Thursday, February 23, 2017
MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017
- Next You are viewing Most Recent Post
- Previous Denice Simeo Youth Development Expert atoa ushauri kwa vijana wa chuo
google+
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.
8⃣ *SEMINA YA NENO LA MUNGU DAR ES SALAAM TANGANYIKA PACKERS*
*MWL MWAKASEGE*
*HALI YA KIROHO YA ARDHI INAVYOHUSIKA KUFUNGWA AU KUFUNGULIWA KWA MAFANIKIO YAKO*
*SIKU YA NANE: 2017 MARCH 12*
LEO IKIWA SIKU YA MWISHO KUNA MISTARI NAKUPA ILI TUOMBE.
Kama hukuwepo hakikisha unapata kanda au CD na vitabu vitakusaidia.
Jambo la maombi leo
*Kufuta maneno yaliyopo kwenye ardhi yanayokwamisha mafanikio yako*
2Wakorintho 3:12-18
_Basi, kwa kuwa mna taraja la namna hii, twatumia ujasiri mwingi; nasi si kama Musa alivyotia utaji juu ya uso wake, ili kwamba Waisraeli wasitazame sana mwisho wa ile iliyokuwa ikibatilika; ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi, *wakati lisomwapo Agano la Kale, utaji uo huo wakaa; yaani, haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo; ila hata leo, torati ya Musa isomwapo, utaji huikalia mioyo yao. Lakini wakati wo wote watakapomgeukia Bwana, ule utaji huondolewa.* Basi “Bwana” ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru. Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho._
Nilikuwa namuuliza Mungu maswali na alikuwa ananipa majibu kwa agano la kale.. na kila nikiomba alikuwa ananirudisha kwenye agano la kale na kila nikisoma nilikuwa sielewi na niliomba Mungu anipe kuona na Bwana alinisaidia.
Ukisoma biblia utaona Musa alikuwa anafunika utaji ili kupunguza utukufu aliokuwa nao ili wanaIsrael waweze kumuona maana alikuwa anang'aa sana kutokana na ule utukufu aliokuwa nao.
Uwepo wa Mungu ulikuwa unamfanya Musa kuweza kuwa na utukufu sana, na ili waweze kumuona alikuwa anajifunika na utaji ili kupunguza utukufu.
Ukitaka kusoma agano la kale soma kwa jicho la agano jipya na ukisoma kwa mtazamo wa agano la kale ule utaji (kutokuona kilichoko ndani) unakukulia kwa hiyo lazima utazame kutoka kwa Kristo.
Usisome biblia kwa kuigawa, biblia ni kitabu cha agano. Japo kuna maagano mengi sana kwenye biblia na ujio wa agano jipya halikuja kufuta maagano ya agano la kale maana katika agano jipya ni mambo halisi. Na ndio maana Yesu alisema
_Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. *Mathayo 5 : 17*_
Lazima utazame kwa sura ya msalaba lasivyo utaacha baadhi ya mambo na utakwama.
Damu ya Yesu inafuta makosa hado yaliyofanyika katika agano lilopita.. ndio maana nasema agano jipya ni bora kuliko agano la kale na damu ya Yesu ni damu ya agano.
*Yeremia 22:29-30*
_29 Ee nchi, nchi, nchi, lisikie neno la Bwana. 30 Bwana asema hivi, *Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda.*_
Hapa nchi ni ardhi yenye mipaka halali ya kiumiliki.(2 Nyakati 7:14)
Angalia mstari 18 _Basi, Bwana asema hivi, katika habari ya Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda; Hawatamwombolezea, wakisema, Aa! Ndugu yangu; au, Aa! Dada yangu; wala hawatamlilia, wakisema, Aa! Bwana wangu; au, Aa! Utukufu wake._*Yeremia 22 :18*
_21 Mimi nalisema nawe wakati wa *kufanikiwa kwako*; lakini ulisema, Sitaki kusikia. Hii ndiyo iliyokuwa desturi yako tangu ujana wako, kutokuitii sauti yangu._ *Yeremia 22 :21*
Huyu mtu alikataaa kusikia sauti ya Bwana na aliiambia ardhi iandike.
👉Alikuwa hana watoto
👉Hatafanikiwa siku zake zote.Hata atakapokuja kuzaa.
Maneno hayo yaliandikwa kwenye ardhi na Mungu aliisemesha ardhi
_28 Nikutanishieni wazee wote wa kabila zenu, na maakida yenu, ili niseme maneno haya masikioni mwao, *na kuwashuhudizia mbingu na nchi juu yao.*_ *Kumbukumbu la Torati 31 :28*
(Kuna vitu nataka kuweka kama kumbu kumbu kwenye mbingu na ardhi)
kwa nini alisema👇👇
_29 Kwa sababu najua baada ya kufa kwangu mtajiharibu kabisa, na kukengeuka katika njia niliyowaamuru; nayo mabaya yatawapata siku za mwisho, kwa vile mtakavyofanya maovu machoni pa Bwana kumtia kasirani kwa kazi ya mikono yenu. 30 Musa akasema maneno ya wimbo huu masikioni mwa kusanyiko la wana wa Israeli hata yakaisha._*Kumbukumbu la Torati 31 :29-30*
_1 Sikilizeni, enyi mbingu, nami nitanena; Na nchi isikie maneno ya kinywa changu._
*Kumbukumbu la Torati 32 :1*
Biblia inasema wameitwa wazee na maakida ili wasikie maneno yatakayokaa kwenye ardhi kama shahidi
_63 Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima._*Yohana 6 :63*
Maneno ni roho yanabeba na uzima na maneno ya mauti yanakuwa ni roho ya mauti.
