SIKU 7: SOMO: *HALI YA KIROHO YA ARDHI INAVYOHUSIKA NA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO* MWL. C. MWAKASEGE | Apostle Darmacy Blog MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 | Apostle Darmacy Blog

APOSTLE DAMAS

Breaking News

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Thursday, February 23, 2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 

 

Goo

 

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 
About Muses Radio Player...
Version 2.1 (html5)

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.
-->

Tangaza nasi

Breaking News
Loading...

Soma App

Soma App
DOWNLOAD Somaapp NOW!

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Sunday, March 12, 2017

SIKU 7: SOMO: *HALI YA KIROHO YA ARDHI INAVYOHUSIKA NA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO* MWL. C. MWAKASEGE

7⃣SOMO : *HALI YA KIROHO YA ARDHI INAVYOHUSIKA NA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO*

ENEO: *DAR ES SALAAM*

SIKU: 7 March, 11 2017

MWL. C. MWAKASEGE

*TANGAZO MUHIMU*
👌🏽Na tarehe 14 May Diamond Jubilee siku ya vijana

👌🏽Kila siku maombi yatakuwa yanafanyika mahali hapa kufuatana na somo la siku hiyo

👌🏽Kesho ukiweza kufunga funga kwa ajili ya maombi maana kesho muda wa maombi utakuwa mrefu

*LENGO YA SOMO:*
Kuhakikisha ya kwamba Mafanikio yako yaliofungwa kwenye hali ya kiroho ya ardhi yanafunguliwa

*Kumb 6:12, 2Nyk 7:14*

_ndipo ujitunze, usije ukamsahau BWANA aliyekutoa nchi ya Misri, nyumba ya utumwa._
KUM.6:12

_ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe *dhambi yao, na kuiponya nchi yao.*_

*SUMMARY YA SIKU YA 6*
✳Pitia somo la siku ya kwanza mpaka siku ya tatu ili kujua tulipotoka na yale mambo ya msingi 5 juu ya kufungua mafanikio yako yaliyofungwa na hali ya kiroho ya ardhi inayofanya mahali unapoishi pawe nyumba ya utumwa siku ya kwanza na vipengele 6 vya namna ya kujiondoa kwenye madhara ya lango ya ardhi ya nyumba unayoishi inapomilikiwa kiroho ya nguvu za shetani kwa siku ya pili, siku ya tatu tulijifunza mambo 7 juu ya kufunguliwa toka kwenye kiapo kilichoifunga nafsi yako na hali ya kiroho ya ardhi na kwa siku ya nne tulijifunza hatua 8 za kimaombi kwa ajili ya kujitoa kwenye kifungo cha kiapo kilichoungwa na ardhi na pia siku ya sita tulijifunza

Leo tuzungumze juu ya *HATUA ZA KIMAOMBI ZA KUCHUKUA ILI KUONDOA TATIZO LA UKIWA KATIKA ARDHI ILI UFANIKIWE*

*Ezekiel  15:8*
_Nami nitaifanya nchi kuwa *ukiwa, kwa sababu wamekosa, asema Bwana MUNGU.*_
EZE. 15:8

➡Ukiwa ni adhabu au hali ya kiroho inayoashiria kwamba eneo hilo liko kwenye adhabu. Shetani haleti ukiwa bali hutumia ukiwa kusumbua watu. Ukiwa ni adhabu halali kabisa ambayo MUNGU anaichachilia kufuatana na maandiko kwa sababu kuna kosa kwenye hilo eneo

➡Si mapenzi ya MUNGU mahali pawe na ukiwa maana MUNGU aliumba dunia ikaliwe na watu pasipo ukiwa. Ukiwa ni adhabu

➡Hatua hizi zitakuwa mtaji kwako angalau utapata mtaji mkubwa sana wa kuomba utakapotaka kuomba

1⃣Omba MUNGU akupe ufahamu ikiwa ardhi inayohusika na nyumba inayokuhusu inayo tatizo la ukiwa

