Zoezi hilo liefanyika katika Chuo cha
Biblia kilichopo Itende jijini Mbeya ambapo Askofu huyo katika kuonesha
uzinduzi na yeye alichangia.
Akizungumza na waandishi wa habari mara
baada ya kuchangia, alisema Wachungaji wameona wachangie damu kutokana na
upungufu na mahitaji yanayoikabili Benki ya damu salama.
Alisema katika zoezi hilo ni wachungaji
800 ambao ni waangalizi wa kanisa ndiyo watakaoanza kuchangia na kufuatiwa na
wachungaji wote kutona nchi nzima ambao watakuwepo mkoani Mbeya kwenye
maadhimisho ya miaka 75 ya TAG.
Askofu alisema uchangiaji damu huo ni
moja ya adhima ya kanisa ili kukabiliana na upungufu wa damu unaokikabili kituo
cha damu salama kanda ya Nyanda za juu kusini hivyo litaendeshwa kwa muda wa
siku tatu kuanzia Julai 10 hadi 12,mwaka huu ili kukamilisha wachungaji zaidi
ya 1000 nchi nzima.
Alisema kama kanisa na Viongozi wameguswa
na tatizo la upungufu wa damu katika mahospitali kutokana na watu kupata ajali
kila siku, wanawake kupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua pamoja na watoto
ndiyo maana wakaona ni vema wakaonesha mfano wa kuchangia damu.
Aidha alitoa wito kwa viongozi wengine wa
dini bila kujali itikadi zao kuchangia damu popote pale walipo ili kuokoa
maisha ya Watanzania wenye mahitaji kwa kuwa damu haiuzwi na hakuna kiwanda cha
kuzalisha zaidi ya mtu kujitolea.
Kwa upande wake Afisa tabibu wa Damu
Salama kanda ya Nyanda za juu kusini yenye makao makuu katika Hospitali ya
Wazazi Meta jijini Mbeya, Alex Kasimba,alisema ni kweli kuna upungufu mkubwa wa
damu katika Benki yao.
Alisema kwa takwimu za Mwaka jana damu
iliyokuwa ikihitajika ni chupa 28000 lakini Benki ilifanikiwa kukusanya chupa
19000 sawa na asilimia 68 hivyo kuwa na upungufu wa chupa 9000 sawa na asilimia
32.
Alisema hata mwaka huu wanauhitaji wa
kiasi kama hicho ili kuweza kuziba pengo la upungufu wa damu ambapo kupitia
maadhimisho ya Miaka 75 ya TAG wanatarajia kukusanya zaidi ya Lita 400.
Aliongeza kuwa taasisi za kidini kama
TAG, Sabato, Waislam na taasisi za elimu kama Shule za sekondari na vyuo ndiyo
wanaojitolea kwa wingi damu tofauti na wananchi wa kawaida.
Credit to; Mbeya yetu
JOSEPH MWAISANGO
MWANDISHI MKUU
j.mwaisango@tonemg.com
+255 754 374408
|