DAY 8: SEMINA YA NENO LA MUNGU DODOMA- MWL. MWAKASEGE | Apostle Darmacy Blog MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 | Apostle Darmacy Blog

APOSTLE DAMAS

Breaking News

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Thursday, February 23, 2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017 

 

Goo

 

Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 
About Muses Radio Player...
Version 2.1 (html5)

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.
-->

Tangaza nasi

Breaking News
Loading...

Soma App

Soma App
DOWNLOAD Somaapp NOW!

Gospel Awards

Gospel Awards
GOSPO AWARDS ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, radio na tv kwa mwaka 2016 kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

RSA TANZANIA

RSA TANZANIA
RSA ni kifupi cha maneno ROAD SAFETY AMBASSADORS ikiwa na maana Mabalozi wa Usalama Barabarani.

Radio Sayuni

ASAS Dairies LTD

Soma BIBILIA

Soma BIBILIA

Sunday, April 9, 2017

DAY 8: SEMINA YA NENO LA MUNGU DODOMA- MWL. MWAKASEGE

SEMINA YA NENO LA MUNGU DODOMA UWANJA WA BARAFU NA MWL MWAKASEGE*
SOMO: *FAHAMU YAFUATAYO KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI UFANIKIWE KIMAISHA*

*APRIL 9, 2017*
*SIKU YA 8*
DOWNLOAD KITABU CHA HONGERA KWA KUOKA https://drive.google.com/…/0BxdP6mgDJWByVERtampLTGZWR…/view…
SALA YA TOBA http://www.mwakasege.org/mafundisho/okoka.htm
Lengo: Kuimarisha uhusiano wako na Mungu ili ufanikiwe kimaisha.
Ndoto ni njia ambayo Mungu anatumia kuongea na mtu, na kwa wakati ule wetu ilikuwa shida sana kupata masomo haya ya ndoto. Kwa hiyo hii ni neema kusikia masomo haya kwa wakati huu. Tafsiri za ndoto zipo kwenye biblia kwa hiyo fuatilia hatua kwa hatua.
*Na nilikuambia tunaandika kitabu cha Ndoto na tunaomba Mungu atusaidie kitoke mwaka huu.*
*Summary*
_Kwa kuwa Mungu husema, wakati huu kwa njia moja, au wakati mwingine kwa njia nyingine, ingawa mwanadamu anaweza asielewe. Mungu husema na mwanadamu katika ndoto, katika maono ya usiku, wakati usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu wasinziapo vitandani mwao,Ayubu 33:14‭-‬15 NEN_
👉Ndoto ni njia ambayo Mungu anatumia ili uweze kusikia kitu ambacho Mungu anataka kukuambia
_Ikawa, mwisho wa miaka miwili mizima, Farao akaota ndoto; na tazama, amesimama kando ya mto. Na tazama, ng’ombe saba wazuri, wanono, walipanda kutoka mtoni, wakajilisha manyasini. Na tazama, ng’ombe saba wengine wakapanda nyuma yao kutoka mtoni, wabaya, wamekonda, wakasimama karibu na wale ng’ombe wengine ukingoni mwa mto. Kisha hao ng’ombe wabaya waliokonda wakawala wale ng’ombe saba wazuri, wanono. Basi Farao akaamka. Akalala, akaota ndoto mara ya pili. Tazama, masuke saba yalimea katika bua moja, makubwa, mema. Na tazama, masuke saba membamba, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao. Kisha hayo masuke membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. *Basi Farao akaamka, kumbe! Ni ndoto tu*.MWANZO. 41:1‭-‬7 SUV_
👉Farao aliposema kumbe ni ndoto tu ina maana alikuwa anataka kudharau. Na naamini wewe sasa hutaweza kudharau ndoto .
Na ndoto zina vyanzo mbali mbali japo Mungu anaweza tafsiri ndoto zote.
1. Mungu
2.Shetani
3 Shuguli nyingi unapokosa vipaumbele vya kutumia muda vizuri unakuwa na shughuli nyingi maana yake hazina mpangilio
4.Hali ya Kiroho ya mahali unapolala.
Mungu ndiye aliyetengeneza lango la ndoto na kwa kuwa hatujui namna ya kulinda shetani nae analitumia. Na nilikufundisha kuwa linalindwa kwa kwa damu ya Yesu. Ndio inatumika kuziba lango la ndoto