*Yer 4:27-28*_Maana BWANA asema hivi, Nchi yote itakuwa ukiwa; lakini sitaikomesha kabisa. Kwa ajili ya hayo nchi itaomboleza, na mbingu zitakuwa nyeusi; kwa sababu mimi nimeyanena haya, na kuyakusudia, wala sikujuta wala mimi sitarudi nyuma niyaache._
YER. 4:27‭-‬28  Na kufutana na *2Nyk 7:14* *kuiponya nchi yao*

➡Nchi ni ardhi yenye mipaka halali ya kiumiliki kwa hiyo unaposoma kwenye Biblia juu ya nchi itakufungulia macho kwenye vitu vingi

➡Si kila ardhi yenye matatizo ina ukiwa na si kila mahali penye ukiwa huo ukiwa uko kwenye ardhi unaweza ukawa juu ya mtu kama ilivyokuwa kwa Tamari. Unaweza kuombea hiyo ardhi mpaka ukachoka maana ukiwa haupo kwenye ardhi bali mtu aliokuja nao ameambukiza eneo hilo

➡Ukishajizoeza kumsikiliza MUNGU juu ya kukusemesha kwenye ukiwa utajua tu ukiwa huu unasababishwa na nini je ni ndani ya mtu ama ndani ya ardhi

➡Kiroho moyo wa mtu umeumbwa kama ardhi, Biblia inasema NENO ni mbegu linapandwa katika ardhi na linapandwa katika moyo, moyo ambao hauwezi kupokea NENO linapandwa pembeni shetani anakuja kulichua, udongo tifutifu unafananishwa na moyo ambao uko tayari kwa ajili ya kupokea. Kwa hali ya udongo inavyofanya kazi kiroho na hali ya moyo au ya kiroho katika nafsi yako kuna vitu ambavyo vinafanana ambavyo ukifuatilia vinaweza kukusaidia. Ni rahisi sana kwa moyo wako kudaka kitu ambacho ardhi inasikia, inaposikia moja kwa moja kama ardhi iliyopo mahali hapo ina maombolezo ndani yake kule kuomboleza utakusikia ndani, yaani ukisha kuja na kukanyaga utasikia maombolezo ndani yako

➡Wapo watu wanakaa bila kumalizia nyumba miaka 10 na hana maelezo kwanini hawezi maliza, sasa si kila mtu aliyeshindwa kumalizia nyumba na kujenga swala ni ardhi, sasa tafuta kiwakilishi chochote iwe ramani, hati halafu omba mpaka MUNGU aseme ndani yako na utasikia tu.

➡Utakapoanza kusikia hali ya ukiwa usikimbilie kuomba maana lazima ujue hiyo hali ina ujumbe gani ndani….unasema nitajuaje? Jana tulisoma *Mwz 1:2*_*Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji*; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji._

➡ROHO WA MUNGU alitulia pale hakufanya kitu chochote hakubadilisha mazingira yaliyokuweko kazi yake ilikuwa kufunua kilichopo pale, kulikuwa na ukiwa, kulikuwa na utupu

➡Nguvu za MUNGU zinaweza kushuka mahali hazibadilishi kitu zinakueleza shida iliyoko, kwa hiyo ile kukanyaga na ukasikia ukiwa haina maana ROHO MTAKATIFU amemaliza kukusemesha lazima uwe na UTULIVU kama ROHO MTAKATIFU ametulia na wewe unapaswa kutulia ili amalize kukukamilishia kilichoko ndani sababu inawezekana kati ya hivi

*CHA KWANZA*
Unapewa taarifa na ROHO kuwa eneo hilo liko chini ya adhabu ya MUNGU iitwayo ukiwa

➡Ukiwa kwenye sura ya kwanza ya mwanzo ulichanganyika na utupu na giza, ukiwa ule wa Tamari ulichanganyika na hasira na uchungu na kulipiza kisasi, unaenda ukiwa mwingine umenyanganya furaha ndani, mwingine una maombolezo, ukiwa mwingine unanyang'anya utoaji sadaka kanisani.

