MAKOSA AMBAYO YANAWEZA KUFANYA MMILIKI WA BUS KUFUNGIWA KUTOA HUDUMA
Mmiliki wa bus la abiria au mwendeshaji wa huduma hiyo, anaweza kufungiwa kutoa huduma na m
amlaka iwapo atashindwa kuzingatia mojawapo kati ya haya yafuatayo:
1. Kutozingatia kanuni za kiusalama za abiria, kama vile
(a) Kutofanya matengenezo ya mara kwa mara ya magari yake kiasi cha
kufanya magari hayo kuwa hatari kwa usalama wa abiria au kuharibika
haribika hovyo njiani;
(b) Gari kutokidhi viwango vya kuwepo barabarani, yaani roadworthiness
(c) Kujenga bodi juu ya chesisi ya lori
(d) Endapo fremu ya chesisi, ekseli,springi, na rim zimeungwa ungwa kwa welding
(e) Ujenzi wa bodi kutozingatia viwango vya TBS
(f) Uchakavu wa gari, mfano Sakafu ya gari kuwa yenye utelezi, na
iliyochubuka na yenye isiyolinda abiria dhidi ya vumbi, unyevu, hewa
chafu, shoti za umeme, na kelele.
(g) Gari kujaza mafuta au kufanya matengenezo huku likiwa na abiria
(h) Kuhatarisha usalama wa abiria kwa kuacha mlango wazi wakati gari linatembea au wakati wa kuondoka
2. Kutowasimamia vema kondakta na dereva kuzingatia kanuni za usalama
na ubora wa huduma pamoja na masharti mengine ya usafirishaji.
3.
Kutozingatia ubora wa huduma kwa abiria, mfano abiria kutopata huduma
kulingana na fedha waliyoilipia; kutozingatia usafi, kutotoa huduma kwa
abiria baada ya bus kuharibika au kutekeleza abiria
4. Gari kutokuwa na bima
5. Kutozingatia masharti ya leseni ya usafirishaji ambayo ni
(a) Kuhakikisha wafanyakazi wake wakiwa kazini hawafanyi mambo yafuatayo yaliyokatazwa:
(i) matumizi ya lugha mbovu na za uhasama;
(ii) kuzuia au kufanyia fujo magari mengine;
(iii) kuendesha kwa mwendo kasi Zaidi ya ule uliowekwa kisheria na kufanya mashindano ya kugombania abiria;
(iv) kukatisha ruti kabla ya kufika mwisho wa safari
(v) kuendesha wakiwa wamelewa
(vi) kuendesha kwa hatari na kwa kupuuzia hatari au kinyume cha sheria ya usalama barabarani
(vii) kuwakatili abiria
(viii) kuwazuia au kuwakatili wanafunzi;
(ix) kuendesha huku wakitumia simu;
(x) kupakia wanyama na vitu vya hatari kwenye gari.
(b) Kuzingatia ruti na ratiba (kif.19(1))
(c) Kuripoti kwa mamlaka ikiwa gari lake halitatoa huduma kwa siku
thelathini na Zaidi au kama halitaweza kufanya safari kwa masaa 24
yajayo
(d) Kutoa usafiri kwa abiria kulingana na masharti na vigezo
vilivyopo kwenye tiketi, ratiba na kutoa usafiri mbadala wa hadhi ile
ile inapotokea gari husika limeharibika.
(e) Kuondoa gari barabarani
mara moja baada ya kuharibika, na pia kufanya marekebisho ya gari ndani
ya masaa mawili tangu lilipoharibika.
(f) Ikiwa gari halitatengemaa
ndani ya masaa mawili basi mmiliki atatakiwa kuwatafutia abiria usafiri
mbadala au kuwarudishia nauli kamili. [kif.22(1)na(2)]
(g) Kutochaji mzigo usiozidi kilo 20 [kif.23(1)]
(h) Kutoa tiketi
6. Kutorekebisha makosa au mapungufu mbalimbali yanatojitokeza katika
uendeshaji wa biashara yake hata baada ya kuwa ameshaarifiwa au kuonywa
na SUMATRA.
NB: Mambo yaliyoanishwa hapo juu yatafanya mmiliki
afungiwe kutoa huduma iwapo tu yamejitokeza mara kwa mara au hata kama
ni mara moja yamekuwa katika kiwango ambacho hakikubaliki au kuvumilika
kuruhusu kampuni au gari husika kuendelea kusafirisha abiria, mathalani
pale ambapo gari litakutwa halina mikanda, tairi zote kipara, halina
bima na sehemu ambazo hazitakiwi kufanyiwa welding zimefanyiwa welding.
Hapa mamlaka inaweza kusimamisha huduma husika mara moja ili gari husika
lifanyiwe marekebisho.
Kwa ufupi hizo ndizo sababu zinazoweza kupelekea mtoa huduma kufungiwa kutoa huduma.
Ni Imani yangu sasa utakuwa umepata uelewa angalau wa vigezo gani
vinatumika kufungia kampuni kutoa huduma. Kwa maelezo Zaidi maafisa wa
SUMATRA wataongezea ufafanuzi.
RSA TANZANIA
USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE.
Toa Maoni Hapa Chini