Kama hukuwepo hakikisha unapata kanda na sikiliza itakusaidia sana.
Jana nilipitia baadhi ya ndoto na nyingi sana ni ndoto za shule. Na jana nilikupa mtaji wa kuanzia kufanya maombi
*UMUHIMU WA KUFANYA MAOMBI YA KUONDOA KINACHO KUFUATILIA KWA NJIA YA A NDOTO TOKA KWENYE ENEO UNALOLALA AU ULILOWAHI KULALA*
1⃣ *SEHEMU YA KWANZA*
*.Kutoka eneo unalola*.
Nyumbani kwako, hotelini, kazi, nyumba ulipanga
_Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani. Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale. *Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake. Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako*. Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa. Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia._
_*Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli BWANA yupo mahali hapa, wala mimi sikujua. Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni*.MWANZO. 28:10‭-‬17 SUV_
Yakobo alipolala na aliota ndoto na kazi ya ile ndoto ilikuwa na kazi kubwa ya kumtaarifu juu ya mahali alipolala.
Na Mungu alikuwa anajitambulisha kwake na ndio maana yako alisema hapa ni nyumba ya Mungu. Ina maana mahali pale palikuwa uwepo wa Mungu.
Jambo lingine ni lango ina maana kuna vitu vya kiroho vinapita pale kutoka katika ulimwengu wa roho kuja ulimwengu wa mwili.
Tulikuwa mkoa mmoja na tulikuwa tunajenga hema, na kuna watu walikuja na wakasema hapa mnapojenga hema mnakata network zetu. Na walisema tutaona nikasema haisha shida. Na tulijua kabisa ni wachawi.
Baada ya siku 2 mchawi wa kwanza aliokoka na wakaenda kutafuta mchawi mwingine mkubwa maana na wao wana ngazi zao.
Jumamosi alikuja kupambana na sisi. Alijaribu kila kitu na alishindwa na akarudi nyumbani kwake na anakaandika bango lake na kuwa mganga wa kienyeji.
Na alikuwa na uwezo wa kujigeuza umbo lolote na anaingia chumbani kwake na anafungua hata Ardhi. Na alishangaa aliporudi nyumbani kwake alijaribu kila kitu alishindwa.
Na ilibaki moja na alikuwa na kadi ya ATM, na alikuwa anatumia kila mahali maana alipewa kuzimu. Na alipewa masharti kuwa hela atakayochukua lazima aitumie yote . Sasa jumapili alipoenda benki kutoa hela kadi yake ilimezwa.
Na aliona sasa kapatikana alinyoosha moja kwa moja uwanjani aliwakuta wenzangu na alijitambulisha kuwa anaenda kijisalimisha kuwa anataka kuokoka. Na wakamhoji maswali na walienda nae nyumbani kwake.
Na walienda nae nyumbani kwake, na gari zinapiga nyimbo za injili na walishangaa kuona mganga anakuja na nyimbo za injili maana pale kwake walikuwepo watu waliokuwa wanahitaji wake na magari yao.
Na bango la mganga walilitoa na kila kitu chake wakaondoa kila kitu wakachoma uwanjani. Na tukaomba nae na alipokuwa kwenye madhababu wenzake walishindwa kuingia ndani.
Na hii iwasaidie wahudumu na alikuwa haoni mtu na alikuwa anaona miali ya moto. _Na kwa habari za malaika asema, Afanyaye malaika zake kuwa pepo, Na watumishi *wake kuwa miali ya moto*.Waebrania 1:7_
Na hata mapepo yanakuwa hayaoni watu yataona moto tu. Hata wachawi walipokuwa wanatafuta kuingia walishindwa. Kwa hiyo biblia inaposema kuwa hili ni lango ina maana ni eneo maalumu la kuingilia.
Kwa hiyo hadi sasa huyu ni mtumishi wa Mungu na mchungaji sasa. Sasa turudi kwa Yakobo, chukulia huyu Yakobo angekutana na miungu mingine ingekuaje?
Sasa twende kwa mtoto Samuel na nafuatilia kwenye maandiko na sijaelewa bado kwanini aliwekwa karibu na sanduku la agano. Maandiko yanasema alipompeleka hekaluni na Kuhani Eli alimpeleka karibu na Sanduku la agano sasa kama unalala karibu na sanduku la agano utalala kweli? Biblia inasema kuwa akaanza kusikia sauti, maana kuna watu huwa usiku wakilala wanasikia sauti. Sasa ile sauti ilikuwa ni ya Mungu.