Maneno yakikaa kwenye ardhi kudumu kwake inategemea na roho iliyoambatana na roho iliyoko nyuma yake.
Maneno ya Mungu ya uzima ndani yake
_15 Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule. *16 Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake*. 17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari._*Ufunuo wa Yohana 12 :15-17*
👉Mungu aliweka ardhi ili imsaidie mtu kwa ajili ya kufanikiwa ardhi ni mpiganaji mzuri sana maana ardhi iko vizuri sana kwenye vita na mtu akitumia vita kwenye ardhi inakuwa ni kali sana.
Ardhi iko pale kwa ajili ya kukusaidia
Mwanamke kama ndani yake kabeba neno la Bwana na shetani anawinda ili anyakue na Mungu anataka akusaidie na ardhi iko pale nayo kukusaidia..
*Mathayo 26:28*
_kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, *imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.*_
Cheki damu ilivyoandikwa ndivyo inavyotumika.
👉Kumwaga.. na unapomwaga inaondoa na kila kitu kilichoambatana na hicho kitu.
Kunyunyiza.. damu ya kunyunyiza nayo ina kazi yake tafuta kwenye biblia utaona
Ntamwaga damu ya Yesu mahali hapa na popote na unapomwaga damu ya Yesu ni lazima kusimama nayo kwa imani.
Unaweza msaidia mtu hata kama ana dhambi na hataki kwenda mbinguni na Mungu anaingia kati. *Na unasimama nayo kama kuhani*
Unamiliki juu ya ardhi kwa hali ya Kikuhani au Kifalme.. na unatumia kinywa chako.
👉 Na jua wakati naomba nasema Mungu nasimama kama kuhani hata kama una dhambi.. Mungu anaingilia kati
Haruni alikuwa anaenda na chetezo kwa sehemu ambapo kwenye tauni na Mungu alikuwa anaachilia uponyaji sio kwamba wametubu hapana bali kwa sababu kuhani kaomba.
Na Ezekiel 22:30 _Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu._
👉 kusimama mahali palipoboma.. na unasimama kama kuhani na kuomba na unachukua damu ya Yesu maana ipo kwenye madhababu unaimwaga kwenye ardhi unapotaka uponyaji utokee
Na nikisema hivyo.. damu ya Yesu ina uhai inakuja hapo
Na pana geuka kuwa pekundu.. tena peupe.. tena ..unaona uhai..kwenye miguu ya mtu aliyekanyaga hapo inabadilika
Mara ya kwanza niliona hiki kitu nakuambia,Nilikiwa Iringa nilimwaga damu ya Yesu. Na ghafla mtu aliyekuwa amekaa kwenye kiti alinyanyua mtoto akamuweka pale na yeye alikimbia ili kutoka nje ya hema maana alikuwa anaona moto unawaka kwenye miguu.
Pia kuna mtu alikuwa hali ya maombi ilikuwa mbaya. Nilimwambia kuwa kata kiraka kama vile Mungu alivyomwambia Musa na aliachilia damu ya Yesu na ile hali ya maombi ikarudi.
Tulikuwa mkoa mmoja na kulikuwa na watu wamekaa kwenye miti na wengine wanakuwa na magari.. na nilianza kuachilia mahali popote pale damu ya Yesu maana niligundua nikiachilia ndani ya hema wengine huwa wanakimbilia nje sasa nikaanza kumwaga maeneo yote
Na kesho yake baada ya maombi tulikuta mti umeanguka na unafuka moshi. Baada ya maombi ule mti haukuweza kusimama tena japo ulikuwa na majani mabichi lakini damu ya Yesu iliutetekeza. Kwa nje unaona mti wa kawaida kumbe ni madhabahu.
Mungu alishighulika nayo na mahali Mungu kainuliwa madhabu zingine lazima zianguke.kumbuka wafilist walipochukua sanduku la agano na kuipeleka kwenye miungu yao.. miungu yako ilianguka chini.
Damu ya Yesu ni damu ya agano inaangusha madhababu za miungu mingine, itumie na utavuka pakubwa sana
Yuko Mungu ambaye ata kukusaidia..
*Maombi..*
👉 Kufuta maneno kwenye ardhi yaliyonenwa kwenye ardhi ya yanatesa watu.
👉 Kama maneno yalinenwa kama ni neno la Mungu basi uwe na uhakika Mungu atalithibitisha neno lake. Na kama lilinenwa na kambi nyingine basi ujue shetani atakaa hapo nae kuthibisha neno lake.
👉Tulikuwa mkoa mmoja na wakati wa maombi nikamwaga damu ya Yesu katika viwanja vile. Sasa alikuwepo dada mmoja pale alikuwa kavunjika mguu wake na alikuwa na POP. baada ya maombi pale na kumwaga damu ya Yesu. Mapepo yalilipuka na yule dada wakambeba na aliacha fimbo yake na mimi nikambandika mikono.
Alipozinduka akashangaa mguu wake umekuwa mwepesi. Wahudumu wakamuuliza je unaweza kutembea akasema naomba fimbo.. yangu maana alikuwa anatembea na fimbo. Sasa aliopoona mguu wake umekuwa mwepesi akajaribu kusimama na kutembea ghafla alianza kuruka ruka..
Baada ya hapo yalifanyika maombi makubwa sana sana na baraka za Mungu ziliachiliwa pale..
KUJUA SEMINA INAYOFUATA BONYEZA MAANDISHI HAYA.
👇👇👇
http://www.mwakasege.org/ratiba017.htm
*2-9 APRIL 2017 NI DODOMA MJINI*
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.