Thursday, February 23, 2017
MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017
- Next You are viewing Most Recent Post
- Previous Denice Simeo Youth Development Expert atoa ushauri kwa vijana wa chuo
google+
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.
5⃣ *SEMINA YA NENO LA MUNGU DODOMA UWANJA WA BARAFU NA MWL MWAKASEGE*
SOMO *FAHAMU YAFUATAYO KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI UFANIKIWE KIMAISHA*
*TAR MARCH 6, 2017*
*DAY 5*
Lengo ni kuimarisha uhusiano na Mungu ili umtegemee na kumtumini ili yakisaidie.
Baada ya semina Mungu akusaidie kukupa maarifa ya ndoto na uelewe.
Jambo la 5.Vijue vyanzo vya ndoto ili ujue kuviombea ipasavyo.
Ni rahisi kufuatilia na kuombea ndoto ambayo unajua chanzo chake.
1.Chanzo cha kwanza ni Mungu.
Usingizi mzito
2.Shetani..
Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda BWANA, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. Tembeeni kwa kumfuata BWANA, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.
KUM. 13:1-4 SUV
http://bible.com/164/deu.13.1-4.SUV
Haijalishi ndoto ina mbwembwe kiasi gani au ishara kiasi gani kuna zingine sio za Mungu. Hivyo kuwa makini sana.
3.Shughuli nyingi.
*Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi*; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno.
MHU. 5:3 SUV
http://bible.com/164/ecc.5.3.SUV
-ndoto zingine huja kwa sababu ya shughuli nyingi.
4.Hali ya Kiroho ya mahali ulipolala.
_Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani. Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale. *Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake. Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako. Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa. Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia. Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli BWANA yupo mahali hapa, wala mimi sikujua. Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni.* Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake. Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu._
MWA. 28:10-19 SUV
http://bible.com/164/gen.28.10-19.SUV
👉 lile eneo lilikuwa ni madhabahu ya Mungu hapo mahali alipolala yakobo.
👉jua hivi vyanzo maana itakupa mtaji wa kuomba na tutapita kwenye mifano hapa ili kuomba.
MFANO.
ndoto kutoka kwa Mungu angalia Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao,
AYU. 33:14-16 SUV
http://bible.com/164/job.33.14-16.SUV
Omba Mungu akupe neema ya kusikia sio kupuuzia lakini kuna kitu kipo anataka upate. Omba Mungu akupe hiyo neema maana hataki upoteze muda.
Na omba Mungu akupe.. neema ya kujua.. kufungua masikio lengo Mungu afungue masikio yako maana mchana unaweza ukawa busy..
Omba Mungu akusaidie kusikia kilichoko ndani ya ndoto ili afungue masikio yako ya ndani. Angalia 16. Muhuri Mafundisho yao. Kama umepata Mafundisho na hujui kuwa ni ya Mungu atakuja kwenye ndoto kuthibisha au kubatilisha kwa ndoto.
Mfano kuna mtu alikuwa kaokoka na anenda mahali kupata neno la Mungu. Na alienda mahali hapo mara kwa mara na mwishoni akaamua kuhamia. Na usiku aliota ndoto Mchungaji wa mahali hapo anawaongoza kwenda porini na wakapotea njia. Na yeye alikuwa anaowaona.
Na alipoamka . Alikuja nisikia nikifundisha na akajua kuwa kuwa Mungu amkataza.
Na angali 17 .. alikuwa anamtoa kwenye makusudi yake.
Na usipuuzie ndoto na Mungu alinisukuma kulifuatilia somo la ndoto lea sababu Mungu alisema nami kwa ndoto.
Siku nataka kuacha kazi kabla ya wakati maana wito uliwaka ndani sana.. na hali hii unaweza dhaniwengine wanatania.. na elia alisema nimenaki peke yangu Mungu alimwambia kuwa wapo watu 700 Kwa hiyo usiwaze kuwa wewe tu ndio mtenda kazi.
Basi niliona watu ng'ambo wako kwenye senyenge na kuna mto na mimi niko upande mmoja. Akaja mtu mweusi ananiambia ruka ruka. Nikasema ngoja nitafute pa kupitia.