Sasa fikiria unaenda kulala hotel na unalala sehemu mtu kasahau hirizi yake hapo na wewe unakuja speed kuwa na hujaombea hapo. Sasa lazima utaota ndoto ngumu ngumu ivi.
_Na Babeli, huo utukufu wa falme, uzuri wa kiburi cha Wakaldayo, utakuwa kama Sodoma na Gomora hapo Mungu alipoiangamiza. Hautakaliwa na watu tena kabisa, wala watu hawatakaa ndani yake tangu kizazi hata kizazi. Mwarabu hatapiga hema yake huko, wala wachungaji hawatalaza makundi yao huko. Lakini huko watalala hayawani wakali wa nyikani; na nyumba zao zitajaa bundi; mbuni watakaa huko; na majini watacheza huko. Na mbwa-mwitu watalia ndani ya ngome zake; na mbweha ndani ya majumba ya anasa; na wakati wake u karibu kufika, na siku zake hazitaongezeka.ISAYA. 13:19‭-‬22 SUV_
👉Hii ni adhabu iliyotolewa katika mji wa Babeli na Mungu Mungu aliweka zuio na aliweka na wanyama wakali na majini yacheze ndani yake na mbwa mwitu walie huko ndani.
👉hujawaji jiuliza kwanini mtu anaota ndani kwake kuna nyoka au jogoo au myama yoyote? Na ukiamka ni unasema ni ndoto tu na Mungu anakuambia kuwa hapa kuna shida.
Kuna mtu aliota mbwa kalala kwenye kitanda chake. Na majini yapo pale kisheria na huwezi nyamazisha maana wapo pale kihalali na ukitaka kuwatoa pale lazima uwe na *eviction order* ya mahakama ya mbinguni. Kwa hiyo lazima utumie neno la Mungu kisheria.
Na nilikuambia kuwa kila picha unayoota ina maana yake. Ukiona nyoka kuna maana yake ukiona mbuni kuna maana yake.
Kuna mtu alikuwa anaombea nyumba yake na kila akilala alikuwa anaona nyoka kweye ndoto na akimka anawakuta kweli mara mlangoni na akiamka anakutana na nyoka kweli. Na aliua zaidi ya nyoka 30 na wote wana rangi ya kufanana. Nenda kwenye biblia kuna mifano na mifano.
Kuna wakati wana wa Israel walitolewa Samaria.
_Naye mfalme wa Ashuru akaleta watu kutoka Babeli, na Kutha, na Ava, na Hamathi, na Sefarvaimu, akawaweka katika miji ya Samaria badala ya wana wa Israeli; wakaumiliki Samaria, wakakaa katika miji yake. Basi ikawa, wakati ule walipoanza kukaa huko, hawakumcha BWANA; kwa hiyo BWANA akapeleka simba kati yao, nao wakawaua baadhi yao. Kwa hiyo wakamwambia mfalme wa Ashuru, wakasema, Wale wa mataifa uliowahamisha, na kuwaweka katika miji ya Samaria, hawaijui kawaida ya Mungu wa nchi; kwa hiyo amepeleka simba kati yao, na tazama, wanawaua, kwa sababu hawaijui kawaida ya Mungu wa nchi. Ndipo mfalme wa Ashuru akatoa amri, akasema, Mpelekeni mmojawapo wa makuhani, mliowachukua kutoka huko; aende akakae huko, akawafundishe kawaida ya Mungu wa nchi. Basi mmoja wa makuhani waliochukuliwa kutoka Samaria akaenda akakaa katika Betheli, akawafundisha jinsi ilivyowapasa kumcha BWANA. Lakini pamoja na hayo watu wa kila taifa wakajifanyia miungu yao wenyewe, wakaiweka katika nyumba za mahali pa juu, walipopafanya Wasamaria, kila taifa katika miji yao walimokaa.2 WAFALME. 17:24‭-‬29_
Baada ya kuraruliwa na simba walisema kwa sababu hatujui kawaida ya Mungu wa eneo hili. Ndio maana kuna wengine wanaota wanakimbizwa na nyoka au mbwa au wanyama wakali hivi.
Cha kufanya ni ombea kwanza mahali pako pa kulala na Mungu anakuambia kuwa mungu wa eneo hili ana alama hii. Na kama wewe ni mpangaji na hujafuatilia uwe na uhakika kuwa utaondolewa hilo eneo kama ni kwako patakukinai na uwe na uhakika kuwa utahama.
*MAMBO YA KUFANYA KAMA UMEKUTANA NA HALI YA NAMNA HIYO*.
🛐1.Omba toba kama kuna kitu kiko mahali hapo na hakimpendezi Mungu. Omba toba . Na nilikufundisha namna ya kuzia ndoto mbaya kuwa ombea
