DAY 4. FAHAMU YAFUATAYO KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI UFANIKIWE- Mwl. Mwakasege | Apostle Darmacy Blog MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 | Apostle Darmacy Blog

APOSTLE DAMAS

Breaking News

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Thursday, February 23, 2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 

 

Goo

 

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 
About Muses Radio Player...
Version 2.1 (html5)

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.
-->

Tangaza nasi

Breaking News
Loading...

Soma App

Soma App
DOWNLOAD Somaapp NOW!

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Wednesday, April 5, 2017

DAY 4. FAHAMU YAFUATAYO KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI UFANIKIWE- Mwl. Mwakasege

4⃣  *SEMINA YA NENO LA MUNGU DODOMA UWANJA WA BARAFU NA MWL MWAKASEGE*

SOMO: *YAFAHAMU YAFUATAYO KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI UFANIKIWE KIMAISHA*

*SIKU YA 4*

*TAR 5 APRIL 2017*

LENGO: _kuhakikisha uhusiano wako na Mungu unaimarishwa ,pia tuendelee kumtegemea yeye katika mafanikio_

Jambo 1,2 na 3 (tumeyaona kwenye masomi ya siku zilizopita Leo tuendelee na Jambo LA NNE)

*JAMBO 4*
Imarisha IMANI yako inayohusu kutumia Damu ya Yesu ili ikusaidie kushughulikia Ndoto zilizobeba vitu vinavyokwamisha maisha yako

⏩Tofauti katika kuombea Ndoto ni ile imani uliyonayo kwenye Kutumia Damu ya Yesu

⏩Ndoto pia huwa zina vipindi vyake, unapoota ndoto angalia muda uliyoota ndoto hiyo na cheki  huwa unaota muda gani. *Kuna vipindi 4 vya muda - SAA 1-3, SAA 4-6, SAA 7-9 na SAA 10-12*
check ndoto zako unaota ktk kipindi gani

_Waebrania 11:1, Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana._

_Warumi 10:17 Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo_.

⏩Imani chanzo chake ni kusikia sio Neno. Ni lazima usikie kwanza .Unaweza kusikia ila usisikie na unaweza kusikia na usielewe

_Yakobo 2:20,26 Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba *imani pasipo matendo haizai?* Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na *imani pasipo matendo imekufa*._

Unaweza kuwa na Imani na isikusaidie kitu

⏩Wakristo wengi wana Imani ya Damu ya Yesu ila wengi hawana Imani katika kuitumia hiyo Damu ya Yesu.

🚶🚶‍♀ *HATUA ZITAKAZOWEZA KUIMARISHA IMANI YAKO*

*HATUA 1*
_Uwe na Mistari ya Neno la Mungu katika Biblia juu ya Damu ya Yesu_

Kutoka12:12-13, 21-23
_Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA. *Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri*.  Hapo ndipo Musa akawaita wazee wa Israeli, na kuwaambia, Nendeni, mkajitwalie wana-kondoo kama jamaa zenu zilivyo mkamchinje pasaka. Nanyi twaeni tawi la hisopu, mkalichovye katika ile *damu iliyo bakulini na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli;* tena mtu ye yote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi. Kwa kuwa BWANA atapita ili awapige hao Wamisri; na *hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu*, na katika ile miimo miwili, BWANA atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi._

KUT. 12:12‭-‬13‭, ‬21‭-‬23

1 kor 5:7
_Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana *Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo*;_

Unapotumia na mstari katika Agano la kale uwe na unaofafana nao katika agano jipya. Tafuta mstari utakaokupa uhalali wa kuitumia katika MAOMBI yako.