Ghafla nikaona mwamba nikasema si uneona nikapata kupitia. Na nilipoamka Roho mtakatifu akiniambia kuwa hiyo pressure ya kuacha kazi sio yangu. Tukia hadi upate pakukanyaga.
Hivyo inahitaji utulivu.
Mfano 2.
Mwanzo 41. Farao alipoota ndoto za njaa na ndoto zile haikuwa kwa taarifa bali alikiwa na maelezo ya kipindi cha maandalizi ya kuweka akiba.
Na angepuuzia ina maana dunia nzima na yeye mwenyewe angepata hasara.. na ndio maana Mungu aliweka ishara.
Maisha ya Yesu alipokuwa mdogo yamefuatiliwa na ndoto. Yusufu alipotaka kukuacha Mariam na Mungu alisema nae kwa ndoto ili asimuache. Wakati nawaza namna ya kumuacha Malaika akaongea nae. Na Yusufu alikubali.. maana haikuwa rahisi kuamino kuwa mimba ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
Quote. Herode.. na mamajusi na jinsi Mungu alivyongea nao..
Na ilipita muda herode alijua kadangangwa.
Quote. Ndoto ya kwenda misri.. tena ndoto ya kurudi misri.
Search akisha kuonywq kwenye ndoto litimie neno la kuitwa mnanazayo.
Kama angepuuzia ingukwa hasara sana.. hivyo ndoto itakusaidia kupata utulivu ndani.
Mungu alisema nami mengi sana.
Nilikuwa eneo la kijinini eneo la migomba na kuna mtu alinipeleka pale. Na mchungaji wa pale kila akihubiri wanakufa. Na akatoka na mimi niliingia na hap kanisa lote watu wamekufa na yule mtu kanipa nguo nyeupe na mimi nikaanza kufundisha watu wakaamka wote na mara 3 kwa theluthi.
Na nikaamka.
1.Nilijuq wito wangu ni kwa ajili ya kanisa na kuwqkwqmua mahali walipokwama.. ndio maana utaona. Mafundisho ya kukuwqmua.
Mfano wa ndoto Kutola lwa shetani.
Ziba lango la ndoto ili lisipitishe mambo ya shetani maana za shetani ndoto zake zinakuharibu Kutoka 12:21-23. Nanyi twaeni tawi la hisopu, mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu ye yote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi. Kwa kuwa BWANA atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, BWANA atapita juu ya mlango, *wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi.*
KUT. 12:22-23 SUV
http://bible.com/164/exo.12.22-23.SUV
Waliziba kwa damu ule mlango ndio maana aliwaambia waweke damu katika vizingiti vya mioomo ya malango.
Muhimu. Damu itamila kuziba mlango na omba. Kwa damu ya Yesu Kristo nafunga mlango shetani asipitishe ndoto zake. Omba mara kwa mara.
Mungu hatumii damu iliyopo kwenye bakuli ambayo haitumiki. Weka neno kwenye matendo kwa upande wako na yeye anafanya kwa upande wake.
Ombea na wototo wake na semea neno eneo la ndoto. Ombea watu na ombea sana watoto ili shetani asipitishe vitu vyake. Na kuanza kupitisha ombea sana hili jambo.
Yule dada anazini na mtu kwenye ndoto na alikuwa anaomba na nilipoomba kwa damu ya Yesu zile ndoto zilikatika.
Na endelea kusoma ili imani yako ijenge na kristo ni pasaka wetu na inaziba.. hii ni siri sana..
3.Ndoto zinazokuja kwq sababu ya shuguli nyingi
Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake; naye alipokuwa akizipanda, nyingine zilianguka karibu na njia, zikakanyagwa, ndege wa angani wakazila. Nyingine zikaanguka penye mwamba; zilipoanza kumea zikakauka kwa kukosa rutuba. Nyingine zikaanguka kati ya miiba, na miiba ikamea pamoja nazo ikazisonga. Na zilizoanguka penye miiba ni wale waliosikia, na katika kuenenda kwao husongwa na shughuli na mali, na anasa za maisha haya, wasiivishe lo lote.