*CHA PILI*
Unataka kukuonyesha kwamba kuna kosa lililofanywa na mtu au watu waliomiliki au waliokaa eneo hilo kabla yako lililosababisha hiyo adhabu

*Ezekiel  15:8*
_Nami nitaifanya nchi kuwa *ukiwa*, kwa sababu wamekosa, asema Bwana MUNGU_

✳Vipengele unavyoona hapa
✅Inakuonyesha wazi kabisa nchi itakuwa ukiwa sababu imekosa hivyo ukiwa ni adhabu

✅Kuna kosa limefanyika na mtu aliyekuwa anamiliki kabla yako au ni kosa lako wewe mwenyewe, maana kuna adhabu za kimaonezi katika ulimwengu wa roho na kuna adhabu za kihalali na zote hushughulikiwa tofauti

✅Kosa hilo liwe limefanywa na wewe au mtu mwingine linatakiwa kurekebishwa kwa TOBA la sivyo eneo hilo la ardhi haliwezi kuendelezwa ipasavyo

➡Ukikanyaga eneo ukasikia hiyo hali hizi taarifa tatu huwezi kuzikosa ndani ya ROHO MTAKATIFU
Pana
✅Adhabu
✅Kosa
✅Hilo eneo lirekebishwe au hilo tatizo lirekebishwe la sivyo haliwezi kuendelezwa kabisa

➡Kwa hiyo taarifa hizi unapopewa zinakusaidia namna ya kujipanga. Saa nyingine unapoenda kuomba MUNGU anaweza kusema na wewe kwa njia ya ndoto kwa sababu kwa njia ile ya kawaida ndivyo Biblia inavyotaka uwe na uwezo wa kumsikia MUNGU kwa njia ya ROHO MTAKATIFU maana yeye ni muhusika Mkuu wa kukushirikisha mambo ya MUNGU na mambo yote katika ulimwengu wa roho sasa si kila mtu anauwezo wa kumsikia maana wengi wetu hukosa utulivu au si wengi wanaweza kudaka ndiyo maana MUNGU husema mara nyingi kwa njia ya ndoto kama alivyosema na Yakobo alipolala eneo liitwalo luzu baadaye akaliita Betheli aliota ndoto na ishara katika ile ndoto MUNGU alimwonyesha kwamba chini ya ardhi ile kulikuwa na madhabahu

➡Sasa eneo ulilolala je linamilikiwa na nani ama kuna madhabahu ya nani chini ya ardhi. Mara nyingi sana watu wanapoota hawafuatilii hizo ndoto kujua maana yake nini lakini mara nyingi unataarifiwa kujua kilichopo

2⃣Omba TOBA kwa MUNGU kwa ajili ya maeneo yafuatayo:

*2Nyk 7:14*

_14 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, *nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.*_

➡Haisemi na kuwaponya wao, wataomba TOBA wao lakini MUNGU ataiponya nchi, hazungumzii juu ya Taifa bali ni ardhi, anazungumzia juu ya kuiponya ardhi inayoombewa. Huwezi kuponya kitu ambacho hakijaugua ama hakiko sawasawa.

➡Kuna aina fulani ya maombi yanaruhusiwa kupita na kuna aina fulani ya maombi hayaruhusiwi mpaka ardhi inayohusika imepokea uponyaji.

➡Unapoomba TOBA lazima uombe kwa IMANI si kwa mazoea, kwa Imani maana yake lazima uwe na mstari wa kusimamia kwenye Biblia na kujua ni kitu gani unachotaka kwenye huo mstari

*Ebr 11:1*

_1 Basi imani ni *kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo*, ni bayana ya mambo yasiyoonekana._

➡Huwezi kuomba kitu kwa IMANI bila kuwa na uhakika na kitu unachokitarajia

*Warumi 10:17*
_17 Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na *kusikia huja kwa neno la Kristo.*_

➡Unapewa mstari usitumie mstari *sikia kilichoko ndani* ya mstari tumia ulichosikia maana wengi sana wanatumia mstari hawatumii wanachosikia kwenye ule mstari halafu wanashangaa kwanini hawapati kilichoko ndani ya mstari sababu MUNGU hajasema IMANI inakuja kwa NENO lililoko pale bali huja kwa kusikia na kusikia huja kwa NENO  la KRISTO.

