|
Mwl Tuntufye Mwakyembe |
Ni
mpango wa Mungu kabisa kuwa tuishi maisha ya mafanikio
ukisoma katika 3Yoh 1:2 anasema “Mpenzi
naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile
roho yako ifanikiwavyo.”
I.
Mungu amekusudia tufanikiwe Rohoni
II.
Mungu amekusudia tuwe na afya njema
mwilini
III.
Mungu amekusudia tufanikiwe katika
mambo yote
Yafuatayo
ni mambo 16 ya kuzingatia
a)
Jifunze kujikubali wewe mwenyewe na
umshukuru Mungu.
Zab
139:14 anasema “Nitashukuru
kwa kuwa nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, na nafsi yangu yajua sana”
b) Jifunze
kujiona unafaa, hata kama watu na mazingira yanakuonyesha haufai – maana wewe ni
ukuhani mteule
1
Petro 2 :9 anasema “Bali
ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya
Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita”
c) Jifunze
kuyakubali mapungufu yako au madhaifu yako maana kila mtu anayo yake na hayo
mapungufu yako/ madhaifu, ndio
yanayokufanya kila siku uone sababu na umuhimu wa kuusogelea Msalaba wa Yesu
ili upate msaada
2korintho11:9-10
Anasema “Nae akaniambia neema yangu
yakutosha maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu
wangu kwa furaha nyingi ili uweza wa Kristo ukae juu yangu kwa hiyo napendezwa
na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo
maana niwapo dhaifu ndipo ninapokuwa na nguvu.”
d) Kaa
na watu wenye hekima, chunga sana aina
ya marafiki unaokuwa nao, kaa na wale wanao kuelewa, kukutia moyo na kuchukuliana na mapungufu yako ogopa kuwa rafiki wa wapumbavu wasio na muelekeo chanya maana ni hakika
utaumia.
Mith
13:20 anasema “Enenda
pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima, bali rafiki wa wapumbavu
ataumia”
e) Hakikisha
unayo maono
Mithali
29:18 anasema "Pasipo
maono watu huacha kujizuia…” Maono yatakusaidia kuishi maisha ya
kuwa na mipaka, maisha ya kuwa na hofu ya Mungu, maisha ya kujizuia kufanya
baadhi ya vitu, maisha ya kujizuia kushiriki baadhi ya mambo kwa manufaa yako
ya baadae.
f) Jiwekee
mipango ya namna ya kuyafikia maono yako ukijua wazi kuwa Mungu anakuwazia
mawazo mema, kwa ufupi anasaport mipango yako ya mafanikio
Yeremia 29:11
anasema “Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya
amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho”
g) Kila
siku tafuta kufanya vitu vinavyokuongezea thamani (
Mungu anakutazama kama mji wenye Boma alafu anakutazama kama chombo
kikali kipya)
Yeremia
41:15 anasema “Tazama
nitakufanya kuwa chombo kikali kipya cha kupuria, chenye meno; utaifikicha
milima, na kuisaga, nawe utafanya vilima kuwa kama makapi.”
pia ukisoma katika Yeremia 1:18 anasema
“Maana, tazama, nimekufanya leo kuwa mji
wenye boma, na nguzo ya chuma, na kuta
za shaba, juu ya nchi yote…” kumbuka
hili siku zote kuwa Mungu anakutazama kama chombo kipya, tena anakutazama ka
mji au nguzo ya chuma na kuta za shaba hivyo basi thamani yako kwa Mungu ni
kubwa sana, siku zote jione hivyo na utafute kujiongezea thamani kwa Bwana.
h) Amini
kuwa ni Mungu peke yake ndie anayeweza
kukufanikishia njia yako na kuwa pasipo yeye wewe huwezi kufanya neno lolote
Yoh
15:5b anasema “Maana
pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno
lolote.” Pia unaposoma Mith 3:5 anasema Mtumaini
Bwana kwa moyo wako wote , wala usizitegemee akili zako mwenyewe
i) Amini
kwamba uko duniani kwa ajili ya kusudi lake maalumu, kazi maalumu na kwa kipndi maalumu,
hii tunaipata katika
Waefeso
1:11
anasema “Na ndani yake sisi nasi
tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye.”
j) Elewa
kuwa unao mchango fulani katika kuifanya dunia iwe mahali bora zaidi pa watu
kuishi kupitia karama na vipawa ambayo
Mungu ameweka ndani yako, Hivyo usiache kutumia vipawa na karama ulizo nazo kwa
ajili ya ufalme wa Mungu
2Timoth 1:6 anasema “ Kwa sababu hiyo nakukumbusha , uichochee karama
ya Mungu iliyo ndani yako…”
k) Jifunze
kuwajibika na kufanya kazi ambayo Mungu
amekupa kwa bidii
Muhubiri
9:10
anasema “Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako;
kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa , wala hekima, huko kuzimu
uendako wewe”
l) Amini
kuwa ndani yako kuna uwezo wa kufanya mambo yote katika kristo Yesu
Filipi 4:13 anasema “Nayaweza mambo yote
katika yeye anitiaye nguvu.
m) Jifunze
kufanyika Daraja ili watu wengine waweze
kupita na kuelekea mafanikio yao, siku zote ona kwamba ni wewe unayetakiwa
kuwarithisha watu mafanikio ambayo Mungu amewakusudia.
Yoshua
1:6
anasema “Uwe hodari tu na moyo wa ushujaa, maana ni wewe
utakayewarithisha watu hawa nchi hii
niliyowaapia baba zao kwamba nitawapa”
n) Amini
kuwa Mungu amehaidi kukurithisha Mali na kuijaza hazina yako
Mithali
8:21
anasema “Niwarithishe Mali wale
wanipendao, tena nipate kuzijaza hazina zao”
o) Jifunze
kuwa mvumilivu na mwenye subira maana baadhi
ya mambo hutokea katika majira na
nyakati ambazo ni maalumu kwa Mungu.
Rumi
4:20 anasema “ Lakini
akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa
kutokuamini,
bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu; huku akijua hakika kuwa Mungu aweza
kufanya yale aliyoahidi”
p) Jifunze
kuona positive, ona mambo mema, ona ukifanikiwa, ona ukisonga mbele kataa kuona
mambo mabaya na ya kukuvunja moyo hii ni
kutokana na kuwa unavyoona ndivyo
unavyokuwa
Mithali 23:7 anasema “Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo
alivyo.
Yatumie mambo
haya kama Muongozo wako wa kuyafikia yale ambayo unayatarajia kutoka kwa
Bwana, sisi tunakutakia Baraka za Mungu katika Maisha yako.
Kwa mawasiliano zaidi.
+255767629562
Arusha. Tanzania