App
DOWNLOAD Somaapp NOW!

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Thursday, March 9, 2017

SIKU 4. *HALI YA KIROHO YA ARDHI INAVYOHUSIKA NA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO* *MWL MWAKASEGE*

4⃣SOMO: *HALI YA KIROHO YA ARDHI INAVYOHUSIKA NA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO*

ENEO: *DAR ES SALAAM*

SIKU: 4 March, 8 2017

MWL. C. MWAKASEGE

*TANGAZO MUHIMU*
👌🏽Jumamosi asubuhi kama una huduma ya ualimu hata kama hujui njoo kuna mafundisho na shule ya ualimu kujua na kutambua

👌🏽Na tarehe 14 May Diamond Jubilee siku ya vijana

👌🏽Kila siku maombi yatakuwa yanafanyika mahali hapa kufuatana na somo la siku hiyo

Video ya somo:   https://youtu.be/mU9O0mTgBrU

*LENGO YA SOMO:*
Kuhakikisha ya kwamba Mafanikio yako yaliofungwa kwenye hali ya kiroho ya ardhi yanafunguliwa

*Kumb 6:12, 2Nyk 7:14*

*SUMMARY YA SIKU 3*
✳Pitia somo la siku ya kwanza mpaka siku ya tatu ili kujua tulipotoka na yale mambo ya msingi 5 juu ya kufungua mafanikio yako yaliyofungwa na hali ya kiroho ya ardhi inayofanya mahali unapoishi pawe nyumba ya utumwa siku ya kwanza na vipengele 6 vya namna ya kujiondoa kwenye madhara ya lango ya ardhi ya nyumba unayoishi inapomilikiwa kiroho ya nguvu za shetani kwa siku ya pili na kwa siku ya tatu tulijifunza mambo 7 juu ya kufunguliwa toka kwenye kiapo kilichoifunga nafsi yako na hali ya kiroho ya ardhi

➡Leo tuangalie *HATUA ZA KIMAOMBI KWA AJILI YA KUJITOA KWENYE KIFUNGO CHA KIAPO KILICHOUNGWA NA ARDHI*

➡Ziko hatua nyingi lakini tujifunze kama mtaji wa kukutoa

1⃣Omba MUNGU akupe kujua eneo la ardhi lililotumika/tumiwa kukufunga nafsi yako kwa njia ya kiapo

*Yosh 6:22-23*
*Yosh 2:8-18*

➡Kiapo hiki cha sura ya 6 kilifanyika sura ya 2

➡Kuna maneno ya msingi mawili katika sura ya 2 nataka uone
i)mstari wa 12…..Niapieni kwa BWANA

ii)mstari wa 17….. Sisi tunataka tusiwe na hatia kwa ajili ya kiapo hiki tulichokuapia

➡Sasa mambo mawili ya msingi

i)Kile kiapo kilifunga pande zote mbili kilimfunga Rahabu na kiliwafunga wale wapelelezi

i)Kile kiapo walikiweka kianze kufanya kazi namna gani na katika eneo lipi

➡Walimpa alama ya uhaminifu kuweka katika dirisha na ikashikilia nyumba yake na ule ukuta ulipoanguka lile eneo la nyumba lilipobaki pale pale na Rahabu hakutoka mpaka ametolewa na kwa sababu hiyo kile kipindi cha kiapo kufanya kazi maana alisema mtakapoingia kwenye mji huu mtakapo kaa kwenye nyumba hii waliweka eneo la kiapo

➡Kabla hawajaingia katika ile inchi kile kiapo kilikuwa hakiwasumbui maana Rahabu alikuwa anaweza kutoka na kuingia lakini wakikanyaga wana wa Israeli Yeriko kiapo kinaanza kufanya kazi na kiapo kile kilikuwa kinawafunga mpaka maelekezo ya kuwatoa yalipofika

➡MUNGU alijifunga kwenye kiapo na Ibrahimu kuwafanikisha wana Israeli katika nchi ya Kaanani wala si misri na akajiwekea na muda miaka 400 na alipowafuata alisema amekumbuka agano langu, alitaka kutimiza kiapo alichomwapia ibrahimu.

