UWANJA UNAOWAUA WAHUBIRI TANZANIA WAPATA TIBA
Yawezekana umewahi kusikia maneno zamani au hata leo kwamba kuna eneo
fulani haliingiliki kirahisi kwasababu ya matambiko ama nguvu za giza
zilizoko katika eneo hilo ama mkoa huo. Moja ya maeneo hayo amabyo
yamepata tiba ni Handeni huko mkoani Tanga ambako timu ya The Voice of
Hope ministries chini ya mkurugenzi wake mchungaji Peter Mitimingi
wanawasha moto wa injili.
 |
| Baadhi ya umati wa watu waliofika mbele kumkabidhi Yesu maisha yao. |
Chini ni maelezo ya mchungaji Mitimingi akieleza kuhusiana na eneo wanapofanya mkutano kwamba wahubiri watatu waliaga dunia....
Hapa ni Handeni Tanga wa Wazigua
Uwanja huu unahistoria ya kuangusha wahubiri jukwaani na kufa.
Wameshakufa wahubiri 3 na maagano yamefanyika kwa miaka mingi kwamba
hapa kijijini hakutakuwa na kuristo wala mtu yeyote kuhubiri na atakaye
thubutu atakwenda chini futi 6. Tuliposikia hayo majigambo ya adui
tukasema lazima tupeleke kikosi cha makomandoo wa Yesu kupitia VHM
kwenda kumaliza mzizi wa fitina.
Tulipoanza tu wazee walitengeneza
mvua ya radi uwanjani kumdondosha mwinjiristi lakini kama Bwana Aishivyo
leo ni siku ya 9 tunakandamiza kwa kwenda mbela na mavuno sio ya
kubahatisha HADONDOKI MTU HAPA WALA HAFI MTU HAPA WALA HAKUNA CHA MAFUA
WALA NINI chezea nguvu za Yesu aliye hai.
 |
| Wakina mama wakimsifu Mungu licha ya mvua kubwa. |
 |
| Makomandoo wa Yesu wakifanya kazi ya kumtukuza muumba wao. |
 |
Hata watoto hawakutaka kupitwa na neema ya neno la Mungu.
|
 |
| Mchungaji Peter Mitimingi akicheza mbele ya Mungu wake. |
 |
| Moja ya hirizi iiliyosalimishwa na watu waliokuwa wakitenda vitendo vya kishirikina | |


Source
Toa Maoni Hapa Chini