LK. 8:5-7, 14 SUV
http://bible.com/164/luk.8.5-14.SUV
Shughuli nyingi maana yake kutumia muda bila kufuata mapenzi ya Mungu. Yesu alisema sifanyi neno ila lile baba analofanya.. search kuiimiza kazi yake.
Haya sio kwa ajili ya Yesu tu bali hata wewe.. (tangu sasa hatumtabui mtu kwa ajili ya mwili...kwa ajili yake yeye.. tumesulubiwa pamoja na Kristo.. Yesu alisema mimi ni mzabibu nanyi ni matawi) search.
Matunda anayotaka.. matunda yape kukaaa.. matunda yake yanayotokana na mbegu maana Mungu ndiye akuzaae. Na anakuja kuona kama kila mwaka kama kuna mtu ana matunda na kama huzai Mungu anasema ukate.
Mungu hatazami maisha bali anaangalia matunda kila siku .wiki mwezi.. Mungu antaangalia.. search matendo yao yabawtabgulia..
Mungu anakusidia na anangalia na kuwa je unafanya.. na kuna watu wapendwa kwenye miba.. omba Mungu maisha yako yasikae kwenye miimba.. miimba imekuja kwa ajili ya adhabu.. jifuze kitembea katika toba..
Omba toba.. mahali ukifika.. Mungu akusamehe.. fanya hilo.. kila wakati.
Aliyoko kwenye miimba haivishi kitu na maana kuna mahangaiko huko.. kasome kwenye biblia. Maana yake kuna watu hawataki wakuzungike na akasemw kaa nao mbalo lakini wewe unawang'ang'ania..
Kama marafiki hawakusaidiii kaa nao mbali fika ng'ambo nyingine fika mbali.. *watakuwa miimba search)
Huwa nawaambia wanafunzi usikae na watu ambao hawasomi.. na wengine wanasema hela ya baba ipo kama hujui alipataje.. maana ulirithi tosha ni kukuambia kuwa alipate huo utajiri.. au mali.. maana mali ni fikra.
Ikawa katika kuenenda kwao aliingia katika kijiji kimoja; mwanamke mmoja jina lake Martha akamkaribisha nyumbani kwake. Naye alikuwa na umbu lake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake. Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie anisaidie. Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi; lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa.
LK. 10:38-42 SUV
http://bible.com/164/luk.10.38-42.SUV
👉Maneno magumu sana.. na fikiria unachaharika kumtumika Yesu na anasema unapoteza muda.. na niliomba Mungu anisaidia nisitumike kwa hasara..
👉Unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya utumishi mwingi.. na unapomtumika Mungu una utulivu kiasi gani.. na usihangaike.. na usifutahie unavyomaliza kilomita.. je unakimbia kwenye utumishi wa kwako.
👉Unajua kwanini Yesu hakuenda kumponya Lazaro, lakini yeye aliona baba yake aliona kuwa anamfufua.. japo alipelekewa taarifa.. kwa emergence..lakini hakwenda.
👉Yohana 17 Yesu anasema kazi uliyonipa nimemaliza.. na mbona dodoma hajafika.. alifanya alichotumiww kufanya.. na lengo kubwa sio kuponya magonjwa bali ni kufa msalabani.
Mungu anatafuta vipaumbele na huna muda wa kufanya kila kitu. Na hakuna mwalimu atake fundisha kila kitu..
Na mungu hawezi kukupa kufundisha kila kitu. Sasa wewe umefundisha hesabu unataka kufundisha physics.. na wewe ndio utanata uonekane.. na utajimini wewe mwenyewe...
Na anasema fundisha na hili na hili huwa nasema nasubiri Mwalimu mkuu ndiye anipangie kipindi...
Na nikisema namwaga zege.. najua kabisa shetani hawezi bomoa.. kazi ya mtu itapimwa.. na jenge akisema itakuaje.
Yesu akija wakati tunajenga hema anatafuta nini, na kati kati ya semina anangalia nini.. au baada ya semina..