👉Nyumba unayolala
👉Ombea mbingu
👉Au mtu huyo a aingia kwako.
👉Secure chumba cha kwako. Ombea hicho tu.
👉Ombea ardhi ya hapo.
👉Zuia kwa damu ya Yesu ndoto mbaya
Kama uko hotel ombea mahali pako tu usianzishe ugomvi bila sababu.
Siku moja tulikuwa Calfonia kwenye mkutano wa uchumi. Na sisi tuliwahi siku nne kabla. Sasa tulifika eneo la hollywood nadhani mnajua. Sasa unaweza kuelewa Mhubiri anaingia holly wood.
Na kama hujawahi muona shetani akitembea nenda pale. Na tukamuuliza Mungu tunafanyeje hapa. *Mungu alituambia jifunike kwa damu yangu.*
Si unajua hata Yesu alikwepa vita, na sisi tulijiombea wenyewe. Sasa kama hujui namna ya kufanya mazingira ya namna hiyo unaweza kwama.
Mahali popote pale watu hawakai au nyumba au chumba ina maana kuna ukiwa na ukiwa ni adhabu. Unasafiri muda mrefu hata kama ni kwako jifunze kuomba maana unaweza kutana na vitu vigumu.
🛐 *2.Mwaga damu ya Yesu kwenye eneo unalokaa au unalolala*
Damu ikimwagika huwa inaondoa kila kilichoko hapo.fanya zoez nyumbani kwako. Na kuna kijana mmoja alisikia hili somo na yeye akaenda akamwaga damu ya Yesu nyumbani kwake na aliweza kuomba maana mara ya kwanza alikuwa hawezi.
Mwingine alikuwa anashindwa kulala lakini baada ya kumwaga damu ya Yesu eneo lake aliwaza kulala vizuri.
*3.Hakikisha unakemea nguvu za giza zilizoko mahali pale*
Kama watu wamelala hapo na wamefanya uasherati na eneo hilo hilo, juzi nilikuambia sabuni haiondoi nguvu za giza. Na unashangaa unalala hapo na mapepo yanaanza kukusumbua.
Kwa hiyo ombea na mashuka kwa damu ya Yesu maana damu ya Yesu hua
safisha kabisa.
*4 Ombea uwepo wa Roho Mtakatifu na malaika zake*
Neno la Mungu linasema _*Malaika wa Bwana hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.Zaburi 34:7*_
Kwa hiyo malaika wanaweza kukufanyia ulinzi.
*SEHEMU YA PILI*
*ENEO ULILOWAHI KULALA NA UKAONDOKA KATIKA HIMAYA YA MAPEPO*
_Biblia inasema Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni *juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho*.Waefeso 6:12_
👉Hiyo ni hirach yao sasa jeshi la pepo wabaya wana vikosi vyao. Na nilishangaa siku moja niliona makundi Tofauti Tofauti ya malaika. Na wanakuwa miili Tofauti wale wa kuligana na kazi iliyopo. Wale wapiganaji hawana mabawa ila wanakuwa na Farasi weupe. Na wengine wana maumbo ya kwao. Na wale wanaoimba nao wana sura tofauti. Ni mara chache huwa nawaona , na muda mwingine na wao wanakuja kuimba na sisi.
Ukisoma Mwanzo 28:10-17angalia 28👇
_Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake. Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu. Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae; nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu. Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.MWANZ. 28:18‭-‬22 SUV_
_Na malaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, Yakobo! Nikasema, Mimi hapa. Akasema, Inua, basi, macho yako, ukaone; mabeberu wote wanaopanda wanyama wana milia, na madoadoa, na marakaraka; maana nimeona yote aliyokutendea Labani. Mimi ni Mungu wa Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri. Sasa ondoka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa.MWANZO. 31:11‭-‬13 SUV_
_Mungu akamwambia Yakobo, Ondoka, panda uende Betheli, ukakae huko; ukamfanyie Mungu madhabahu huko; yeye aliyekutokea ulipomkimbia Esau, ndugu yako. Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake, na wote waliokuwa pamoja naye, Ondoeni miungu migeni iliyoko kwenu, mjisafishe mkabadili nguo zenu. Tuondoke, tupande kwenda Betheli, nami nitamfanyia Mungu madhabahu huko; yeye aliyenisikia siku ya shida yangu, akawa pamoja nami katika njia yote niliyoiendea.MWANZO. 35:1‭-‬3 SUV_
