SEMINA YA NENO LA MUNGU DODOMA UWANJA WA BARAFU NA MWL MWAKASEGE*
SOMO: *FAHAMU YAFUATAYO KUHUSU NDOTO UNAZOOTA ILI UFANIKIWE KIMAISHA*
*APRIL 8, 2017*
*SIKU YA 7*
Jana tulianza kuangalia jambo la sita. Na endelea kufuatilia somo hili
kwenye ukurasa wa Facebook. Christopher &Diana Mwakasege (Mana
ministry).
https://web.facebook.com/Christopher-Diana-MwakasegeMana-M…/
Pia tuombee tutayarishe kitabu cha Ndoto kibiblia. Na kikiwa tayari tutawapa.
Summary.
*YAJUE MAENEO MUHIMU YATAKAYOKUSAIDIA KUTAFSIRI/KUFASIRI NDOTO*
1.Uwe na kiu ya kutaka Mungu akusaidie kujua tafsiri ya ndoto hiyo.
Mwanzo 40:8 Mwenye kufasiri ndoto ni Mungu. Hata Daniel alisema hivyo.
2.uwe na neno la biblia la kutosha moyoni mwako ili uweze kusikia ujumbe uliomo katika ndoto.
Warumi 10:17 Kusikia huja kwa neno la Kristo na Wakolosai 3 inasema
neno la Kristo na likae kwa wingi moyoni mwako kwa hekima yote.
3.Omba Mungu akupe ufahamu wa kudumu juu ndoto.
Daniel alikuwa na ufahamu wa mambo yote. Na wewe omba. Ombeni nanyi mtapewa.
4.Kumbuka ukichokuwa unawaza/kuombea kabla ya kuota ndoto.
Waefeso 3:20 Mungu anajibu mawazo yako.
5.Ikiwa umeota ndoto na umesahau omba Mungu akukumbushe.
Daniel 2:1-29. Daniel aliomba Mungu na akamkumbusha ndoto ya Nebukadreza.
*LEO TUNAENDA NDANI KUANGALIA ZILE NDOTO AMBAZO WATU WAKO SHULE AU CHUO*
👉Hata kama hujawahi kuota daka sana hili somo. Na utapa maarifa ya kumsaidia mtu mwingine
_Mfalme akamwambia Ashpenazi, mkuu wa matowashi wake, awalete baadhi ya
wana wa Israeli, wa uzao wa kifalme, na wa uzao wa kiungwana; vijana
wasio na mawaa, wazuri wa uso, wajuzi wa hekima, werevu kwa sababu ya
maarifa yao, wenye kufahamu elimu, watakaoweza kusimama katika jumba la
mfalme; tena alimwambia awafundishe elimu ya Wakaldayo, na lugha yao.
Huyo mfalme akawaagizia posho ya chakula cha mfalme, na ya divai
aliyokunywa, akaagiza walishwe hivyo muda wa miaka mitatu; ili kwamba
hatimaye wasimame mbele ya mfalme.DANIEL. 1:3-5_
👉Iko siri ya ajabu sana kwa watu wanaoota wako shule au chuo katika habari hii ya Daniel
*1.Ukiota uko shuleni au chuoni maana yake ni*
👉Hatua iliyoko mbele yako inahitaji maandalizi ya fikra zako yanahitaji utaratibu maalumu
_tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu
ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;
Yaangalieni yaliyo mbele ya macho yenu. Mtu akijitumainia mwenyewe ya
kuwa ni mtu wa Kristo, na afikiri hivi pia nafsini mwake, ya kwamba kama
yeye alivyo mtu wa Kristo, vivyo hivyo na sisi_.
2 KOR. 10:5, 7
*Maana aonavyo nafsini mwake*, ndivyo alivyo. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.
MITHALI. 23:7 SUV
kwa maana yeye ni aina ya mtu *ambaye kila mara anafikiri juu*ya
gharama. Anakuambia, “Kula na kunywa,” lakini moyo wake hauko pamoja
nawe.
Mithali 23:7 NEN
CHUO ni sehemu ya maandilizi na huwa
unaandaliwa kifikra. Na maandalizi ya watu kifikra upo kwenye mfumo wa
elimu. Na biblia inasema Fikiri.