➡Misri hawakufungwa na kiapo huku kanan kiapo cha ndipo kilifanya kazi ya kuwafanikisha maana kuwafanikisha Misri ni nje ya agano

➡Yusufu alikuwa na upako nje ya agano alibarikiwa nje ya agano, hata ishmail alibarikiwa nje ya gano, essau alipewa eneo la kukaa, Lutu alipewa eneo la kukaa, pamoja ya kwamba MUNGU amewapa lakini alikuwa la kiapo alikuwa na Baraka ya kiagano ndani yake

➡Msihi MUNGU sana akuonyeshe kama ipo ardhi yoyote ambayo imekufunga kwa kiapo, unaweza kufungwa kwenye eneo unaloishi, unalofanyika kazi ama ibada ama kwenye eneo la familia yenu.

2⃣Omba maombi ya TOBA kwa ajili ya mambo mawili makubwa

*MOJA*
Maovu ya wazazi ya kukufunga kwenye kiapo kinachounganisha ardhi na miungu yao

*MBILI*
Kwa ajili ya dhambi yaw ewe mwenyewe kujifunga kwenye kiapo cha ardhi..waweza usijue lakini kama umefika katika kiwango fulani cha kutafuta msaada utaelewa

➡ *Dan 9,10* TOBA kwa ajili ya dhambi zao na uovu za wazazi wao.MUNGU anaweza kukupa si tu kuombea uovu wa wazazi hata kama hukufanya wewe maana TOBA inakazi nyingi sana

✅Ina zaidi ya kusamehe
✅Kubwa zaidi nataka uone hapa ni kumfungulia MUNGU uhalali wa kisheria kushughulika na kesi yako

➡Baada ya mwanadamu kumkorofisha MUNGU na dhambi kuingia ikaleta mauti mahusiano ya mtu na MUNGU yalikatika ndiyo maana kuna vitu MUNGU hawezi kujibu wala kukupa bila kusema na kuhitaji usiposema hawezi kukusaidia lazima ufanye TOBA na kumwamini YESU kama BWANA NA MWOKOZI wako halafu umfungulie mlango kukusaidia yaani maombi ya TOBA

3⃣Batilisha kiapo hicho juu yako

*Hes 30:2,14-15*

➡Biblia inapozungumza juu ya kubatilisha kiapo au batili inazungumza juu ya kuondoa uhalali wa hicho kitu juu yako ambayo ni kukuondoa kwenye ushiriki kama jina lako lipo na umeingizwa kwenye kiapo hujui. Mfano kama una cheti batili na ndicho umekitumia kupata kazi anapotokea mwenye nacho na kusema hicho ni batili jua umepoteza kazi

➡Kubatilisha kiapo ni swala la kiroho ambalo unaweza kulitumia kwa DAMU YA YESU KRISTO kwa hiyo unapoanza ngazi ile ya maombi ya toba inakuweka mahali pazuri kwa kuwa na msaada wa MUNGU kuwa upande wako kwa ajili ya kubatilisha maana kama MUNGU hayupo upande wako usijaribu kubatilisha kitu ambacho shetani alishirikiana na watu wengine kuingiza jina lako halafu kwa nguvu zako unasema hii ni batili

➡Bibilia inasema kuna sheria ya ROHO WA UZIMA, sheria ya ROHO WA UZIMA ufanya kazi chini ya DAMU YA YESU, sheria hii hukuacha mbali na sheria ya dhambi na mauti

4⃣Tangua kiapo

➡Kutangua kiapo inahusisha kuondoa uhalali wa vifungo kuendelea kukufunga au kukuzuia

➡Kutangua kunahusika na vifungo
Kubatilisha kunahusika na ushiriki

➡Mfano mtu gari yake ni mbovu unaipeleka garage na fundi anasema kaa chini nikufundishe kutengeneza gari ili ukipata breakdown njiani utengeneze mwenyewe kwahiyo mafundisho haya ni kutaka kukufundisha jinsi ya kutengeneza gari. Na watu wengi hawana uvumilivu kupata maarifa ya kutengeneza gari wengi hutaka kuacha gari garage na kusema nirudi saa ngapi kuchukua, utafikiri anajua hatua za utengenezaji wa icho kilichoharibiga

5⃣Futa kwa DAMU YA YESU alama za uaminifu zinazofanya ufuatiliwe na utambulike

➡Na mara nyingine ukitambulika unatambulika kabisa wewe ni wa agano lipi maana kuna mahali wataangalia hadi alama