*HATUA 2*
Tafakari hayo maneno👆🏼 hadi uone ile Waebrania 11:1 na Yakobo 2:20  itokee moyoni mwako (imani na matendo)

⏩Mistari ya HATUA ya kwanza ina mambo yatarajiwayo. Mungu aliwaambia wana Wa Israel watapona tu kwa sababu ya Damu ikiwepo juu ya miimo ya milango yao, nao waliyasikia hayo na kupata uhakika wa kuwa yaliyosemwa yatatokea

Yakobo 2:20
Imani pasipo matendo haizai

⏩Suala la kuweka kwenye matendo ni la muhimu sana katika utumiaji wa Damu ya Yesu. Musa nae aliweka kwenye matendo kwa kutii ndio maana hawakuangamizwa ( Kutoka 12:21-23)👆

*HATUA YA 3*
Wana wa Israel kushiriki kwa matendo kuitumia Damu ya Pasaka ili Mungu aweze kuitumia kama wao walivyoitumia.

*Kumbuka:* Mungu haitumii Damu ya Yesu ambayo wewe huitumii ni lazima kwanza uikubali kuitumia ndipo naye ataitumia kama waisrael walivyofanya huko Misri

⏩Mungu anatazama Damu uliyoitumia kwanza kwani inaonyesha Imani yako ipoje

⏩Mungu hutafuta Damu iliyofanyika Ishara ili yeye naye aone Imani yako

⏩Mfano : kuna tofauti ya  kupanda bus na kujifunza kuendesha bus, hii itakusaidia hata dereva akishindwa kuendesha wewe unaweza kuendesha.

Hiyo pia ipo ktk utumishi wetu kuna watu wanajua kuombewa tu ila kujiombea hawawezi.

*Mfano mwingine ni pale unaponunua simu itategemea unataka kuijua kwa kiwango gani, kama unataka kujua kupiga na kupokea uwezo wako utaishia hapohapo. Hivyo kama una kiu ya kutaka kujua zaidi utajifunza zaidi ili kupanua uelewa wako*

⏩Vivyo hivyo kama Damu ya Yesu unaitumia kwa ajili ya kwenda mbinguni tu au kujifunika tu, itaishia kufanya kazi hiyohiyo unayoiamuru, ila kumbuka Damu ya Yesu inatumika popote unapoihitaji alimradi uwe na imani katika kuitumia.
Kumbuka Damu ya Yesu unaweza
👉 kuimwaga,
👉inanyunyuziwa
👉pia unaweza kunywa hivyo usikariri kazi moja tu,

⏩Kama hulitumii Jina au Damu ya Yesu jua nae Mungu hatalitumia kwako.

NB:
Kuna walioota wakifanya mapenzi kwenye ndoto, wengine wakifunga ndoa ktk ndoto au unakuta upo kwenye ndoa ila unaota unafanya mapenzi na mke/ mumeo hizo ndoto sio nzuri.

Kwani unakuwa tayari umeingia katika Agano la kwanza katika ulimwengu wa roho. Ndio maana unakuta binti au kijana wanachelewa kupata wenzi kwani wanakuwa tayari wameshaingia Agano ktk ulimwengu wa Roho. Au ndoa INA mafarakano au zinavunjika kwa ajili ya hayo maagano. Hapo inabidi uitumie Damu ya Yesu ili uvunje hilo Agano la kwanza

*MAOMBI*
⏩. Kama umeota hayo👆🏼 shika kitovu chako alafu ingia kwenye:
👇
*1.* Toba, rehema na utakaso.

Tubu popote ulipoacha mlango hadi hiyo roho ya uzinifu ikaingia kwako, pia Toba kwa ajili ya UOVU wa wazazi wetu vizazi vya nyuma

*2.* Ondoa Agano la kwanza kwa kutumia Damu ya Yesu

*3.* Jitenge na huyo uliezini nae ktk ndoto na uliefunga nae ndoto , jitenge na Pete, mavazi, zawadi,nk. kwa Damu ya Yesu

*4.*Pia tulifanya MAOMBI ya kujiweka WAKFU kwa Bwana
- Wakfu Nafsi,mwili na roho
- Uongozwe na Bwana ktk mambo yako

- Usonge mbele kimwili na kiroho

- Utumie mapenzi ya Mungu katika maisha yako na sio akili yako.

🙏🙏Ubarikiwe sana!!!
Noted by
_Glory_
_Dodoma._

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.