Na jion na asubuh omba Mungu akuongoze hatua kwa hatua.. na usifurahie njia bali hatua ambazo Mungu atakupeleka..
Na mbinguni utaenda na utumishi sahau
Omba Mungu akusaidie...
Ndoto kwa shuguli nyingi zitakuonesha na watu uliokwama nao na Mungu anasema kaa nao mbali.. na omba kwa Mungu usilale kwenye adhabu.. omba toba na Mungu analisamehe tu..
Hamna sababu ya kulala kwenye adhabu walayi damu ya Yesu ipo.. na shughuli nyingi zinakusaidia..
Anasa za dunia hii ni vile vitu vinakuvuta na sio vya Mubgu kwako.. enenda sawa sawa na wenye haki.
Mtu yeyete aliyoko kwenye utumishi na kijana aliyoa mtu na vitu visivyo vyake..
Kuna mahali ukiona utashtuka.. na utanishangaa mimi na mwakasege yuko hapa.. na kwa sababu ya nafasi niliyonayo.
Omba kwa Mungu vipaumbele vya kwako.. na vipaumbele na mke wangu nae ananfasi yake na kuombeana na na huyu abebe hiki na huyu abebe hiki.
4.Mazingira ya kiroho.
Mambo 4 muhimu
1.Ombea chumba unacholala.. funika kwa damu ya Yesu. Kama ni hotel omba toba kwa kila kilichofanyika nje ya mapenzi ya Mungu.
Nguo zinabeba roho ombea kwa damu ya Yesu.
Nilikiwa nchi moja na nilifika kwenye hotel na alikuwa anatufuatilia kila hotel tunayolala.na alikuwa analal baada ya sisi kutoka
Na akawa anasema nawahi upako, nikalala nalia usiku kucha.. na yeye atalia..
Ombea nyumba nzima.. na ombea ardhi unayolala..na kama kuna madhabahu nyingine na ombea hili jambo mara kwa mara.
Mtu mmoja alipita kwenye Ardhi anasikia vitu vinagonga chini...
Na aliomba Mungu naomba ardhi kama imebeba kitu kicho cha kwako.. na akasema naomba itapike kila kitu hapo na akatoka nyoka.
Ombea mbingu iliyoko juu maana ina sauti ya kiroho.. na Yesu alipotoka juu ya maji na mbingu zilifunika zina siri ya ajabu sana.. mbingu zinatatandaza utukufu wa Bwana.
€Ombea watu wanaoingia mahali hapo.. Tamari alipobakwa alienda mahali kwa kaka yake.. na ukiwa wa tamari ulishika kaka yake ulileta hasira ya kuua. unaua hali ya kiroho.. omba Kama Ayubu.. aliwaombea watoto wake.
Kama ni mgeni omba kwa ajili yake na vichujwe.. na ombea hili jambo.
Kama uombea nyumba yako.. hiyo hamu inaisha hata kama anavuta sigara.. na omba sana hivi vitu.
Ni vitu vya kawaisa kabisa.. na anakuja mtu kuwatembelea nyumbani na mnaanza kuota ndoto ngumu ngumu.
Walikuja watu kuniona na mtoto wakasema kuna vitu vinaruka.. na wakasema kuna vitu vinaruka na kumpiga mtoto. Na walisema mama mkwe akuja nyumbani, na alikuja na mambo yake.
Na niliwaambia kuwa either mumuwekee kikao au mwombee rehema.. na usione aibu. Mweleze ukweli.
Mtoto katoka shule kafundishwa hadi kwenda kuzimu.. na anataka kugeuza chumba chao kuwa kama lango la kuzimu. Na ujue hamtalala salama.
Funika macho yako tuombe
.. _-wimbo wa nisalama rohoni--
There is greatness inside of you
I believe that there is a seed of greatness in all human beings. Therefore the aim of my blog is to bring to my readers awareness of things that are happening around us. I will focus majorly on inspirational news that can motivate my readers to doing more with their lives too. If you are too busy to get acquainted with what is in the newspapers or you have read the papers but have not felt any inspiration or motivation, please log on this page and be inspired to walk in your purpose and dream.