Katika kiingereza
For as
*he thinks in his heart, so is he.* As one who reckons, he says to you,
eat and drink, yet his heart is not with you [but is grudging the
cost].
Proverbs 23:7 AMPC
*for he is like one who is inwardly calculating*. "Eat and drink!" he says to you, but his heart is not with you.
Proverbs 23:7 ESV
*For as he thinketh in his heart, so is he*: Eat and drink, saith he to thee; but his heart is not with thee.
Proverbs 23:7 KJV
*For as he thinks within himself, so is he*. “Eat and drink”, he says to you, but his heart is not with you.
Proverbs 23:7 TLV
👉Alivyo
kimtazamo ndivyo alivyo, ulivyo ni matokeo ya misimamo yako ya kifikra
uliyonayo. *Maisha yako hayabadilishwi na cheti, bali ni misimamo yako
kifikra.*
Kuna mfumo rasmi huu unaitwa mfumo wa Elimu na biblia
inaita elimu ya ufalme wa Mungu. Na shetani anataka kupinga na kuweka
wa kwake.
Lakini haina maana ya watu wasiosoma na wana maisha
mazuri maana kuna watu wemeishia darasa la saba lakini wana maisha
mazuri kuliko watu wa degree 3. *Maana maisha sio cheti ni fikra*.
Mungu anaongea na wewe kukuambia kuwaa kuna hatau iko mbele.. na akili
ziko kwenye nafsi yako. Katika nafsi kuna nia, maamuzi na akili.
Ayubu 33:14-15 Mungu husema na mtu kwenye ndoto na hajali na 16.
Anafungua masikio yake 17 anasema kumuondoa kwenye makusudio yako.
Unakuta mtu anaomba Mungu naomba nisaidie hatua iliyoko mbele yangu na
Mungu anakuletea ndoto ya shule. Ina maana kuna hatua iliyoko mbele yako
inahitaji maandalizi.
Au uko katikati ya maandilizi na Mungu
anakuletea ndoto ya shule na anakumbia hapo uko shule.. akina Daniel
waliwekwa shule miaka 3 kwa ajili ya maandalizi. Sasa ingekuwa ni kosa
kwao kutafuta kazi baada ya mwaka mmoja. Na kama wangekuwa wanaomba
Mungu awape kazi uwe na uhakika angewaletea ndoto ya kuwa wako shule au
chuo.
👉Ina
maana kuna hatua iliyoko mbele mbele yao. Na hii inawapata sana hawa
watumishi ambao moto wa kumtumikia Mungu unawaka sana ndani yao. Na
Mungu wakiwa katika hali ya namna hiyo Mungu anawaletea ndoto ya kuwa
wako chuo. Hapo inamaanisha kuwa ni sehemu ya maandalizi. Kaa hapo
vumilia hapo ulipo maana saa yako bado.
👉Pia
Mungu anasema na wewe kuwa maandalizi ya hatua inayokuja huwezi
kujiandaa ipasavyo peke yako. Na ina maana huwezi jisomea peke yako na
nenda shule ili uandaliwe.
*2.Kama unaota na chuo au shule uliyosoma zamani maana yake nini.*
👉
Ina maana ya kwamba kuna jambo fulani ulitakiwa kuvuka hapo kifikra
lakini hukuweza kuvuka. Na kwa sababu hiyo kuna eneo kwenye maisha yako
limekwama kwa sababu hiyo.
Ndio maana nilikuambia lazima
ujifunze kuhusu ndoto ili uulize na ujifunze zaidi. Kwa hiyo kama
huelewi uliza kwa Mungu na fuatilia kwenye biblia .
*3.Kuota uko Primary(shule ya msingi)*
👉Haijalishi
uko wapi na ume ota uko shule ya msingi. Maana yake fikra za kimsingi
yaani foundation za kufikiri kuna kitu ulikosa kwenye msingi wa
kufikiri.
Sasa unakuta wewe unaomba kwa ajili ya kuingia kwenye ndoa au kupanda cheo lakini unajikuta unaota ndoto uko primary.