➡NENO lina sauti ndani yake ile sauti inapoachiliwa inakuachilia kitu kinaitwa ufahamu, kwa IMANI twafahamu, inaachilia kitu kinaitwa uhakika sababu IMANI ni uhakika, imani huachilia picha ndani yako katika ulimwengu wa roho kwa jinsi ya kawaida usingeona

➡Kuna TOBA za aina nyingi ndani ya Biblia na zina kazi yake tofauti tofauti kwa mfano kuna TOBA ya kuingia kwenye UFALME WA MUNGU na kuna TOBA ya kukaribisha UFALME WA MUNGU mahali ulipo

➡Watu wengi ukiwaambia tubu wanaanza kujihesabia haki kwa sababu wao wana aina moja tu ya TOBA, unatubu kama *fire escape* ili usiende motoni kwa hiyo wao wana aina moja tu ya TOBA, kukwepa jehanamu lakini ni kwa sababu hawajajua uwanja mwingine wa TOBA

*Mathayo 4:17*
_17 Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, *Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.*_

➡Hakusema tubuni kwa maana safari ya kwenda mbinguni imekaribia kwa hiyo huwezi simamia huu mstari kwa ajili ya kwenda mbinguni unasimamia huu mstari kwa ajili ya ufalme wa Mungu  kuja mahali ulipo

➡TOBA inakupa maandalizi ya ndani, badilisha mtazamo wako na kuwa tayari kuupokea mfumo mpya unaokuja

➡Lakini pia kuna TOBA ya kukuingiza kwenye UFALME WA MUNGU, kuna TOBA ya kuombana msamaha ninyi kwa ninyi.

➡Hapa tunazungumzia si watu walioko juu ya ardhi bali shida ya watu walioko juu ya ardhi wanazopata kutoka kwenye ardhi na MUNGU anadai TOBA ya hao watu itakayomfanya aponye ardhi yao ili apate kuwasikia zaidi ya kiwango walichokuwa wanaomba aponye ardhi yao ili maisha yao yabadilike, aponye ardhi yao ili waweze kufuga bila shida, aponye ardhi yao ili ardhi iwaruhusu kumalizia nyumba zao na kujenga lakini lazima ardhi ipokee uponyaji na huu uponyaji MUNGU anadai uje kwa TOBA

➡Kwa hiyo unapoingia kwenye TOBA ndani yake angalau kuna vitu 3 unapaswa kukumbuka

*MOJA*
Omba toba kwa ajili ya kuvunja au kutofuata masharti ya MUNGU yanayohusu ardhi hii

➡MUNGU anapokupa eneo la kukaa lina masharti na katika mazingira ya Agano jipya watu hawajajua namna ya kuunganisha kati ya Agano la kale na jipya. Mfano kuna ardhi imewekewa zuio isiuzwe, MUNGU anaweka masharti katika eneo unalokaa haruhusu madhabahu ya miungu mingine, sasa usijaribu kuweka madhabahu za miungu mingine gharama yake ni kubwa sana. Na ROHO MTAKATIFU anakuwepo mahali hapo kukusadia na kuelewa masharti ya MUNGU

➡Si watu wengi wanaelewa kwamba wanaweza kukorofisha masharti na ukakwama, maana hakuna eneo lisilokusudiwa kitu, maana yake usinunue kiwanja bila *kuwauliza watu wa mpango miji kuna nini wamepanga kwenye eneo hilo*

*MBILI*
Unaweza kuomba TOBA kwa kuchanganya MUNGU na miungu
Wakristo wengi wana shida ya kuchanga MUNGU na miungu mahali wanapoishi na mahali wanapofanyia biashara na kazi, leo wanasali kanisani kesho wameenda kwa waganga