Sasa kwanini Mungu alitaka kumkubusha kuwa Mungu wa Betheli. Na kila mahali nilienda na wewe na malaika wangu. Sasa fikiria Yakobo angekutana na mapepo?
Mungu anataka kuingia kwenye agano. Mara nyingi huwa nawaambia watu kuwa kama unaota ndoto unakula na watu waliokufa kwenye ndoto usiowajua au unakula nyama ambayo sio kawaida kula. Maana yake ni kuwa unaingizwa kwenye agano na mapepo yako pale
Kama Malaika alimfuata Yakobo kwa Labani na alimkumbusha kurudi Betheli. Na kama ulikutana na mapepo yaani ulilala shule na hapakuwa pazuri kuna mapepo yataanza kukufuatilia. Kuna mapepo yanaitwa Demon monitors na kila mahali yanakufuatilia. Miaka na miaka na unaota ndoto uko shule. Sasa kumbuka kukata kitu cha kiroho ulicho kutana nacho mahali hapo maana itakutesa.
Jifunze namna ya kujikung'uta maana unaweza ukaokota kitu hotelini na inaanza kuhamia kwako. Cheki unamtembelea mwenzio na unakuta ugomvi wa nyumbani kwa rafiki yako na unahamia kwako na unaanza kufanana fanana na kule.
Kwa hiyo hakikisha unakata hiyo connection kwa damu ya Yesu. Jikung'ute kila mahali ulipotoka hata kama mtu amekuja kukutembelea kwa kwako hakikisha unaomba na kung'uta kila kitu anachokuja nacho.
Hujawahi ona umeota ndoto katika mazingira mbali mbali na uko sehemu tofauti tofauti. Mara uko Morogoro na Dar es Salaam au Dodoma. Hiyo ni Mungu anataka kukumbia kuwa kata hiyo connection.
Ninaona mtu aliachiwa alama mkononi kwenye ndoto na nyoka ulipolala. Na kuna pepo lipo linakufatilia na kila ukienda mahali popote una tembea nalo. (Mwl alifanya maombi ya mtu huyo na kukata hiyo network.) Na pepo lilipuka na kumtoka huyo mtu.
Hili lilikuwa ni zoezi ili kuthibitisha kitu alichokuwa anafundisha. Kwa hiyo jifunze namna ya kuomba toba. Na sasa nakata connection ya hilo pepo na baada ya maombi mtu alifunguliwa.
Tunakwenda sawa sawa.?
WEKA MKONO WAKO JUU YA MAGOTI NA MAHALI ULIPOLALA NA ARDHI INAKUMBUKA.
NA NAOMBEA ENEO LOLOTE AMBALO UNALALA NA UKIWAHI KULALA NA NAACHILIA DAMU YA YESU.
KAMA KUNA KITU NYUMBANI KWAKO CHA KAMBI NYINGINE KAKITOE MAANA NAMWAGA DAMU YA YESU SASA HIVI KWA KILA ANAYEFUATILIA SOMO HILI
MAOMBI NA BARAKA.
Pia kama hujampokea Yesu hakikisha unaokoka na kumpata Yesu. Soma kitabu pale juu cha hongera kwa kuokoka.
Pia tembelea www.mwakasege.org na angalia eneo la chini utaona alama ya Facebook like pale na utakuwa unapa masomo kwa njia ya Facebook.
Pia somo hili la ndoto linaendelea Facebook kwenye ukurasa wa Christopher & Diana Mwakasege (Mana Ministry)
Ubarikiwe sana sana na tuonane tena semina ijayo
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

 

NURU MINISTRY

PURE MISSION

PURE MISSION
MAPINDUZI YA FIKRA

Apostle Damasy

Apostle Damasy

Emare Arts Collection - E.A.C

Emare Arts Collection - E.A.C
Sw: Karibuni kwa ununuzi wa picha za kitamaduni ili kukuza Sanaa ya nyumbani, kupitia 0625 927 752 au 0758 576 065, Bei ni nzuri, Asanteni! ******* Eng: Welcome for purchasing different Africultural Arts, as to boost the market of African cultural products via the numbers 0652 927 752 or 0758 576 065. The prices are affordable, Thank you!

ABC Studio Mwanza

ABC Studio Mwanza
Photograph,Video shooting & all Printing works +255756143999, +255658720091, We are located at New Post Office Pamba Road & Nyerere Road, Mza Tz www.facebook.com/abcmwanza,www.youtube.com/abcstudiomwanza
apostledarmasy. Powered by Blogger.