👉Mungu
anzungumza na wewe juu ya misingi yako mizuri ya maamuzi na wewe
hujaandaliwa bado/ hauko vizuri. Biblia inazungumza juu ya maamuzi na
inasema *"amani ya Kristo iamue moyoni mwako"*
Ndio maana waalimu
wanaofundisha shule ya msingi na mwalimu akakosea kumuwekea msingi
mwanafunzi wa kupenda shule ataharibu kabisa maisha yake.
Na
sasa watu wengi wanatarajia masomo ya msingi yapelekwe awali lakini si
kila mtoto atapata nafasi ya kwenda awali. Lakini mfumo rasmi unahitaji
uendele darasa la kwanza na ndiko kuna foundation ya kufikiri kwako
maana ndipo inajengwa hapo.
*Waalimu wa darasa la kwanza na la
pili ni muhimu sana maana ndio msingi wamaisha ya wengi. Mwalimu ukipewa
hiyo nafasi chunga sana*.
Mama yangu alikuwa mwalimu na kafundisha miaka yote lakini alifundisha darasa la kwanza na la Pili na alikuwa mwalimu mkuu.
Sasa watu wengi Mungu anawapa ndoto za kuwa wako primary hata kama
wamemaliza chuo kikuu. Na hapo Mungu anasema na wewe kuwa misingi yako
ya kimaamuzi, kihisia au makusidio hayako vizuri. Kwa hiyo unahitaji
kwenda kwa Mungu ili akusaidie ujue hiyo misingi.
*4.Je wale watu ulio nao darasani katika ndoto.*
👉Ina maana kuwa hao ni watu mlio nao ngazi moja ya kimaandalizi.
*5.Ukiota ndoto uko darasani na watu uliowahi kusoma nao zamani*
👉Maana
yake kuna eneo mlikwama kifikra kwa kufanana ina maana kuna maandalizi
unahitaji kufanya. Wewe fanya utafiti utakuta na wewe umekwama hapo.
Kwa hiyo Mungu anasema na wewe kuwa unahitaji kuvuka hapo.
*6.Ukiota hukai darasani na unategea au unatoroka.*
👉Maana yake huna utulivu unaotakiwa kuwa nao ili uweze kujiandaa au kuandaliwa kwa ajili ya hatua inayokuja.
Au unaomba Mungu akupe kujua kwanini umekwama hapo unakuta Mungu
anaongea na wewe kwa njia hii ili kukuonesha kuwa ulikuwa unatega shule
aliyokuwa anakuandaa.
Mtu anayetega darasani anakuwa na maisha
mabovu. Maana kuna baadhi ya chuo usipohudhuria masaa kadhaa
wanakudiaqualify. Maana hamna namna nyingine ya kuweza kuelewa kama
hukai darasani.
Kwa wale waalimu kama mimi wanaelewa maana yake
nini hapa. *Maana nazungumza na wewe lisaa limoja kila siku. Na huwa
natumia masaa 4 au matano au siku 2 au tatu kabla na unasema na
kufundisha lisaa limoja*.
Huwezi fanya maandalizi ya dakika 5
alafu uongee masaa 2. Kwa Mungu muda wa maandalizi ni muhimu sana
kuliko muda wa kufanya kazi. Sasa jaribu tegea shule alafu tafuta
kazi. Ujue huwezi pata. Kwa hiyo tafuta utulivu mbele ya Bwana.
Kuna vitu vinaweza kukuondolea utulivu kama miradi, marafiki, au maisha
haya.. ndio maana kusoma shule ukubwani ni shida. Au ni mazingira nayo
yanakukosesha utulivu.
Nadhani mlisikia msiba wa mama yangu
uliotokea Dar es Salaam. Na tulikuwa familia na nipo katikati ya semina.
Na Mungu alitupa kufanya maamuzi na kujua na gharama yake. Sasa
tulichagua kuendelea na semina na *halikuwa jambo jepesi*. Na kwa mara
ya kwanza ndio nilielewa kwanini mtu *akifiwa huwa anazungukwa na watu*.
Na niliwahi fiwa lakini sikuwahi kukutana hali hiyo.