*Yosh 2:17-18*

➡Walimwambia weka kamba hii nyekundu maana aliwaambia nipeni alama kiapo tu peke yake hakitoshi, kiapo kinaambatana na alama, ile alama ya kamba nyekundu ina maana fulani. Kamba ikikosekana na nyumba ya Rahabu inaenda chini maana kamba inafanya ufutailiaji uwe mwepesi

➡Alama inaweza kuwa imewekwa ndani ya damu yako, ndani ya mwili na nafsi kuweza kutoonekana kirahisi kwa macho ya nje na alama nyingine ziko kwa jinsi ya nje kama mavazi, pete n.k sasa huzifuti tu wa jinsi ya kawaida kama kuchoma na kutupa ukifikiri umefuta rohoni, bali ni *DAMU YA YESU* pekee inaweza kuingia ndani na kufuta kabisa

6⃣Kemea mapepo yanayotumia kiapo kukwamisha maisha yako

➡Mahali popote penye kiapo pana agano, mahali popote penye agano pana kitu cha kiroho na ngazi tofauti tofauti

➡Na unapo kemea, kemea kwa kutamka kabisa *“mapepo mnaofanya kazi kwa uhalali wa kiapo hicho kiapo nimebatilisha, nimetangua, nimefuta alama za uaminifu hamna uhalali wa kuendelea kukaa ninawahamuru katika JINA LA YESU achia nyumba yake, mafanikio yake, maisha yake, biashara zake…utaongozwa na ROHO MTAKATIFU kutamka ni eneo lipi huyo mtu kabanwa”*

➡Ndiyo maana unahitaji kusimama kwenye nafasi yako vizuri maana mapepo yaliyokaa sehemu kihalali uwa yanatafuta kukata rufaa, huwa yanatafuta kukusumbu na kucheck kama unajua kitu unachofanya. Mfano mzuri ni Paulo na Silla walikemea pepo la kijakazi wakaishia jela

7⃣Omba uponyaji wa nafsi hasa eneo la akili ili ziweze kukusaidia zaidi ya mipaka ya kiapo kilichokufunga

*Ayubu 32:8*
…Na pumzi za mwenyezi huwapa akili

*Mwz 2:7*

➡Akili ziko kwenye nafsi, akili zimeletwa ndani ya mtu na pumzi ya MUNGU wakati anamuumba mtu. Njia mojawapo ambayo ulimwengu wa roho unatumia kushika nafsi za watu ni kwa kutumia nyazo zao na miguu yao na kwa ajili hiyo kwa sababu miguu ugusana na ardhi maagano mengi na vaipo vingi vilivyopo ndani ya ardhi vinaelekezwa kwenye nafsi na vikifika kwenye nafsi uenda kwenye akili na akili zinakuwa blocked huwezi kufikiri zaidi ya mipaka ya kiapo. Mfano wastaafu akisha staafu kama hajatoka na kufunguliwa kwenye kiapo

*Ez 21:21-23*

➡Mtu alienda kufanya uganga kwenye njia panda na anawafunga watu kwenye kiapo kwenye njia panda, shetani anaweka jina lako kwenye njia panda kukumaliza kwenye maamuzi, watu wengi  wanaenda mpaka njia panda wanashindwa kuamua wanakuwa na mawazo mengi, mipango mingi na ukiwauliza wanakwambia hawajui wafanye lipi maana kimawazo wana mambo mengi

➡Rahabu ilibidi atolewe ili kutekeleza mawazo yake nje ya kiapo. Hujatoka basi umebanwa hapohapo hutatoka. Mfano mtoto amemwamisha shule gafla matokeo yake yanashuka

8⃣Pokea jibu la maombi kwa IMANI ndipo upokee kwa kuona

*Mark 11:23-24*

➡Kuna mahali pa kusema na kuomba
✳23: Kama unasema sema kwa Imani ukiamini kwamba hayo usemayo yametukia

✳24: Kama unaomba omba amini ya kwamba ulichoomba MUNGU amesikia na kujibu

➡Pokea kwa imani kwanza maana ukishaamini MUNGU amefanya kuna hatua ROHO MTAKATIFU atakupelekea hatua kwa hatua hata kukwambia ulichokiomba kimefika madhabahuni na kimejibiwa kwa hiyo utabadili maombi na kuanza kushukuru

➡Kuna mwingine hatoki mpaka umemtangazia kufunguliwa kwake…Paulo na Sila waligoma kutoka mpaka walipoambiwa wamefunguliwa kwa hiyo kama unamuhudumia Paulo na sila uwatangazie

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.