➡MUNGU ni MUNGU mwenye wivu anataka heshima yake peke yake ukimchanganya namna hiyo ananyamaza kwa sababu hawezi kupokea utukufu na mapepo, kwa manana haitajulikana nani kafanya kwa hiyo anaamua kunyamaza na kuweka pingamizi kwamba huwezi kufanikiwa kwa stahili hiyo kama hujafanya TOBA hutafanikiwa

*TATU*
Kuomba kilichosababisha shetani akapata nafasi ya kumiliki eneo hilo na kuweka masharti yake haijalishi wewe umehusika au amehusika mwingine

3⃣Omba MUNGU aondoe zuio, sababu ukiwa ni adhabu kutoka kwa MUNGU
Popote ulipokwama omba MUNGU akuondolee zuio yaani pale ulipozuiliwa

*Malaki 1:3-4*

_3 bali Esau nimemchukia na kuifanya *milima yake kuwa ukiwa, na urithi wake nimewapa mbweha wa nyikani*. 4 Ijapokuwa Edomu asema, Tumepondwa-pondwa, lakini tutarudi na kupajenga *mahali palipoachwa hali ya ukiwa;* Bwana wa majeshi asema hivi, Wao watajenga, bali mimi nitaangusha; na watu watawaita, Mpaka wa uovu, na, Watu ambao Bwana anawaghadhabikia milele._

➡Si shetani anaangusha bali MUNGU anaangusha ndiyo maana anasema ondoa zuio ukishatubu mwambie MUNGU aondoe zuio

4⃣Kemea viondoke vyote vilivyokaa kwenye eneo la ardhi hiyo unayoiombea iliyoshindikana kuindeleza

*Isaya 13:19-22*
_Na Babeli, huo utukufu wa falme, uzuri wa kiburi cha Wakaldayo, utakuwa kama Sodoma na Gomora hapo *Mungu alipoiangamiza. Hautakaliwa na watu tena kabisa, wala watu hawatakaa ndani yake tangu kizazi hata kizazi. Mwarabu hatapiga hema yake huko, wala wachungaji hawatalaza makundi yao huko*. Lakini huko watalala hayawani wakali wa nyikani; na nyumba zao zitajaa bundi; mbuni watakaa huko; na majini watacheza huko. Na mbwa-mwitu watalia ndani ya ngome zake; na mbweha ndani ya majumba ya anasa; na wakati wake u karibu kufika, na siku zake hazitaongezeka._

➡Kuna vitu ambavyo vinapata nafasi kihalali kabisa kukaa mahali hapo ambavyo vinaweza kukutesa sana kwa hiyo lazima uweke *eviction order*

5⃣Omba madhara yaliyotokea kwenye eneo lile yaishie
Sababu umeomba
✅Toba,
✅zuio likaondoka,
✅umekemea nguvu za giza zilizokuwepo ndani
✅sasa omba uponyaji upite maana kuna madhara yaliyotokea, uzalishaji umepotea MUNGU arudishe tena, madhara kwenye ndoa MUNGU aweze kuiponya ndoa, huduma yako imeharibika MUNGU aweze kurudisha kibali tena, omba uponyaji kwenye kila eneo ufugaji wako na kila madhara yaliyotokea

➡Kama ni mwombaji utajua ya kwamba unahitaji kuomba na kuomba na kuomba na kuomba mpaka ndani yako usikie umevuka kumbuka MUNGU alipokuwa anamtoa Rahabu walilazimika kuzunguka siku 6 sababu kulikuwa na misingi kwenye ardhi ile ambayo ilitakiwa kushughulikiwa kila siku

➡ROHO MTAKATIFU atakusukuma kama unaona ile hali uliyoikuta wakati unaoomba ya kuomboleza ukirudi kwenye lile eneo hali haijaondoka maana yake hujamaliza kazi endelea kuomba mpaka ile hali imeachia maana utaona kuna mabadiliko ndani

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.