Na wenzangu
wanaliponiuliza niliwaambia kuwa tutaendelea na semina. Na wadogo zangu
nao wakasema kaka tuko pamoja na tukagawana majukumu na tukatawaanyika
kila mtu eneo lake. Hapo ilikuwa ni masaa 7 tu tokea mama kafariki. Na
jion semina inanisubiri. Sasa wote wameondoka na nimebaki peke yangu ili
kuandaa semina na hicho ndio kilikuwa kipindi kigumu kwangu sana.
Maana ghafla picha ya mama yangu dk za mwisho ilikuja na naona
madaktari wamemzunguka na mmoja akaja kuniambia Mwakasege mama hayupo na
kila nikitazama ile picha yake. Niliona wakiandika death certificate.
Na walisema ngoja tukaweke mwili mortuary na tuliusindikiza.
Na
nilipofungua biblia sikuona maandiko ya biblia nilikuwa naona picha
ya mama yangu, na nilianza kuwaza maamuzi haya kuwa sasa kama sina
utulivu wa ujumbe kutoka kwa Mungu sasa ndio ntaenda kuhubiri kitu gani.
Kwaa mara ya kwanza nilielewa kwanini unazungukwa na watu ukifiwa maana
niliona mara ya kwanza tulikuwa na watu wametuzunguka na uchungu
uliisha pale maana si watu walikuwepo.
*Nikafunga biblia na
nikaanza kuomba kwa kunena kwa lugha, maana kwa mazingira ya namna hiyo
huwezi kuomba kwa kiswahili*. Maana nakumbuka nilipokuwa nazungumza na
wenzangu. Walisema Mwakasege sio swala la kuhubiri bali ni kuwa
utaweza. Na niliwaambia niinulieni watu wa kuniombea. Na baada ya muda
baada ya kuomba nguvu za Mungu zilinishukia na ghafla nikapata utulivu
kama sina msiba vile. *Mkono wa Mungu ulinyamazisha kila kitu.*
Na ujumbe ukaja na nilikaa lisaa lizima na niliandika na nilipokuwa
nimeenda kufundisha nilikuwa nafundisha kama sijafiwaa vile. Hata watu
wengine walikuwa wanasema inawezekana hatujasikia sawa sawa maana
sidhani kama amefiwa.
Nataka kukuambia kuwa kwa *Mungu kuwa
utulivu ni muhimu maana hata Martha na Mariam walikuwa na shida hiyo*.
Yesu alisema huyu aliyetulia ndiye kachagua fungu jema.
*7. Ukiota unasoma na ukaona somo unalosoma*.
👉Maana yake Mungu anasema na wewe juu ya aina na eneo unalohitaji kujiandaa vizuri kifikra.
*8. Ukiota unajindaa kufanya mtihani au unafanya mtihani*.
👉Maana yake unapimwa kiwango chako ulichofikia kimaandalizi. Ulichofikia kimaandalizi kama unaqualify kwenda hatua nyingine.
Hili unaliona pale ambapo akina Daniel walipewa mtihani wa kitaifa. Na
ulitungwa na Nebukadreza na alisaisha mwenyewe. *Na wa nne tu ndio
waliofaulu.*
Kazi ya mtihani sio kupima tu masomo yako bali ni kucheki kama uko tayari kwa kilichoko mbele yako.
*Ndio maana usifurahie tu kufaulu mtihani, bali faulu maisha kwa kutumia masomo*.
_*Biblia haisemi kwenye lugha walipata ngapi, bali biblia inasema hivi
waandaliwe ili waweze kusimama kwenye ikulu ya mfalme, na wanne ndio
walionekana wanafaa kusimama mbele ya mfalme na haisemi ndio waliofaulu
masomo yao*_.
Wakati nilipokuwa nazungumza na watoto wangu
wakiwa primary. Nilizungumza nao sentensi hii na iliwashatua kidogo
nilipowaambia kuwa *si suala la kufaulu mtihani bali ni kufaulu maisha*.
Na kama mkifaulu tu mtihani na mkakwama maisha ina maana sikuwekeza
vizuri kwenye maisha yenu. Kwa hiyo ninacho tafuta ni kufaulu maisha na
mtihani. Na hili suala sio jepesi maana wengi wanataka kufaulu masomo
tu. Na sio kufaulu maisha.
Na utashangaa hufaulu maisha, na
ulikuwa hujiandai kufanya kazi na ulikuwa unajindaa kufaulu mitihani.
*Unafaulu mitahani lakini maisha umekwama*.
👉Na fuatilia na hilo somo ulilooneshwa.
*10.Ukiota unafanya mtihani na umefeli.*
👉Hujafikia kiwango ambacho ulikuwa unatakiwa. Kwa hiyo huaminiki kwenda hatua inayofuata.
*11.ukiota uko shule au chuo na ukioa kitu kinachohusiana na mambo ya kiroho.*
👉Mwingine
anaota yuko darasani na kuna biblia. Na anauona nyoka, mjusi au bibi
yake na aliyekufa au unamuona mchungaji kavalia rasmi.
👉Ukiona
namna hiyo ina maana kuna jambo la kiroho limetokea ukiwa shule na
linakusumbua mpaka sasa. Mungu aliwaambia akina Daniel kuwa chakula na
vinywaji havikuwa vizuri rohoni. Na lazima vyakula vilikuwa vinatolewa
sadaka.
Na walijua kabisa hali ya kiroho ingeweza haribu
maandalizi yao. Hali ya kiroho ilijotokeza mwanzoni kabisa wakati
wanaanza maandalizi ya masomo yao ya miaka 3.
Baada ya miaka 3 walionekana kuwa mara 10 zaid kuliko wachawi wale waliokiwa wame wazunguka.
Huyu ndugu alikuwa na wachawi na alikuwa anawataka kuwaondoa kazini,
aliwatafuta watu wengine na ndio maana alikuwa anataka kuona je wanafiti
kiasi gani.
Maana hamna haja ya kuondoa watu wazuri kazini na
ukaleta watu ambao si bora kuliko hao. Ujue tu utendaji wa kazi
utakwenda chini.
Na kilicho wasababisha kuwa wawe mara kumi bora
ina maana ni kitu cha kiroho kilichokuwa chuoni. Na ilikuwa ni
chakula. Na ndio maana Mungu aliwazuia kula.
*12.Ukiota uko shule au chuo na uko eneo la chakula (dining au cafeteria)*
👉Kama
ni hivyo ombea chakula ulichokula au kitu kilichogusa fikra zako. Maana
utashangaa kuwa ulipokuwa unakula kumbe kuna vitu mlizungumza na
vikapandwa na viliharibu maisha yako.
Kwa hiyo kila ukiomba Mungu akuvushe unaonesha hapo ombea ulichokula shule.
Tulikuwa mkoa mmoja hapa nchini kwenye mkutano kama huu na niliona
katika ulimwengu wa Roho watu wana mavazi marefu na wanafuatilizia
watoto na wanawapa chakula watoto chakula si kizuri. Mungu aliniambia
futa hiyo kitu kwenye damu yao maana kinashika fikra zao.
Na
nilitangaza kufuta kwa damu ya Yesu. Na kulikuwa na mapepo mengi sana
yalilipuka na Mungu alinionesha wazi wazi lakini anaweza sema na wewe
kwa njia ya ndoto.
*13. Ukiota uko shule au chuo na umemaliza course na hupati kazi na ukiomba Mungu upate kazi unaota uko shule*.
👉Maana
yake ni hii kuna shida kati ya kitu ulichosoma na soko la ajira
unalotafuta kazi. Kwa hiyo lazima uombe Mungu aunganishe kati ya
ulichosoma na soko la ajira.
Kuna watu walisoma miaka 3 na akina
Daniel na hawana kazi kwa sababu masomo yao ilikuwa ni kwa ajili ya
kukaa ikulu ya Nebukadreza . Na hawana kazi.
Omba kwa Mungu ili
akusaidie kusoma masomo yatakayohitajika na soko la ajira.usisome masomo
ambayo soko lake linabadilika na unasoma sasa na baada ya miaka 3
imejaa watu. Na unaanza kukemea shetani.
Hamna mfumo wa Elimu
unao fundisha watu saa hiyo hiyo au muda huo huo waingie kazini.
*Ikitokea wanaita crash program au inservice training*.
Lakini kama ni kwa ajili ya miaka 5 utashangaa hata hawahangaiki kupata kazi maana ajira zao zinakuwa tayari (demanded)
Miaka ile tunasoma sisi tulikuwa tunaletewa barua kabisa chuoni hata
kabla ya kumaliza. Na barua ya kwanza ilikuwa ni National Insurance
Corporation. Lakini sikuenda huko. Maanaa nilienda kufanya kazi
nyingine.
Hii ni dondoo kwa uchache.
*MAMBO YA KUFANYA SASA*
🛐1.Omba toba kwa Mungu kama kuna mahali hujufanya vizuri wakati wa maandalizi.
🛐2.Omba Mungu akuvushe .
Na mtu mmoja alidaka na alianza kuomba na alisema Mwalimu
ulipofunsidha nilikuwa naota ndoto niko tu primary na nilianza kuomba na
kuomba na niliomba Mungu aniasidie.
Baada ya muda kadhaa niko chuo na niliendelea kuvuka hatua kwa hatua. Na nilimwambie endelea kuvuka
*USIKUBALI FIKRA ZAKO ZIKWAME OMBA KWA MUNGU*
Mungu atakusaidia kwenda darasani au atakupa Vitabu. Fanya kitu ambacho Mungu atakupa.
Niliona mahali katika shule ya seminary sista yuko form one na watoto wadogo nae anasoma.
Kwa hiyo fuata maelezo Mungu atakayokupa.
Ubarikiwe.
**************************
✨✨ *TANGAZO*
✨✨
Leo siku ya mwisho ya semina ungana nasi kwa njia zifuatazo.
👇👇👇👇
Bwana Yesu Asifiwe. Tunawakaribisha kwenye semina inayoendelea Dodoma
mjini katika uwanja wa barafu. Semina imeanza jana tarehe 2 April
itaendelea hadi jumapili tarehe 9 April.
Redio zinazorusha Semina inayoendelea Dodoma mjini ni;
1. Redio Sauti ya injili -
Moshi, 92.2 FM
Arusha,96.1 FM.
Tanga 102.6FM & 96.7 FM
Same 100.4 FM
Rombo 96.4 FM
Manyara 102.9 FM & 96.1FM
Morogoro 99.1 FM
Mara 96.1 FM
Unguja, Pemba na Mombasa 102.6 FM
Voi - Kenya 96.4 FM
Dodoma 102.9 FM
Pwani, Rufiji, Kiluvya, Tegeta, Ubungo, Manzese, Mbezi, na Ruaha 99.9 FM
Daraja la Mkapa (Lindi) 99.9 FM
2. Redio HHC Alive
Mwanza, Mara, Simiyu, Geita, Kagera, Shinyanga, - 91.7 FM.
3. Redio CG FM
Kigoma, Simiyu, Shinyanga, Tabora na Katavi 89.5 FM
4. Redio Baraka
Iringa, Njombe, Mbeya, Rukwa 107.6 FM
5. Radio Rungwe
Rukwa, Malawi,Mbeya na Njombe102.5 FM
6. Radio Info
Mtwara 92.1 FM
7. Redio Uzima
Dodoma 94.0 FM
8. Redio Bunda FM
Mwanza, Mara, Simiyu na Kagera 92.1 FM
9. Redio Mpanda FM
Katavi, Rukwa na Kigoma 97.0 FM
Unaweza kusikiliza live kupitia
www.kicheko.com na
www.mwakasege.org, unaweza kusikiliza na kuangalia live kupitia
www.ustream.tv/chanel/mwakasegemanaministry na
www.youtube.com (jina la chanel ni Christopher Mwakasege)
https://youtu.be/Ul6ONaN6Mtc
Mungu Awabariki!
https://m.facebook.com/story.php…
Noted by
*felixmbwanji@gmail.com*
*Arusha, Tanzania*
🙏🙏🙏🙏7⃣ *SEMINA YA NENO LA MUNGU DODOMA UWANJA WA BARAFU NA MWL MWAKASEGE*